Je, Rais Samia anastahili tuzo ya Mo Ibrahim?

Je, Rais Samia anastahili tuzo ya Mo Ibrahim?

MWATANI

Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
45
Reaction score
44
Salaam Wana JamiiForums,

Naanza andiko hili fupi kwa marejeo ya usemi usemao " Myonge Myongeni lakini haki yake mpeni" ni usemi wenye maana Pana kimantiki, Sasa ni miaka miwili ya Rais Samia tangu ashike hatamu ya uongozi wa nchi, amefanya mengi hata ambayo wahafidhina ndani ya CCM na nje ya chama hawakutarijia.

Demokrasia na mifumo ya utawala Bora imeshika Kasi, uhuru wa maoni, na uhusiano chanya wa kidiplomasia unavutia na kufungua fursa za kiuchumi, Vyama shindani au upinzani wanapumua katika siasa za uwiano sawia.

Aidha Rais Samia ni binadamu inawezekana anayo mapungufu yake kama walivyo binadamu na watawala wengineo, lakini hadi sasa Rais Samia anastahili kupewa alama za utendaji bora zisizopungua 95% Kwa uongozi uliotukuka na wenye dira ya kitaifa na kimataifa. Je, anastahili kutambuliwa Kwa uongozi Bora na kupewa tuzo ya Mo Ibrahim?

Nawasilisha.
 
Nikajua Lucas mwashambwa kumbe daah haya sawa Mama Samia najua anapita humu ataona atakufikiria kwenye teuzi zijazo, umesahau kuweka namba yako ya simu lakini
 
Kwa Rais kutoka Bongo, kuipata hiyo tuzo; ifanyike kazi ya ziada. Siyo kwa sababu tu ya maridhiano na akina Mbowe, halafu ndiyo iwe kigezo cha kupewa hiyo tuzo.
 
Back
Top Bottom