6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Raisi wangu, kwa heshima na taadhima napenda kukusalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mama kuna ule msemo unaosema kuwa "ukicheka na nyani shambani mwisho wake utakuja vuna mabua"
Yanayoendelea nchini kupitia hao panya wa barabarani bila shaka unayajua, lkn inaonesha bado haujawa serious kuyakomesha au kuyadhibiti kwa vile hao panya wa barabarani wanagusa raia wa kawaida na sio viongozi wa serikali au familia za viongozi hao.
Kila mtu ukiwemo wewe mwenyewe unafahamu fika kwamba haya matukio ya panya wa barabarani miaka 5 iliyopita yani 2016 hadi 2020 au 2021, chini ya uongozi wa raisi Magufuli na mkuu wa mkoa wake Paul Makonda yalikuwa nadra sana kutokea.
Yani yameanza kushamiri zaidi sasa hivi baada ya raisi Magufuli kufariki na mkuu wa mkoa kuwa nje ya mamlaka.
Sasa mpaka hapo ushajua ni nani na nani waliokuwa kiboko ya hao vijana mpaka wakashindwa kufurukuta miaka hiyo.
Cha kufanya kwa sasa ni kuweka siasa pembeni na kumrudisha kijana Makonda haraka iwezekanavyo aje akusaidie kazi ya kurudisha amani, usafi na usalama katika jiji kubwa la Dar es salaam. Otherwise ukidharau utakuja kujuta baadae (2025) maana wananchi hawatokuwa tayari kumpa kura mtu asiejali usalama wa maisha yao, pamoja na mali zao.
Please tunaomba utafakari kabla ya hatari. Bila hivyo utakuja kujilaumu baadae.
Kazi "ya kupambana na panya road" iendelee.