Je, Rais Samia unaujua msemo huu?

Je, Rais Samia unaujua msemo huu?

Panya Roads ni matokeo ya unemployment na poverty mkuu, tutibie ugonjwa sio dalili zake, vijana hawa tunaishi ishi nao majumbani mwetu hawatoki kwenye sayariya Mars, president Nyerere (rip)aliliona hili na alipambana na kuwapa uchaguzi ingia kwenye vijiji ili ulime au mitaani huku utahangaika,sasa unawachoma moto na hujawapa alternatives ya kujiajili huku sio kutibia ugonjwa we need a political will wa kuwafanya vijana wetu to think out of box 🗃, kilimo na ufugaji ndiko kunaweza kutuzalishia ajira zaidi kwa vijana wetu, elimu ya uzazi ipewe umuhimu, hatuwezi uchumi ukue kwa 5% na tuongezeke kwa more than 3%,it's craze kikawaida Tanzania ilitakiwa iwe na raia kama 23M,but now tuna 60M!,tunaishi in a timing bom
Hapa naona kama vile umeingiza siasa mkuu. Hivi ni kijana gani amezuiwa kujiajiri mwenyewe pale ambapo hakupata nafasi ya kuajiriwa na serikali? Ni kijana gani aliezuiwa asirudi kijijini akalime nk?

Swala la ajira sio la Tanzania peke yake hata huko USA, Europe na Asia kuna jobless kibao achilia mbali hapa kwetu Afrika. Mbona ujinga ujinga wa aina hii hatuusikii kwengine?
 
Kwaiyo tanganyika kote makonda ndio kiongozi bora? Umetumia mbinu yakijinga sanaa
Sio bora lkn ana uthubutu katika kulitafutia ufumbuzi tatizo. Tofauti na viongozi wengine wanaoshinda ofisini kusubiri mwisho wa mwezi msahara uingie bila kuutolea jasho.
 
Wanaume wengi wanakataa mimba, na wanawake wengi wanalea watoto katika mazingira ya shida, watoto wao wanaolelewa katika mazingira magumu. Hapa lazima panya road waongezeke.
Basi kama ni hivyo inahitajika plan B ili kudhibiti huu ujinga kuendelea.
 
Hao panya wako watamalizwa wote na hakuna atakayebakia hatammoja, watasakwa na kufuatwa Hadi shimoni waliko, Tanzania Ni Salama katika mikono ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
Unazungumzia usalama wa watu kukatwa katwa mapanga kila siku mpaka kupelekea juzi mtoto wa miaka sijui 8 tena wa kike kupoteza maisha kwa sababu ya majeraha ya mapanga au?
 
Daudi Albert Bashite, kijana asiye na vyeti, nihatari sana kuongozwa na mtu aliye forge vyeti
Wewe unaongozwa na vyeti au mtu makini?
Watanzania hawahitaji vyeti. Wanahitaji usalama na unafuu wa Maisha.
Aliyekuwa hana vyeti aliweza aliwadhibiti Panyaroads, lakini mwenye vyeti Panyaroads wanammudu.
Hapo sasa nani ni bora zaidi?
 
Tulijua kabisa hakuna kitu kinaitwa Panya Road wala nini. Mnavumisha uongo tu kwa maslahi mnayojua nyinyi ikiwemo kumhujum Rais Samia.

Kila anayekuja analeta nyimbo z Makonda.

Vyombo is watching you.

Mna creat chaos kwa jamii kwa propaganda za Panya road wasiokuwepo.

Kama ni uhuni wakabaji Dar walikuwepo, wapo na watakuwepo ktl miji yoote duniani hasa ya maskini.

Mbona mnataka kulifanya kama jambo jipya?
Wakati wa JPM Panyaroads hawakuwepo, ndugu.
Kwa nini iwe Leo?
 
Wewe unaongozwa na vyeti au mtu makini?
Watanzania hawahitaji vyeti. Wanahitaji usalama na unafuu wa Maisha.
Aliyekuwa hana vyeti aliweza aliwadhibiti Panyaroads, lakini mwenye vyeti Panyaroads wanammudu.
Hapo sasa nani ni bora zaidi?
Mtu anaepinga uongozi wa Makonda atakuwa ni miongoni mwa wavuta unga, wauzaji au kibaka.
 
Wakati wa JPM Panyaroads hawakuwepo, ndugu.
Kwa nini iwe Leo?
Uongozi wa sasa umeshindwa kabisa kuja na mbinu za kuwadhibiti hawa mbwa koko. Haiwezekani mtu aliefanya matukio ya kutisha kama hayo na muda mungine mpaka kuuwa, afu akifikishwa mahakamani anahukumiwa kwenda jela miezi 3 au sita. Na hapo hapo kuna wengine wanakubaliwa kuwekewa hadi dhamana huku serikali ikiangalia tu.
 
Sio bora lkn ana uthubutu katika kulitafutia ufumbuzi tatizo. Tofauti na viongozi wengine wanaoshinda ofisini kusubiri mwisho wa mwezi msahara uingie bila kuutolea jasho.
Hakuna mtu au kiongozi mwingine tanganyika nzima? Kwanini umempendekeza yeye?
 
Panya Roads ni matokeo ya unemployment na poverty mkuu, tutibie ugonjwa sio dalili zake, vijana hawa tunaishi ishi nao majumbani mwetu hawatoki kwenye sayariya Mars, president Nyerere (rip)aliliona hili na alipambana na kuwapa uchaguzi ingia kwenye vijiji ili ulime au mitaani huku utahangaika,sasa unawachoma moto na hujawapa alternatives ya kujiajili huku sio kutibia ugonjwa we need a political will wa kuwafanya vijana wetu to think out of box [emoji1003], kilimo na ufugaji ndiko kunaweza kutuzalishia ajira zaidi kwa vijana wetu, elimu ya uzazi ipewe umuhimu, hatuwezi uchumi ukue kwa 5% na tuongezeke kwa more than 3%,it's craze kikawaida Tanzania ilitakiwa iwe na raia kama 23M,but now tuna 60M!,tunaishi in a timing bom
Kwani wakati wa utawala wa Magufuli kulikuwa hakuna Unemployment?

Ninakubaliana na wewe kwamba ufukara wa mali,pia husababisha ufinyu wa fikra na hatimae kuzalisha mawazo mabaya ambayo huweza kumtuma ntu kufanya uhalifu kama njia pekee ya kujiponya(kwa mtazamo wake ambao sio sahihi pia).

Lakini tusihalalishe uhalifu kwa kuufanya kuwa ajira mbadala!
Huu utakuwa ni moja ya fikra mbaya kabisa kuwahi kutokea.

Kila jambo katika maisha linao mustakabali wake.

Huwezi kwenda kuchinja watu na ukishakamatwa na kufikishwa mahakamani ujitetee kwamba ni kwa sababu ya kukosa ajira.kwa vyovyote ni lazima utapatikana na hatia.na adhabu yake itachukua mkondo kulingana na uzito wa kosa kisheria.

Hapa nchini pamoja na kukumbwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
Lakini bado kuna fursa nyingi mbadala za watu kuweza kuzitumia na kuendesha maisha yao.
Japo kwa kipato cha chini.

Na hilo ni jambo ambalo liko wazi kabisa.
Kuna mambo mengi ya kuweza kufanya na kama Mungu akikuwekea mkono wake....wengine hubadili maisha yao kabisa.

Hatujawafikia kiwango baadhi ya majirani zetu wa nchi za kiafrika,ambako hali ni mbaya sana kama Ethiopia ,Somalia,Eritrea na hata DRC na Burundi kwa uchache tu.

Ambako wamefikia viwango vya kuhatarisha maisha uao kwa kuzikimbia nchi zao,kwa baadhi ya njia ambazo ni hatarishi kabisa.
Lakini hawana namna ingine zaidi ya hiyo.
Ushahidi upo maana tunawaona kila siku wakikamatwa kwenye malori,tena yasiyostahili kwa kusafirishia Binadamu.

Pia ikumbukwe kwamba hawa Panya Road wengi,ni vijana au watoto ambao bado kwa umri wao wanapaswa kuwa mashuleni na vyuoni.

Kuna mahali fulani ambako kuna tatizo la kimalezi na uangalizi kwa watoto wetu kwenye hatua za mwanzo kabisa.

Tunapaswa kutimiza wajibu wetu kama wazazi,kabla ya kuirushia serikali lawama ambazo saa ingine zinatuhusu sisi wenyewe.
 
Wanaume wengi wanakataa mimba, na wanawake wengi wanalea watoto katika mazingira ya shida, watoto wao wanaolelewa katika mazingira magumu. Hapa lazima panya road waongezeke.
Unamaanisha kuwa panya road ni watoto wa singo mamas?
 
Hakuna mtu au kiongozi mwingine tanganyika nzima? Kwanini umempendekeza yeye?
Kwa vile yeye huwa ana uthubutu wa kupambana na wapumbavu wa aina hii. Wengine maneno mengi afu vitendo zero.
 
Back
Top Bottom