Je, Rais wa Tanzania ipo siku atakuwa na la Kujibu kwenye mamlaka zijazo juu ya Kupotea kwa Ben Saanane?

Kanywe damu yake tutolee ujinga hapa
Wewe PIMBI jaribu kuwa na UTU hata mara moja moja, huyo aliyepotezwa ni Binadamu sio mnyama. Hebu weka picha kama angekuwa ni ndugu yako, mwanao, kaka, mdogo wako n.k
Si kila wakati wa kutumia MASABURI kujenga hoja ama kutoa maneno ya kuudhi na kejeli kwa wengine. MUNGU hadhihakiwi na malipo ya ubaya wowote ule ni hapa hapa duniani. Sawa sawa?
 
My suspicion from day one.
OK hilo linawezekana, hapo ndio inapodhibitisha kuwa tuna serikali dhaifu katika uchunguzi, iliyo jaa upumbavu katika ushabiki na watendaji wa hovyo!
Intelijensia watambayo nayo kila siku kuhusu kuzuia mikutano ya ndani na nje wameshindwa kubaini walivyo mpoteza mwanachama na kuchukua hatua ambazo zingewamaliza kuliko kukazania kubambika risasi iliyo muua Akwilina ambayo hata kichaa anajua kuwa ni polisi?
Pascal Mayalla naye anasema could be inside job! kweli degree yake moja (maana wenye NNE ndio wenye akili-Mwakyembe) ya sheria ndio inaweza kumtuma kutamka hayo?
Chadema waue mtu wao halafu file LA polisi lifungwe bila kula kichwa cha mtu?
Tunaposhauri tuwe na hekima maana tunaowashauri wengine wana digrii nne (joke).
 
Possible naweza nikaamini wametulizwa chini kwa chini maana wapo kimya tu.
Hayo ni matusi kwa wale wazee. Mnategemea wangefanya nini zaidi ya kumshukuru Mungu na kukubali yaishe tuu? Kupewa mshiko kwa ajili ya mwanao ambaye hujui yuko wapi, anahali gani?! Sio vizuri!
 
Unalielezeaje lile la Kubenea na Komu kupanga kumdhuru Jacob! Was it not an inside job?!
 
Kwenda zako huko kichwani hamnazo kwani JPM ni personal boardgard wa huyo mtu?
Nakumbuka sometimes in 1979 Iddi Amin akiwa uhamishoni Saudi Arabia alimwambia mwandishi wa habari wa Reuters aliyekuwa akimuhoji kuwa, "I could not be everywhere to protect everybody".

NB: Iddi Amin alifariki nchini Saudi Arabia mwaka 2003 kwa Kidney Failure na kuzikwa huko huko na kuthibitisha ule ukweli kuwa "No one is immortal".
 
Possible naweza nikaamini wametulizwa chini kwa chini maana wapo kimya tu.
Walipewa mil 130, wanawaangalia tu mnavyojifanya mna uchungu kuliko wao, we ushawai kuwasikia popote wakiomba msaada wa vyombo vya dola kuhusu mtoto wao au kuulizia imefikia wapi,
 
Nimeipenda slogan moja ^ wazaz mshitaki kwa mizimu^ wengine ngoja tusifu na kuabudu malaika wetu maisha ya duniani matamu ila changamoto sana.
 
Ipo Siku ingawa yeye kwa sasa haoni wala kuwaza kuwa kuna siku ataondoka madarakani kafungwa macho. Na alivyo muaoga natalia na kusaga meno. Ooh watanzania nimewanunulia mandege na kuwajengea mabarabara leo ndio unaifanyia hivi. Hiyo siku inakuja
 
Unalielezeaje lile la Kubenea na Komu kupanga kumdhuru Jacob! Was it not an inside job?!
Kwani makosa ya wanachama wawili dhidi ya mwanachama mwenzao utaitaje inside job? Kwani ni mipango ya chama?
Ni sawa na uhalifu wa wa Tanzania wawili dhidi ya Mtanzania mwingine uite inside job kwa serikali.
 

Kama ingekuwa ni inside job basi uchunguzi ungefanywa kwa kasi ya bombadia, kwa urefu wa SGR na ukubwa wa Stieglers
 
Atayaandika kwenye kitabu chake baada ya kustaafu

Damu za watu huwa hazipotei bure lazima atalipia maisha ya watu waliouwawa na mamlaka yake
 
Kwani makosa ya wanachama wawili dhidi ya mwanachama mwenzao utaitaje inside job? Kwani ni mipango ya chama?
Ni sawa na uhalifu wa wa Tanzania wawili dhidi ya Mtanzania mwingine uite inside job kwa serikali.
Now you're talking. Safi sana.
 
Walipewa mil 130, wanawaangalia tu mnavyojifanya mna uchungu kuliko wao, we ushawai kuwasikia popote wakiomba msaada wa vyombo vya dola kuhusu mtoto wao au kuulizia imefikia wapi,
Nani aliwapa hiyo hela na kwa nini. Huyu Beni labda hata alibonyezwa kabla na akasepa zake ughaibuni.

Kweli hii serikali inaweza kufanya upumbavu mkubwa hivyo, wamteke mtu na kwenda kumuua wakati wakijua wazi kuwa hawatakaa madarakani siku zote na hata wasihofie mabaya yaliyowahi kuwapata madikteta mbali mbali duniani.
Sijui, but it's difficult to comprehend..
 
OK hilo linawezekana, hapo ndio inapodhibitisha kuwa tuna intelijensia kila siku kuzuia mikutano ya ndani na nje wameshindwa kubaini na kukazania kubambika risasi iliyo muua Akwilina ambayo hata kichaa anajua kuwa ni polisi?
When you don't know for sure who is who, you can't rule out any possibility, ila kwenye hili la Akwilina, mimi nilisema wazi wauaji ni polisi wetu

P
 
Kama ingekuwa ni inside job basi uchunguzi ungefanywa kwa kasi ya bombadia, kwa urefu wa SGR na ukubwa wa Stieglers
Hawana lead ya pa kuanzia!, ndio maana hata uchunguzi wa shambulizi la Lissu bado haujaanza kwasababu wanamsubiri Lissu na dereva wake, wawahoji ndipo waanze uchunguzi.
P
 
Inaonekana una ufahamu na mahali alipo Ben na kuwa yu hai; tusaidiie tafadhali hata Kama unahitaji malipo tutachanga, mbona Lisu tulichanga!!!?
Kubenea alisema Ben yupo mahali salama salmini, una mashaka na Kubenea?!
 
Hawana lead ya pa kuanzia!, ndio maana hata uchunguzi wa shambulizi la Lissu bado haujaanza kwasababu wanamsubiri Lissu na dereva wake, wawahoji ndipo waanze uchunguzi.
P

Hawana lead pa kuanzia?

Huu ni ushahidi kuwa uwezo wao mdogo kwa hivyo basi wangekuwa na nia ya dhati ya kutendea haki hawa wahanga basi wangeshirikisha wenye ujuzi wa mambo ya uchunguzi wa kimataifa, wenye uzoefu zaidi yao, vifaa zaidi yao na uwezo zaidi yao.

Tanzania kuomba msaada wachunguzi wa nje siyo jambo geni, Tumewahi kuomba wachunguzi wa kimataifa kwenda kuchunguza mauaji ya mapadri huko Zanzibar na ripoti ipo kwa wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…