Mimi naamini kabisa kama Mchungaji Mtikila angekuwa bado yupo hai na mwenye afya njema, serikali ya Magufuli ingekuwa ishapelekwa mahakamani siku nyingi sana.
Naamini kabisa angekuwa keshaenda mahakamani kuhusu bunge kutoonyeshwa live. Angekuwa keshaenda kuhusu vyama vya siasa kupigwa marufuku kufanya shughuli za kisiasa.
At least hayo mawili, naamini kabisa asingeishia kunung’unika tu huku uraiani.
Whether angeshinda au la, that’s beside the point.
It’s just the principle of it.
Halafu ujue mahakamani, hususan mahakama za juu, kuna majaji wanaweza kuwa wako tayari kutoa just rulings zitakazopingana na serikali.
Hili tushaliona awali.
Lakini majaji hao hawawezi juqnzisha kesi wenyewe, inabidi jesi zianzishwe, pengine ziletewe figisu za kisiasa, zikatiwe rufani, zifike mpaka juu huko.
Hizi kesi kubwa nazo zina tabia ya kuwahukumu wahukumu, maana yake, the judges themselves will be on trial, watu watawaangalia wanakwenda upande wa haki au upande wa kutetea serikali?
Na majaji wengine hawatataka kuchafuliwa heshima zao, kama serikali inakosea watasema.
Sasa kama kesi hazianzishwi, wao kama majaji inakuwa vigumu kutoa rulings kwa kesi ambazo hazipo.
Tunahitaji kuanzisha kesi zaidi.
Hata zikiletewa figusu tujue nani kasimama wapi. Tujifunze pa kujipanga vizuri zaidi.