SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Unajua humu ndani tunachukuliana poa sana labda kwa sababu ya hizi ID feki. Kuna madogo ambao wanatakiwa wakupe heshma iliyotukuka ila kwa kuwa tunakutana katika nyuzi za soka tunachukuliana wote hamnazo.
Miaka fulani nikiwa bado bwa mdogo nilishajijengea heshima fulani mitaani ya kusakata kandanda. Kulinganisha na umri wangu, nilikuwa serious sana na mpira. Ndiyo maana huwa nabaki nacheka nikianza kubishana na baadhi ya watu kuhusu mambo ya soka halafu unasikia wananiambia "mpira haujui". Hahaha! Nilikuwa na kitabu changu naweka kumbukumbu za mechi nilizocheza na magoli niliyofunga. Watu tumeanza kufuatilia mipira ya South Amerika huko na Italy kitambo sana na siyo kwenye magazeti, nia kuiba maujuzi na mautundu na kuupeleka uwanjani.
Muda fulani ukafika nikawa kama nimestaafu hivi pamoja na kwamba umri wangu ulikuwa bado mdogo. Pia nikawa kama nimeanza kuwa serious hivi na mambo ya shule.
Mzee mmoja akanifuata akaniambia amenifuatilia kwa muda mrefu na anauelewa umahiri wangu dimbani. Akaniomba nifundishe madogo ambao kiumri hatukuwa tunazidiana sana. Kwa heshma yake nikachukua hilo jukumu. Kulikuwa na watoto wasiopungua 20 nikaanza kuwafundisha A, B na C za soka. Nilikuwa nachukua hadi vitabu vya kufundishia mifumo ya soka nasoma ili kujiongeza, halafu naenda kuwapa madini madogo. Masuala ya "total football" watu tunayajua kitabuni hadi kivitendo. Kitaa nilikuwa legend halafu nilikuwa hata siringi.
Nimefuatilia historia ya hapa na pale ya Rais wa Yanga, Hersi Said. Kwa taarifa nilizopata za alipokuwa anaishi, kuna uwezekano wa asilimia 85 hadi 90 kuwa alikuwa ni miongoni kwa hawa madogo.
Vijana wengi wa maeneo alipokulia huyu Rais wa Yanga nimecheza nao sana mpira. Tulikuwa timu tofauti ila tumekutana katika mechi nyingi za kiushindani na wengi walikuwa washkaji. Majina ya wengi yamenitoka ila baadhi naweza kuwataja hapa ili kuhakiki ninayosema.
Kuna watu unaowaheshimu wanantambua na wananiheshimu.