Je, ratiba ya raundi ya kwanza mtoani CAF champions league itabadilika

Lukub

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
3,622
Reaction score
4,100
Kule EGYPT team zilizofuzu Club bingwa ni ZAMALEK na PYRAMID japo ligi haijaisha huku umebaki mchezo mmoja ZAMALEK ana point 77 huku PYRAMID ana point 71 , AHLY point 67.

Kwenye RATIBA ya club bingwa tayari AHLY alipaswa kucheza raund ya pili ya club bingwa Sasa atapaswa kwenda Shirikisho wakati, PYRAMID alipaswa kucheza raund ya pili Shirikisho anakwenda champions league,na anapaswa apangiwe team ya kucheza nayo maana hayupo kwenye team Tano zinazosubiri round ya pili.

Wajuzi hili limekaaje? Pia ZAMALEK atahitaji kucheza round ya pili maana kwa rank yeye anapoint sawa na mazembe na nafasi hiyo ya team ya Tano imebaki wazi baada ya AHLY kuangukia Shirikisho.
 
caf wafate kanuni zao kwa kila timu ipate haki yake, kama kanuni inasema wa3,4 kwenye ligi ni confederetion bas isimamiwe.

Anyway uko ni egypt , ligi yao inautaratibu wao
 
caf wafate kanuni zao kwa kila timu ipate haki yake ,kama kanuni inasema wa3,4 kwenye ligi ni confederetion bas isimamiwe,
Anyway uko ni egypt , ligi yao inautaratibu wao
Kanuni ipo wazi wa kwanza na wa pili champions league wa tatu na wa nne Shirikisho.
 
Wale jamaa nasikia walipeleka msimamo wa first round ya league na PYRAMIDS wameenda FIFA kudai haki yao maana al ahly yupo Caf champions league wakati PYRAMIDS yupo caf confederation wahuni sana jamaa wa Egypt wanaibeba al ahly wazi wazi.
 
Baada ya Ahly kupoteza Leo ndio imempatia nafasi ya Pyramid kuwa wa pili ,kama wamepeleka ZAMALEK na Ahly Kwa mazoea mwaka huu kimeumana ,wanaume wamepambana .
 
alhaly anaenda kucheza CAF champion siyo shirikisho mpira wa egypt ni mauza uza eti pyramid wanampeleka shirikisho na alhaly anaenda CAF champinons
 
Ahly wamemzingua Pitso mpk kaamua kujiondoa, baada ya hapo wakaanza kupoteza muelekeo wa mbio za ubingwa na wameukosa na nnazidi kuwaombea waondolewe CAF Champions lg waende huko Shirikisho

Pyramids wakaze hvyo hvyo madai yao huko FIFA
 
CAF huwaachia mashirika wanachama kutoa wawakilishi kwa kutumia kanuni na vigezo vyao hayo wanachama. Shirikisho la soka Misri wakaamua kupeleka timu kulingana na msimamo wa raundi ya kwanza kwavile walijua ligi yao bado sana kuisha na CAF wanahitaji majina ya timu wakilishi.

Ila kinachonishangaza ni ligi kuendelea wakati tayari wameshatuma wawakilishi CAF
 
Ahly wamemzingua Pitso mpk kaamua kujiondoa, baada ya hapo wakaanza kupoteza muelekeo wa mbio za ubingwa na wameukosa na nnazidi kuwaombea waondolewe CAF Champions lg waende huko Shirikisho

Pyramids wakaze hvyo hvyo madai yao huko FIFA
Kwahiyo pyramid amemshatak nani Fifa??? , naona kosa LA chama cha Moira misri
 
Geita Gold walikuwa waje kucheza na Pyramid Shirikisho, CAF wanaweza kuamua kuitoa Pyramid waiweke Ahly maisha yaendelee.
 
Kwa kutumia kanuni zao, kama ligi itachelewa knisha kwa kigezo chochote, watatumia washindi wa mzunguko wa kwanza, Al Ahly amebebwa na kanuni zao za mchongo.
 
Hapo ni jambo moja nadhani ni kuwa aliyetakiwa kucheza na Alahly sc atacheza na Pyramids kwenye Caf champions league na yule aliyetakiwa kucheza na Pyramids kwenye kombe la shirikisho atacheza na Alahly
 
Pyramids hata waende fifa hakuna kitakachobadilika,chama cha mpira ndio wanaosikilizwa
Kwahiyo pyramid amemshatak nani Fifa??? , naona kosa LA chama cha Moira misri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…