Je Serikali imabariki Dar es Salaam Secondary kufukuza au kuhamisha wanafunzi wanaopata daraja la IV katika mitihani ya ndani?

A

Anonymous

Guest
Naomba mamlaka zinazoshughulika na elimu kuanzia Afisa elimu jiji LA Dar es salaam, Afisa elimu mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa elimu, mtupatie majibu sahihi ya hiki kinachofanyika Dar es salaam secondary na baadhi ya shule za serikali kama Pugu secondary na kwa shule za msingi kinatokea kwa shule kama Mikongeni, Olympio na Diamond, kama kipo katika miongozo ya serikali au watu binafsi wameamua kwa maslahi yao binafsi na kuleta kero kwa wazazi na wanafunzi.

Ninaandika kama mzazi ambae nilimkabidhi mtoto wangu katika shule ya Dar es salaam sekondary miaka mitatu iliyopita akiwa na Division 1, katika mtihani wa mwisho wa mwaka, mtihani huu kwa uelewa wangu ni wa wilaya. Akiwa kidato cha pili FTNA alifaulu kwa daraja la tatu. Kinachonishangaza baada ya kufungua shule nimeitwa na kuambiwa mtoto wangu anapaswa kuhamishwa kwenda shule zingine kwa gharama zangu, kwa kosa la kupata daraja la nne.

Kama mzazi nimejiuliza kwa kadri ya uelewa wangu nikiwa kama mdau wa elimu.
1. Je anapofeli mwanafunzi mtuhumiwa pekee ni mwanafunzi? Kwa ni wasihamishwe walimu waliompatisha division 4 mwanangu Hali ya kuwa walimpokea akiwa na div 1?
2. Je ni kweli kuna miongozo ya kiserikali div 4 hawatakiwi kusoma katika shule za serikali?
3. Ni kwa nini serikali inazuia shule za binafsi kuwaondoa wanafunzi wanaoshindwa mitihani ya ndani?
4. Je mtihani uliopima mwanafunzi huyu ulikuwa na video na sifa za kitaifa?

Ninaomba mamlaka husika ilitolee ufafanuzi ili kama lipo kisheria tuwaondoe watoto wetu pasipo kuleta usumbufu kwa shule husika. Sijaandika hapa lengo la ufitini ikibidi mamlaka zizichunguze shule husika juu ya mienendo hii ya kuwaondoa wanafunzi mashuleni kwa kutofikia madaraja wanayoyataka.
 
Mwanao kilaza anachafua jina la shule.

Wamechoka kuchafuliwa jina hivyo wameamua kuwaondosha wanafunzi wote wazembe wasije wakachafua shule kwenye mitihani ya mwisho ya kujikimu.
 
Back
Top Bottom