Je, Serikali imeamua kugawana 50/50 tozo za simu na Wamiliki wa mitandao?

Unachosema Mkuu ni sahihi kuhusu maboresho ya huduma za simu hadi vijijini, ndiyo maana Serikali ya awamu ya nne iliwekeza kwenye Ujenzi wa Mkongo wa Taifa.

Suala la kodi halikwepeki kama tunataka kupata maendeleo na kupunguza Utegemezi kwa Nchi wahisani.

Muhimu hii kodi ya simu ingekuwa fixed amount kama ni shilingi 100 iwe hivyo kwenye kila muamala sio sahivi kila muamala unakodi yake imefikia muamala unakodi ya shilingi 12,000 plus. Haya ni maumivu kwa Wananchi.

Ila suala la Kodi kama Nchi, halina mbadala. Lazima tulipe kodi Kama tunataka maendeleo na kuondokana na Utegemezi.
 
Angalau sasa kampuni za simu mmeamua kutoka hadharani kulipinga hili. vinginevyo muda utaamua kama kweli mtaweza kuendelea kutoa huduma katika mazingira ya kinyonyaji kama haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…