Je, Serikali imeamua kugawana 50/50 tozo za simu na Wamiliki wa mitandao?

Je, Serikali imeamua kugawana 50/50 tozo za simu na Wamiliki wa mitandao?

Wafanya biashara naona watakuwa na tax holiday of some kind!!
! Wavuja jasho wakamuliwe hadi matone ya damu yatoke!!
 
Mungu ametupatia akili hivi hakuna namna Bora ya kuepuka kufanya transaction kupitia mitandao hii? Hapa ndiyo muda wa kuwasikia vijana tuliowasomesha kwa Kodi zetu.
Kukwepa hakuna maana na hakuna namna ya kukwepa zaidi itakuwa crime, swala la msingi kwa nini serikali iongeze double cost kwa watu, hawakuliona hilo mapema??
 
Unadhani hata angekuwa yeye JPM ndiyo tusingelipa hizo kodi za simu huku ameshauriwa na Waziri wake wa Fedha? Eneo la Mawasiliano hasa Simu ndiyo kwenye hela nyingi sana, Imagine Kwa Mwezi Mmoja fedha zinazopitishwa kwenye M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money n.k zinafika shilingi 12 trilioni.

Mbona ile riba ya 15% ya Loans board iliongezwa naye, hakuna Serikali isiyohitaji kodi kujiendesha
Tusingelipa maana tumemwona wote mzigo mkubwa namna hii kwa wananchi asingekubali
 
Kuhusu Makato ya asilimia 15% hapakuwa na shida kubwa kivile shida ilikuwa kwenye zile asilimia 10 za adhabu ya kuchelewesha na ile ya 6% ya retention.lakini Makato ya kwenye mihamala ni ya kupinga na Kila mtanzania mwenye uelewa mpana
 
Kutoa 100,000 ilikua 3600 sasa hivi 6,100
Kutoa 200,000 ilikua 5300 sasa hivi 8,240
Kutoa 300,000 ilikua 6500 sasa hivi 10,000
Kutoa 400000 ilikua 7000 sasa hivi 11,100
Kutoa 500,000 ilikua 7500 sasa hivi 12,700
Kutoa 600,000 ilikua 8000 sasa hivi 13,900
Kutoa 700,000 ilikua 8000 sasa hivi 15,100
Kutoa 800,000 ilikua 8000 sasa hivi 15,520
Kutoa 900,000 ilikua 8000 sasa hivi 16,900
Kutoa 1,000,000 ilikua 8000 sasa hivi 17,400
Kutoa 3,000,000 ilikua 10000 sasa hivi 20,000

Hiyo list ni ya MAKATO YA ZAMANI NA YA SASA .NA APO NI KUTOA KWA WAKALA.

BADO KUTUMA🤔
Mzee aliyekwambia wanagawana nusu kwa nusu na mitandao nani? hizo tozo za zamani ilikuwa inaenda kwa wakala, mtandao na serikali
 
Kuhusu Makato ya asilimia 15% hapakuwa na shida kubwa kivile shida ilikuwa kwenye zile asilimia 10 za adhabu ya kuchelewesha na ile ya 6% ya retention.lakini Makato ya kwenye mihamala ni ya kupinga na Kila mtanzania mwenye uelewa mpana
Maeneo ambayo Serikali Ina uhakika wa kupata kodi ni Mafuta na Simu. Labda kama utashauri vyanzo vingine mbadala vya kuisaidia Serikali kukusanya kodi.

Kama shilingi 100 ni kubwa bora ipungue hadi 30 lakini isiache kukusanya eneo hilo
 
Serikali inataka ipate na ya kutolea unapowalipa kodi yao🤣🤸‍♂️🐒
 
Tusingelipa maana tumemwona wote mzigo mkubwa namna hii kwa wananchi asingekubali
Asingekubali kwa kuwa tayari alikuwa na uhakika wa kukusanya hela zaidi kupitia DPP kwenye makesi yake ya Uhujumu Uchumi
 
Kwa hiyo Rais akisema mbunge anatii,ndio kazi ya mbunge?
Mama anaonewa tu,
Wabunge 400 hawakuliona kwa kina
Rais nikupitisha sheria kama alivyopitisha sheria ya Kinga
Bunge likikataa kupitisha bajeti ya serikali, RAIS Anayo haki ya kulivunja bunge. Ndio maana watu wanadai katiba mpya ili kuondoa au kupunguza hizi sheria zinazompa mamlaka makubwa Rais. .
 
Nionavya hii kodi sio mbaya sema tatizo wanakata nyingi kana kwamba njaa ya hela walionayo wanataka iishe kwa mwaka mmoja wangeenda taratibu kuliko kukata hela zote hizo, angalia kwenye umeme na maji siku zote huwa tunalipa lkn nani aliwahi kulalamika hivi??? Wapunguze viwango, vimekuwa vikubwa mno, makato mengine wahamishie kwenye chumvi.
 
Unadhani hata angekuwa yeye JPM ndiyo tusingelipa hizo kodi za simu huku ameshauriwa na Waziri wake wa Fedha? Eneo la Mawasiliano hasa Simu ndiyo kwenye hela nyingi sana, Imagine Kwa Mwezi Mmoja fedha zinazopitishwa kwenye M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money n.k zinafika shilingi 12 trilioni.

Mbona ile riba ya 15% ya Loans board iliongezwa naye, hakuna Serikali isiyohitaji kodi kujiendesha
Hata kama inapitia trillion 12 kwenye makampuni ya simu haimpi fulsa Mwigulu kutuibia pesa zetu.
Kazi ya serikali ingekuwa kuboresha huduma za mawasiliano nchi nzima,na kwa tozo za awali serikali ingevuna mara tatu bila kelele kutokea ongezeko la wateja.
Lakini kwa upofu wa waziri huyu asiye na hekima na asiejielewa, anajimaliza kisiasa kwa mihemuko tu ya Zungu, ameamua kuuwa golden goose sijui hayo mayai ya dhahabu atayatoa wapi tena?
Usishangae Mama yetu akakugeuzia kibao atakapositisha tozo mpya,na wewe matarajio ya kuukwa uraisi 2025 yatayeyuka kama siagi.
 
Serikali inatarajia kupata shilingi ngapi kama ongezeko la mapato kwny tozo hizo?

Miamala mingi ya wabongo ni laki moja kushuka chini.

Sasa hizo hela ziende kwny miradi ya maendeleo ili yafaidike makundi yote nchini sio kuongezeana mishahara wachache.
 
Back
Top Bottom