Tumeni hela kwa wakala moja kwa moja ili usipate makato ya kutuma.
Ikiwezekana, kama unayemtumia ana bank account, kwa transaction za kuanzia laki 4 na kuendelea bora umtumie kupitia bank, akitoa kwenye ATM makato hayazidi 2,000.
Kama mbwai na iwe mbwai, tutaacha kutumia simu tuone hizo solidarity zao watazikusanyia wapi.
Matokeo yake,
- makampuni ya simu mapato yatapungua,
- corporate tax zao zitapungua,
- hawa vijana waliojiajiri watapoteza ajira maana watu wakutumia simu kutuma hela watapungua,
Mbaya zaidi, wamepunguza hadi commission walizokuwa wanaoata mawakala kwa about 40%. Vilio vya hawa vijana wanaojiajiri kwenye simu pesa, haitaiacha salama hii serikali. Ogopa sana nchi ambayo unafanya kitu halafu watu wanalalamika kwa machozi.