w0rM
Member
- May 3, 2011
- 99
- 243
Huu ni mfano wa Hospitali inayojengwa huko Tunduma ambapo utashuhudia kuwa kila kitu katika ujenzi huo kinafanywa na Serikali ilihali kuna kampuni nyingi binafsi na zilizoajiri Watanzania wengi zenye uwezo wa kufanya kazi hizo
Ripoti ya takwimu za Tanzania iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mnamo Juni 2019 ilieleza kuwa ajira zinazotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kwa asilimia 42.6 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja
Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Tanzania in Figure 2018”, inaonesha kuwa ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018
Aidha, ripoti hiyo ilieleza kuwa jambo hilo linalotoa changamoto kwa vijana na wadau wa maendeleo kubuni njia mbadala za kuondoa tatizo la ajira nchini
Je, hii ndio njia inayotumiwa na Serikali katika kuongeza ajira katika Sekta Binafsi?
Je, kuna Kampuni ngapi zilizosajiliwa ERB zenye Waajiriwa wengi tu wenye kuweza kufanya hii kazi au Contractors au hata Services Engineers. Kama tunasema mkate wa Taifa ni wetu sote kwanini hatugawani pale inapowezekana?
NBS ambayo ni Serikali imetoa Takwimu yenywe lakini badala ya kusaidia Sekta binafsi ambayo inaajiro watu wengi, Serikali inataka kufanya kila kitu yenyewe. Je, maana yake hii ni nini kama sio kuua Sekta Binafsi na Je, hizi kazi wanazotaka kuzifanywa wenyewe wataweza?