A
Anonymous
Guest
Kwa zaidi ya miaka 7 sasa wafugaji wenye makundi makubwa ya Ng'ombe wa jamii ya wamang'ati na wasukuma wamevamia na kuingiza mifugo holela kwenye vijiji vilivyopo wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Wafugaji hao wamekuwa wakisababisha kuvurugika mfumo wa uzalishaji katika kilimo, kuua na kujeruhi wakulima, kuingiza ng'ombe kwenye mashamba ya wakulima na kulisha na hivyo kusababisha wakulima kuishi kwa hofu na kuwaongezea umaskini.
Pamoja na wakulima kulalamika sana juu ya uvamizi huo lakini hakuna hatua thabiti zinazochukuliwa huku viongozi wa kwenye vijiji ikiwemo askari polisi wakituhumiwa na wakulima kuwa wanashirikiana na wafugaji na kuhujumu operesheni ya kudhibiti ufugaji holela. Wakulima wamekata tamaa na wamekuwa wanyonge kwa sababu kila mwaka juhudi zao za kilimo zinaishia kuwa malisho ya ng'ombe. Wakulima wanaamini kuwa, wafugaji hawadhibitiwi kwa sababu viongozi wa serikali wananufaika na rushwa
Vijiji vinavyoathirika sana ni pamoja na Kiegei, kilimarondo, nakalonji, nahimba, mbondo, chimbendenga, Ngunichile, Lionja, Nditi, namapwia, mtua, nyambi, lipuyu, mbute,,
Serikali ichukue hatua za dhati kuwadhibiti wafugaji hawa wanaosababisha migogoro sugu kwa sababu wakulima wameshakata tamaa na wamekosa imani na namna jambo hili linavyoshughulikiwa, kushindwa kuchukua hatua stahiki inatengeneza bomu la visasi vinavyoweza kuvuruga amani moja kwa moja pale ambapo wakulima wataamua kujihami.