Je serikali imeshindwa kuwafanya wamiliki wa nyumba/majengo ya kupangisha na mafundi ujenzi kukata leseni za biashara ili walipe kodi?

Kwamba somo halijaeleweka au watu mumenuna mnaona nawachomea shughuli zenu?

Nadhani hawajaelewa lugha unayotumia, nini maana ya hili neno "mumenuna", lakini pia wenye nyumba wanalipia kodi ya majengo yao na viwanja.
 
kazi zenyewe za manati,haziko regular,bado mnataka tax..mtakata tax hadi ushuzi
 
Tukilipa nasi tutakupandishia kodi, hela yetu itabaki palepale na chenji kidogo.
 
Mnatoa mawazo mazuri wapi kodi ipatikane ila pia msiwe wakali CAG anapotoa taarifa ya matumizi ya kodi hii mnayohimiza kila kukicha...
 
Tukilipa nasi tutakupandishia kodi, hela yetu itabaki palepale na chenji kidogo.
Kodi nayoisemea mimi ni leseni ya miezi sita sita haiwezi kuwa na implication kubwa kwenye kodi ya pango,cha msingi mapato yapatikane
 
Mnatoa mawazo mazuri wapi kodi ipatikane ila pia msiwe wakali CAG anapotoa taarifa ya matumizi ya kodi hii mnayohimiza kila kukicha...
Lazima tuwe wakali maana ni pesa zetu,tuna changamoto nyingi sana ila serikali imekosa mbinu za kuongeza wigo wa kodi tatizo wamebebana kwenye maamuzi watu wasio na uwezo wa kufikiria nje ya box
 
Ukitaka tuf
kazi zenyewe za manati,haziko regular,bado mnataka tax..mtakata tax hadi ushuzi
Ukitaka tufanye regulation hao wasio na vyeti vya veta watalala njaa ndio maana nikapendekeza wawe na leseni,boda boda wanalipa leseni bima etc kwa pesa gani ya maana wanapata? Kila mtu alipe kodi mkuu kwa kazi anayofanya ili taifa lisonge mbele hasa watu walio kwenye mfumo usio rasmi
 
Nadhani hawajaelewa lugha unayotumia, nini maana ya hili neno "mumenuna", lakini pia wenye nyumba wanalipia kodi ya majengo yao na viwanja.
Hiyo elfu kumi haihusiani na kipato cha nyumba au majengo yao ile ni kodi ya kuendeleza ardhi au kupanga ardhi ya serikali
 
Hoja yako ni nzuri ila umetaka kuiharibu kwa kuiingizia na vitu vingine.

Hii hoja inasimama yenyewe kama yenyewe.

Nakusaidia: Uonezi wa sheria ya kodi kwa mfanya biashara.

Mfanyabiasha popote alipo anamanung'uniko mazito ndani ya nafsi yake juu ya sheria kandamizi ya kodi ya ZUWIO(With holding tax).

Hii kodi ni mzigo aliotwishwa mfanyabiashara ambapo kimsingi ni kodi inayotakiwa kulipwa na mmiliki wa jengo.

Iko ivi kwa wasio wafanya biashara.

Unapoenda TRA kukadiriwa kodi kuna kodi 3 utatakiwa kuzilipa
1.Kodi ya mapato
2.Kodi ya Zuwio
3.Kodi ya stemp

Kwa sasa hoja yetu ipo kodi ya pili japo hata hiyo ya kwanza kuna sintofahamu juu ya ukadiriwaji wake sio sahihi umejikita kuuwa biashara na si kuinyanyua biashara.

Naendele na hoja.

Kodi ya Zuwio huwa ni 10% ya jumla ya pesa uliyomlipa mwenye frem/jengo.

Mfano kama kama unalipa kodi ya frem laki 2 kwa mwezi basi inakuwa
200000*12=2400000/=
Kwahiyo 10% ya hiyo ni 240000( laki 2 na elfu 40).

Hiyo pesa alitakiwa ailipe Mwenye jengo, sasa sheria ilivyo mdhurumu mfanyabiashara inamtaka eti mpangaji ndio aipeleke kisha eti yeye mpangaji atakatana na Mwenye jengo kwenye kodi. Wanadai eti kama Mwenye jengo atakataa kukurejeshea ukawape taarifa.

Jambo hili ni mzigo kwa mfanyabiashara kwani hawezi rudi kwa Mwenye jengo labda kama anataka kutimuliwa kwenye frem.

Hii sheria iwalazimishe TRA wenyewe kwenda kumkata mwenye jengo na mzigo huu wauondoshe kwa mfanyabiashara ni uonevu.

Kwahiyo TRA ikiwapa leseni hawa wenye majengo hasa ya frem za biashara itaweza kuikata moja kwa moja hiyo kodi kwa Mwenye majengo na kuondosha kero kwa wapangaji.


Hiyo kodi ya Zuwio mliyomtwisha mpangaji sio yake. Yake inatakiwa itokane na biashara yake tu.
 
Huku kwenye nyumba za kupanga serikali inapoteza fedha nyingi sana unakuta mwenye nyumba anajipangia kodi tu anavyipenda, ni kweli nyumba ni yake lakini kodi yake pia inakuwa kubwa hailingani na ubora wa nyumba, unampa kodi hakupi cha risiti wala nini, bado dalali naye akupige. Hapobado umeme na maji, kuna nyumba mwenye nyumba anaishi na wapangaji wake anapanga hela ya maji na umeme ya mwezi bila kujali matumizi huu ni wizi wa wazi.

Ikiwezekana kila wizara iangilie namna ya kukusanya kodi kwa kila biashara ambayo ipo chini ya wizara yake bila kuumiza wananchi, mfano hili swala la nyumba wasiachiwe wenye nyumba wenyewe wajipangie bei kwa kuwa ile ni biashara na sio huduma tena hivyo serikali itafute namna ya kuchukua chake kila mwenye nyumba anapochukua kodi. Ikiwezekana malipo yawe yanafanyika ofice ya mtaa au ya kijiji kwa kutumia mashine ya EFD.

Huu mfumo utasaidia wapangaji kulipwa pesa zao kwa wakati sababu itakuwa ni sheria hivyo hakutakuwa na wale wakwepa kodi na wale wapangaji wasumbufu. Pia itasaidia kupunguza usumbufu kwa wapangaji kutoka kwa mwenye nyumba ikiwemo kupandisha kodi kiholela na kijifanya wao ni miungu watu.
 
Umeeleza vizuri mkuu inatakiwa leseni kwa mwenye jengo ndio itaondoa mzigo kwa mpangaji/mfanyabiashara
Sasa je huku kwenye mitaa yetu tunakopanga hilo linafanyika? Jibu ni hapana TRA wanashindwa nini kuwawezesha wenyeviti wa mitaa na watendaji wakusanya pesa ya leseni kwa wenye nyumba za kupangisha maana hao ndio kisheria kabla hujapanga wanatakiwa wajue
Hoja yangu kwa mafundi iko pale pale lazima wawe na leseni ya kazi yao
 
Of course uko sawa yaani mambo yanakwenda holela na serikali inapoteza mapato,sijui wanakigugumizi gani kuwakatisha leseni hawa wakati wanawaumiza wauza mboga mboga kwa vitambulisho mjasiliamali
 
W
Inatakiwa wewe mpangaji,ukate kwenye kodi,ukalipe TRA,kama wewe hulipi,unakosesha mapato,yatakiwa ujitokeze ulipe.
Wewe utanirefund maana ulitakiwa ulipe wewe sasa nakulipia mimi unatakiwa uirudishe,na hapa ndipo hoja ilipo kwa nini sekta hii serikali inapuuza ikadeal na wenye frame ambao wana mkataba kwa nini kusiwe na mikataba rasmi badala ya sasa kila mmiliki wa nyumba ya kupangisha anakuja na masharti yake uchwara,magesti etc wote wana leseni
 
Of course uko sawa yaani mambo yanakwenda holela na serikali inapoteza mapato,sijui wanakigugumizi gani kuwakatisha leseni hawa wakati wanawaumiza wauza mboga mboga kwa vitambulisho mjasiliamali
Hapa kwa kweli inabidi wahusika wafanye utafiti. Sababu hawa wauza mchicha wengi wanatoka nyumba za kupanga hivyo wanabanwa kila sehemu na hawana pakukimbilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…