Habari wakuu!
Kama mada inavyosomeka hapo juu,wamiliki wa nyumba za biashara pamoja na watu walioko kwenye fani mbalimbali za ufundi wakiongozwa na mafundi ujenzi ni makundi yanayopata vipato vya uhakika zaidi ya 170,000 kwa wastani kwa mwezi lakini hawalipi kodi ya mapato
Kwani serikali wanakwama wapi kuwafanya hao watu wakate leseni ya biashara/kazi zao? Kuliko kusumbua wamama na vijana wauza karanga na mbogamboga kwa kukata kitambulisho cha mjasiriamali ilifaa makundi hayo hapo juu yawe na leseni za kazi zao
Viongozi wa mitaa wahakikishe kila nyumba ya kupangisha mmiliki ana leseni na ionekane kwenye mkataba wa wapangaji.Pili kila ujenzi unaofanywa ni lazima fundi awe na leseni ya kazi husika.
Nawasilisha
Hoja yako ni nzuri ila umetaka kuiharibu kwa kuiingizia na vitu vingine.
Hii hoja inasimama yenyewe kama yenyewe.
Nakusaidia: Uonezi wa sheria ya kodi kwa mfanya biashara.
Mfanyabiasha popote alipo anamanung'uniko mazito ndani ya nafsi yake juu ya sheria kandamizi ya kodi ya ZUWIO(With holding tax).
Hii kodi ni mzigo aliotwishwa mfanyabiashara ambapo kimsingi ni kodi inayotakiwa kulipwa na mmiliki wa jengo.
Iko ivi kwa wasio wafanya biashara.
Unapoenda TRA kukadiriwa kodi kuna kodi 3 utatakiwa kuzilipa
1.Kodi ya mapato
2.Kodi ya Zuwio
3.Kodi ya stemp
Kwa sasa hoja yetu ipo kodi ya pili japo hata hiyo ya kwanza kuna sintofahamu juu ya ukadiriwaji wake sio sahihi umejikita kuuwa biashara na si kuinyanyua biashara.
Naendele na hoja.
Kodi ya Zuwio huwa ni 10% ya jumla ya pesa uliyomlipa mwenye frem/jengo.
Mfano kama kama unalipa kodi ya frem laki 2 kwa mwezi basi inakuwa
200000*12=2400000/=
Kwahiyo 10% ya hiyo ni 240000( laki 2 na elfu 40).
Hiyo pesa alitakiwa ailipe Mwenye jengo, sasa sheria ilivyo mdhurumu mfanyabiashara inamtaka eti mpangaji ndio aipeleke kisha eti yeye mpangaji atakatana na Mwenye jengo kwenye kodi. Wanadai eti kama Mwenye jengo atakataa kukurejeshea ukawape taarifa.
Jambo hili ni mzigo kwa mfanyabiashara kwani hawezi rudi kwa Mwenye jengo labda kama anataka kutimuliwa kwenye frem.
Hii sheria iwalazimishe TRA wenyewe kwenda kumkata mwenye jengo na mzigo huu wauondoshe kwa mfanyabiashara ni uonevu.
Kwahiyo TRA ikiwapa leseni hawa wenye majengo hasa ya frem za biashara itaweza kuikata moja kwa moja hiyo kodi kwa Mwenye majengo na kuondosha kero kwa wapangaji.
Hiyo kodi ya Zuwio mliyomtwisha mpangaji sio yake. Yake inatakiwa itokane na biashara yake tu.