Je serikali imeshindwa kuwafanya wamiliki wa nyumba/majengo ya kupangisha na mafundi ujenzi kukata leseni za biashara ili walipe kodi?

Je serikali imeshindwa kuwafanya wamiliki wa nyumba/majengo ya kupangisha na mafundi ujenzi kukata leseni za biashara ili walipe kodi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Habari wakuu!
Kama mada inavyosomeka hapo juu,wamiliki wa nyumba za biashara pamoja na watu walioko kwenye fani mbalimbali za ufundi wakiongozwa na mafundi ujenzi ni makundi yanayopata vipato vya uhakika zaidi ya 170,000 kwa wastani kwa mwezi lakini hawalipi kodi ya mapato
Kwani serikali wanakwama wapi kuwafanya hao watu wakate leseni ya biashara/kazi zao? Kuliko kusumbua wamama na vijana wauza karanga na mbogamboga kwa kukata kitambulisho cha mjasiriamali ilifaa makundi hayo hapo juu yawe na leseni za kazi zao
Viongozi wa mitaa wahakikishe kila nyumba ya kupangisha mmiliki ana leseni na ionekane kwenye mkataba wa wapangaji.Pili kila ujenzi unaofanywa ni lazima fundi awe na leseni ya kazi husika.
Nawasilisha
 
Kwamba somo halijaeleweka au watu mumenuna mnaona nawachomea shughuli zenu?
 
Mapato na Matumizi
Unapokusanya fedha ya wamachinga kama kodi maana yake uwasaidie kuboresha miundo mbinu ya biashara zao au fedha itumike katika sera ya ukuzaji wa mitaji kwa wamachinga/wauzaji bidhaa wadogo.
Ukikusanya fedha za wenye nyumba maana yake barabara za mtaa ziwe bora,uwaboreshee huduma ya maji safi na taka,kila siku takataka zikusanywe, uwape ushauri wa kuboresha huduma ya upangishaji,uwape ushauri juu ya majanga ya moto..
Kwa mafundi nao wana changamoto zao za kuwasaidia..
Kukusanya bila kulenga msaada wa moja kwa moja katika eneo husika huonekana kama unyonyaji haijalishi ni kwa mujibu wa sheria au la ila kabla ya kuunda sheria umezingatia ustawi wa jamii..
 
Mapato na Matumizi
Unapokusanya fedha ya wamachinga kama kodi maana take uwasaidie kuboresha miundo mbinu ya biashara zao au fedha itumike katika sera ya ukuzaji wa mitaji kwa wamachinga/wauzaji bidhaa wadogo.
Ujikusanya fedha za wenye nyumba maana yake..barbara za mtaa ziwe bora,uwaboreshee huduma ya maji safi na taka,uwape ushauri wa kuboresha huduma ya upangishaji,uwape ushauri juu ya majanga ya moto..
Kwa mafundi nao wana changamoto zao za kuwasaidia..
Kukusanya bila kulenga msaada wa moja kwa moja katika eneo husika huonekana kama unyonyaji haijalishi ni kwa mujibu wa sheria au la ila kabla ya kuunda sheria umezingatia ustawi wa jamii..
Ndo hivyo mkuu maana ukimobilize pesa za kutosha kutoka makundi hayo si ndio masuala ya miundombinu yataboreshwa
 
Ndo hivyo mkuu maana ukimobilize pesa za kutosha kutoka makundi hayo si ndio masuala ya miundombinu yataboreshwa
Kukusanya sio shida, changamoto huja kwamba fedha iliyokusanywa imefanya kazi gani?
Unakuta fedha imekusanywa kwa lengo fulani ila inachepushwa kwenda kwingine ambako hakujulikani mambo ambayo yanampa tabu CAG wakati wa ukaguzi.
 
Habari wakuu!
Kama mada inavyosomeka hapo juu,wamiliki wa nyumba za biashara pamoja na watu walioko kwenye fani mbalimbali za ufundi wakiongozwa na mafundi ujenzi ni makundi yanayopata vipato vya uhakika zaidi ya 170,000 kwa wastani kwa mwezi lakini hawalipi kodi ya mapato
Kwani serikali wanakwama wapi kuwafanya hao watu wakate leseni ya biashara/kazi zao? Kuliko kusumbua wamama na vijana wauza karanga na mbogamboga kwa kukata kitambulisho cha mjasiriamali ilifaa makundi hayo hapo juu yawe na leseni za kazi zao
Viongozi wa mitaa wahakikishe kila nyumba ya kupangisha mmiliki ana leseni na ionekane kwenye mkataba wa wapangaji.Pili kila ujenzi unaofanywa ni lazima fundi awe na leseni ya kazi husika.
Nawasilisha
Hujui 10% inayokatwa na TRA kutoka kwenye kodi ya nyumba ?
 
Kukusanya sio shida, changamoto huja kwamba fedha iliyokusanywa imefanya kazi gani?
Unakuta fedha imekusanywa kwa lengo fulani ila inachepushwa kwenda kwingine ambako hakujulikani mambo ambayo yanampa tabu CAG wakati wa ukaguzi.
Sawa hilo ni la udhibiti tuu lakini zikusanywe kwanza,nchi hii ina pesa nyingi sana kwenye informal sector,watu wa serikali za mitaa hii ndio fursa kwao kupata mapato
 
Kwanza lazima iandaliwe 'database' kubwa sana ya kila sekta kabla ya kukusanya la sivyo ubadhirifu utaendelea..
Sijawahi kuona dokumenti yoyote ya idadi ya makisio ya mafundi wasio na vyeti (waashi,mekaniki nk),wenyenyumba na watu wasio na ajira.Kwa wasio na ajira nakumbuka kuna ile kasumba mtu hana kazi alafu wanamjazia kwamba ni mkulima wakati hana ata shamba ni mtumwa wa vibarua visivyompeleka popote kiuchumi "he/she is a beggar"
Kuna haja ya watu wa NIDA na mamlaka nyingine juu kuimarisha mikakati ya utambuzi.
 
Unawajua wapiga kura?,kuwa makini sana na kauli zako
 
Pia kuhusu nyumba za kupanga kuna changamoto kubwa sana ili itoke leseni lazima tuzingatie ubora wa nyumba na kuweka madaraja ili kuweka viwango vya utozaji.
Mfano nyumba daraja 1,2,3,4,5
 
Pia kuhusu nyumba za kupanga kuna changamoto kubwa sana ili itoke leseni lazima tuzingatie ubora wa nyumba na kuweka madaraja ili kuweka viwango vya utozaji.
Mfano nyumba daraja 1,2,3,4,5
Sawa zipangwe tuu sasa TRA kila mwaka pombe na sigara tuu wakati kuna kodi nyingi kwenye mfumo usio rasmi?
Orodha ya Ally Hapi imetoa mwanga watu wafikirie
 
Huu mpango unafaa kuanza 2030 kwa wenye nyumba,pia serikali iingilie kati kuwawekea viwango vya ubora. Bodi ya ukaguzi wa nyumba za kupanga iundwe kila wilaya itakayokuwa chini ya NHC maana nyumba nyingine hazina hadhi ya kuishi binadamu kama kweli tunataka na sisi tuhesabike katika uchumi wa daraja la pili.
 
Back
Top Bottom