Je, Serikali "imevilazimisha" vyombo vya habari viripoti habari nzuri pekee za watawala wa CCM?

Bwana Mayala tangu wakati ule Magufuli alipokupiga na kitu kizito haujawahi kurudi kwenye mstari.
Fani ya uandishi wa habari ni kama wanajeshi wa mstari wa mbele vitani, mkipigwa ambush, ni wajibu wako kutumia kitu kinachoitwa self initiative to survive kwa kupambana kwa akili yako yote, a loner battle ama ushinde na ukiona dalili za kushindwa una retreat na ikitokea umebananishwa you surrender. Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
Tulikuwa tuko vitani Elections 2015 - Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ?
Baada ya kugundua Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

The most important thing is survival, I'm a survivor.
P
 
Naomba utofautishe uhuru wa kuikosoa serikali na uhuru wa kutokana serikali na viongozi wake. Kama ni ukosoaji with facts, if bado tunaongoza sana kuisaidia serikali kwa ukosoaji na nyuzi hazifutwi!. Ila kuna wenzetu humu ambao sio wazima, badala ya kuikosoa serikali wao ni kutokana na kuwatukana viongozi, if modes ni wazima wako macho na halali.
P
Kama viongozi wanajitajirisha kwa pesa ya umma tukiwaita kwa majina na kuwaita wezini kosa?. Mfano Ben saanane alikuwa na facts juu ufisadi wa Phd ya Magufuli kilichompata wewe ni shahidi
 
Paskali umeongea sana kwa uchungu na ukweli yaani jf tukikulinganisha wa Pskali jembe Ulaya wakati ule. Kuna wakati nasoma mchango wa Paskali nisema haya hayjatoka moyoni mwake siyo huyu tunayemfahamu
 
Hiyo mbinu wanayotumia eti to survive ndiyo itakayowaua. Fikiria kipofu anatembea barabarani na hataki kuambiwa palipo na shimo. What will happen?
Njia Bora ni kukubali kuambiwa ulipokosea na kujirekebisha
 
Tanzania Kuna media capture na mbaya zaidi tasnia ya habari kuna viwavijeshi wasio jitambua badala ya kuandika habari na kufanya investigative Journalism wako bize na habari za udaku (Yellow News)

"Waandishi wa habari Tanzania ina bidi wajifanyie uyakinifu thabiti katika kazi zao"
Wengi wa waandishi wa habari, wanaandika habari za kujipendekeza, wakitegemea kuwa mwisho wa siku, dhali litawaangukia na wapate uteuzi, kama waandishi wenzao, akina Godwin Gondww na Fatuma Nyangasa, ambao Sasa hivi ni waheshimiwa ma-DC😃
 
Kwa nchi yoyote yenye utawala Bora, inavitumia vyombo vya habari kama mhimili wao wa 4, usio rasmi, baada ya mihimili rasmi ya Serikali, Mahakama na Bunge, katika kuendesha nchi.

Huwa wanavitumia vyombo vya habari kama "watchdogs" vyao Kwa kuwa huwa wanakosoa, Ili serikali Ione mapungufu yake Ili ijirekebishe, katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Hali ni tofauti Sana hapa nchini kwetu, Kwa kuwa mihimili yote 3, yaani Serikali, Mahakama na Bunge, yote ni kama "imemezwa" na Mhimili wa Serikali, ambao ndiyo unaoelekea kuwa "umejichimbia" zaidi chini, hivyo kufanya mihimili mingine ya Bunge na Mahakama kutoweza kufurukuta!

Hata hivyo pamoja na mihimili hiyo 2 "kumezwa" na Mhimili mmoja, ambao ni Serikali, Bado hufanya Mhimili mwingine, usio rasmi, wa vyombo vya habari, kufanya kazi yake ya kukosoa Kwa weledi mkubwa, hivyo kuufanya Mhimili wa Serikali, kufanya kazi yake ikijirekebisha pale ilipokosolewa.

Hapa nchini kwetu, Mhimili wa Serikali, unachukua nafasi ya u-mungu-mtu, ambao hautaki kabisa kukosolewa na hivyo kufanya utawala Bora, kuwa kama hadithi tuuu ya alifu lela ulela!

Serikali inaweza kusema inatoa uhuru Kwa vyombo vya habari, pamoja na vile vya binafsi, kuwa huru, lakini "indirectly" uhuru huo wanauminya!

Kwa kuwa vyombo vya habari, hususani magazeti, hujiendesha Kwa kutumia matangazo ya biashara, na Serikali ikiwa ndiyo mtoaji mkubwa wa matangazo hayo, huweza "kuvipendelea" vyombo vya habari vinavyosifu sifu utawala huu wa CCM, Kwa kutumia lugha yao kuwa "Rais Samia anaupiga mwingi"na hivyo kutotoa matangazo hayo Kwa vyombo vya habari, ambavyo vinatekeleza wajibu wao kikamilifu wa kukosoa na hivyo kuvinyima matangazo hayo na hivyo kuvifanya vyombo hivyo vya habari binafsi, kutoweza ku-survive katika soko hilo.

Kwa Serikali kujifanya Iko 100 percent perfect, ndiko kunakoifanya ifanye figisu figisu hizo za kuvinyima fursa hiyo ya matangazo vyombo hivyo vya habari ambavyo viko "serious"

Hivi katika nchi kama yetu, ambayo imeweka mfumo wa kumfanya Rais wetu, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chake, kuwa kama mungu- mtu, ambaye ni binadamu, kutotoa nafasi ya kukosolewa, kunadhoofisha Sana mfumo wa utawala Bora.

Kwani vitabu vyote vya dini vinaamini kuwa ni Mungu pekee, ambaye yuko [emoji817] percent perfect, ambaye hapaswi kukosolewa.

Lakini sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na hivyo kutufanya kutumia njia ya kukosolewa kama njia ya kujirekebisha na hivyo kurudi kwenye msitari.

Ukiviacha vyombo vya habari vya mtandaoni kama Jamii forum, ambavyo uhuru wao wa kukosoa uko juu, vyombo vingine vya habari, kama vile magazeti, Televisheni na Radio, uhuru wao wa kutoa habari unathibitiwa na Serikali na upo chini Sana hapa nchini kwetu.

Dawa pekee na ya kudumu ni kupata Katiba mpya, ambayo itaweka mifumo imara ya kiuongozi wa nchi
..
IMG-20220607-WA0000.jpg
 
Hela za kuhonga si zipo
 
Tanzania Kuna media capture na mbaya zaidi tasnia ya habari kuna viwavijeshi wasio jitambua badala ya kuandika habari na kufanya investigative Journalism wako bize na habari za udaku (Yellow News)

"Waandishi wa habari Tanzania ina bidi wajifanyie uyakinifu thabiti katika kazi zao"
In Tanzania the elites have captured the media
 
Ndiyo tatizo kubwa nchini kwetu, badala ya waandishi kufuata "ethics" za kazi yao, wao wakati wote wanawaza uteuzi wa Rais!

Kama ambavyo wenzao Godwin Gondwe na Fatuma Nyangasa, walivyoukwaa u-DC😄

Dawa ya kuzima vurugu zote hizi ni kupata Katiba mpya, ambayo itampunguzia madaraka makubwa ya ki-mungu-mtu, aliyonayo Rais wetu
 
In Tanzania the elites have captured the media
Hivi inakuwaje katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 60, tuwaachie kikundi kidogo Cha watu kituamulie maisha yetu wote kibabe?😎

Ni LAZIMA kama nchi, tuwe na Katiba mpya, ambayo itaweka mifumo imara ya kiuongozi
 
Tatizo ni akili ndogo za wananchi kuto iwajibisha serikali na bunge.
 
Wataiwajibishaje Serikali, wakati wenye jukumu hilo kikatiba, ambao ni Bunge letu, Kila siku wanasifu na kuabudu, Kwa kusema Mama anaupiga mwingi, wakijipendekeza Kwa Rais?

Dawa ya kudumu ni kuandaa Katiba mpya, itakayomuondolea hayo mamlaka makubwa mno, mithili ya ki-mungu-mtu, aliyo nayo Rais wetu na kuleta mifumo imara ya kitaasisi
 
Hivi inakuwaje katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 60, tuwaachie kikundi kidogo Cha watu kituamulie maisha yetu wote kibabe?😎

Ni LAZIMA kama nchi, tuwe na Katiba mpya, ambayo itaweka mifumo imara ya kiuongozi
Kwangu Mimi katiba mpya siyo suluhisho la matatizo ya Tanzania...hata tukiwa na katiba mpya ukiwa na uongozi usio na maono tutabaki kuwa maskini....tatizo la Tanzania ni leadership...tunahitaji uongozi went maono na went elements za uzalendo...
Wewe fikiria uongozi unaruhusu kununua magari ya anasa kwa viongozi huku wananchi wakikosa huduma za msingi Kama maji....gari moja la DED lenye thamani ya sh. Milioni 400 linaweza kuzaa visima vingaoi vya maji vyenye thamani ya sh. Milioni 5 Kila kimoja?!....mbunge Ana maslahi makubwa kupindukia...ndiyo maana wasomi, wafanyabiashara na waandishi wa habari wanakimbilia kwenye siasa/uteuzi kwenye maslahi..
Hatuwezi kamwe kuendelea kama tutaendelea kuamini kuwa mikopo ya IFM na World Bank ndiyo suluhisho la matatizo yetu...
 
Back
Top Bottom