Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Nimezungumza na watu mbalimbali waliowahi kushikwa na polisi kwa makosa mbalimbali karibu wote wanasema walitoka polisi baada ya kutoa fedha.
Wengine waliachiwa kabla ya kufikishwa kituoni baada ya kutoa pesa.
Wengine waliachiwa baada ya kutoa pesa ambayo polisi waliziita pesa ya kumdhamini mtuhumiwa huku kesi ikipelekwa mahakamani.
Polisi wa barabarani almaarufu trafiki wamejiwekea kiasi rasmi. Ilikuwa kila daladala wakilipiga mkono lazima idondoke sh.200, baada ya mafuta kupanda serikali ilitangaza bei mpya za nauli nao trafiki wakaongeza 50% ikawa sh. 3000.
Wanaichukua bila kificho, gari ikisimama konda ndiye hushuka na kumpa 3000 trafiki safari inaendelea.
Je, serikali hii tukufu imewapa polisi ruksa ya kula rushwa?
Ni tatizo la miaka mingi.