Je, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Samia au Majaliwa?

Je, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Samia au Majaliwa?

Magufuli ameshalala kaburini kwa mwaka mmoja na miezi tisa sasa, jaribuni kuamka akilini ili mjue kwamba hatarudi tena na hawezi kuwa ndio kipimo cha ufanisi wa serikali.
Kwahiyo kama Magufuli amekufa ndo na utendaji kazi nao umekufa? Kwamba watumishi wa umma wanaruhusiwa kuiba watakavyo kisa aliekuwa ana deal nao ameshakufa?

Akili za wapi hizi?
 
Ishu vipi wakuu,
Kama swali linavyouliza hapo juu, narudia tena kuuliza.
Je serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na kuendeshwa na raisi Samia au waziri mkuu Majaliwa?
Nauliza hivi kwa sababu kuna madudu mengi yanayofanywa na viongozi wa serikali ambao wengine ni wateule wa raisi, lakini cha kushangaza mpambanaji wa madudu hayo ni mmoja tu Majaliwa peke yake, huku mwenye dhamana na jukumu kuu la kuchukua hatua mh raisi Samia na makamu wake dr Mpango wakiwa busy kupambana na wanaopinga mikopo badala ya ku deal na wabadhilifu wa mali zao.

Raisi Samia na makamu wake wamekuwa wakikutana na madudu mbali mbali katika ziara zao lakini hakuna hata siku moja ambayo waliwahi kuchukua hatua ya papo hapo dhidi ya wafanya madudu hao. Je wanakuaga wanawaogopa au kuwaonea aibu wafanya madudu hao?

Juzi kati makamu wa raisi ambae ni mtu wa pili kwa nguvu ya madaraka baada ya ile ya kwanza inayoshikiliwa na raisi alikabidhiwa majina ya familia 12 zinazoitafuna nchi ili achukue hatua. Lakini cha kushangaza makamu huyo hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kuwahadaa watu kwamba anakwenda kulifanyia kazi swala lile bila kusema itamchukua muda gani kumaliza kulifanyia kazi swala hilo na kuwachukulia hatua wahusika.

Mbona Majaliwa huwa haombi muda wa kulifanyia kazi swala la namna hiyo na badala yake huchukua hatua ya papo hapo?

Je kama wote watatu wangekuwa wanachukua hatua hizi za Majaliwa unafikiri ujinga huu wa kupiga hela ungeendelea?

Inaongozwa na Rais samia
 
We Malaya wa kisiasa in nyerere voice.
We Nashambwa wilenga. [emoji24][emoji24]
 
Hii Nchi ya Kijinga sana..

Sijui Ma DC, na Ma RC wanafanya kazi.

Tatizo kubwa ni Mnyororo wa Rushwa, unakuta kuanzia RC mpaka DED na kamati za Usalama , ni Wala Rushwa tupuuu na wamejitengenezea kachain ka kula Rushwa.

Sasa hamna wa kukemea

Ndo maana unaona Leo hiii Waziri Mkuu, Kipenzi Cha Watanzania, Majaaliwa Kassim, anahangaika kama mtoto !!
Kumbe Majaliwa ni kipenzi cha watanzania !
 
Kipenzi chako,sio cha watanzania.
Hii Nchi ya Kijinga sana..

Sijui Ma DC, na Ma RC wanafanya kazi.

Tatizo kubwa ni Mnyororo wa Rushwa, unakuta kuanzia RC mpaka DED na kamati za Usalama , ni Wala Rushwa tupuuu na wamejitengenezea kachain ka kula Rushwa.

Sasa hamna wa kukemea

Ndo maana unaona Leo hiii Waziri Mkuu, Kipenzi Cha Watanzania, Majaaliwa Kassim, anahangaika kama mtoto !!
 
Hakuna kundi linalokosa watu wema na wabaya. Hata majambazi wanapokwenda kuiba lazima kati yao wakakuwepo wanaotamani kuiba na kuuwa na wengine wanaotamani kuiba tu bila kuuwa. Kwahiyo katika hili sikubaliani na wewe.

Waziri mkuu anaonekana kabisa yuko tofauti na hao niliowataja hapo juu.
Hujajibu hoja yangu. Je angekua yeye Philip ndy Kassim angewadaka wale 12? Toka tumeanza kusikia ufisadi sirikalini ni lini Viongozi wanene wa serikali wakawajibika mahakamani? Msifanye kufikiri kuwa watu bado ni mafala.
 
Kwahiyo kama Magufuli amekufa ndo na utendaji kazi nao umekufa? Kwamba watumishi wa umma wanaruhusiwa kuiba watakavyo kisa aliekuwa ana deal nao ameshakufa?

Akili za wapi hizi?
Aliyekwambia hawa wa sasa wanaiba kwa sababu JPM amekufa ni nani?. Akili za kitoto ni tatizo lako mkuu.

Kila rais anakuja na mtazamo wa kwake binafsi wa ufanyaji kazi. Miradi yote aliyoacha JPM inamalizwa mmoja baada ya mwingine. Wafanyabiashara wanafanya kwa amani kabisa na ulipaji kodi ni wa kiwango kile kile nchi nzima.

JPM ameshaondoka na aliyepo anafanya kazi namna anavyoona inafaa kwa taifa na wadau muhimu wa uendeshaji wa uchumi wana amani na uongozi huu.

Nyinyi wafuasi wa JPM mnaodhani kuwa alikuwa ndio kipimo cha ufanisi, mnaendelea kuzeeka na majonzi ya mioyoni na hakuna wa kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom