Je, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Samia au Majaliwa?

Magufuli ameshalala kaburini kwa mwaka mmoja na miezi tisa sasa, jaribuni kuamka akilini ili mjue kwamba hatarudi tena na hawezi kuwa ndio kipimo cha ufanisi wa serikali.
Kwahiyo kama Magufuli amekufa ndo na utendaji kazi nao umekufa? Kwamba watumishi wa umma wanaruhusiwa kuiba watakavyo kisa aliekuwa ana deal nao ameshakufa?

Akili za wapi hizi?
 

Inaongozwa na Rais samia
 
We Malaya wa kisiasa in nyerere voice.
We Nashambwa wilenga. [emoji24][emoji24]
 
Kumbe Majaliwa ni kipenzi cha watanzania !
 
Kipenzi chako,sio cha watanzania.
 
Hujajibu hoja yangu. Je angekua yeye Philip ndy Kassim angewadaka wale 12? Toka tumeanza kusikia ufisadi sirikalini ni lini Viongozi wanene wa serikali wakawajibika mahakamani? Msifanye kufikiri kuwa watu bado ni mafala.
 
Kwahiyo kama Magufuli amekufa ndo na utendaji kazi nao umekufa? Kwamba watumishi wa umma wanaruhusiwa kuiba watakavyo kisa aliekuwa ana deal nao ameshakufa?

Akili za wapi hizi?
Aliyekwambia hawa wa sasa wanaiba kwa sababu JPM amekufa ni nani?. Akili za kitoto ni tatizo lako mkuu.

Kila rais anakuja na mtazamo wa kwake binafsi wa ufanyaji kazi. Miradi yote aliyoacha JPM inamalizwa mmoja baada ya mwingine. Wafanyabiashara wanafanya kwa amani kabisa na ulipaji kodi ni wa kiwango kile kile nchi nzima.

JPM ameshaondoka na aliyepo anafanya kazi namna anavyoona inafaa kwa taifa na wadau muhimu wa uendeshaji wa uchumi wana amani na uongozi huu.

Nyinyi wafuasi wa JPM mnaodhani kuwa alikuwa ndio kipimo cha ufanisi, mnaendelea kuzeeka na majonzi ya mioyoni na hakuna wa kuwasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…