"Je, Serikali ya Nigeria Inapaswa Kujadiliana na Watekaji Ili Kuokoa Mateka?"

"Je, Serikali ya Nigeria Inapaswa Kujadiliana na Watekaji Ili Kuokoa Mateka?"

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Takriban watu 20 wameuawa baada ya magenge yenye silaha kuvamia vijiji vya Jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria, kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP.

Mwakilishi wa Wilaya ya Sauna katika eneo la Talata Mafara, Nasiru Lauwali, alisema washambuliaji walivamia vijiji hivyo kati ya saa 9:00 na saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki (14:00–15:00 GMT), wakiwashambulia wananchi waliokutana nao.

Soma zaidi:Jeshi la Nigeria limefanikiwa kumuua Kamanda wa Boko Harqm, Abu Khalid

Lauwali alisema idadi kubwa ya watu wenye silaha walivamia jamii hizo na kulenga kuwaua wakazi bila kuchagua, hali iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 20 huku kukiwa na hofu ya idadi hiyo kuongezeka kadri juhudi za uokoaji zinavyoendelea.
Screenshot_20260723-104747.png


Mashambulizi hayo yanajiri wakati Nigeria ikiendelea kukabiliwa na ongezeko la matukio ya utekaji nyara kwa ajili ya kudai fidia. Makundi yenye silaha yamekuwa yakiwateka raia na kuwashikilia hadi pale fedha za ukombozi zinapolipwa.

Usiku wa Jumanne, watu watatu wanaoshukiwa kuwa majambazi waliuawa na vikosi vya usalama katika Jimbo la Kwara. Kwa mujibu wa gazeti la The Punch, vikosi hivyo vilifanikiwa pia kumuokoa mfanyabiashara aliyetekwa nyara, Tuhkur Sanni.

Mamlaka nchini Nigeria zinaendelea kupambana na makundi ya wahalifu huku hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya kutokana na uasi wa kundi la Boko Haram katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi.

Kwa mujibu wa taasisi ya SBM Intelligence, mwaka 2024 watekaji nyara nchini Nigeria walikusanya zaidi ya dola za Marekani milioni 1.6 kupitia malipo ya fidia kutoka kwa serikali na raia waliotekwa.

Mapema mwezi huu, wanafunzi na walimu kadhaa waliotekwa nyara katika Jimbo la Oyo waliokolewa na vikosi vya usalama baada ya kukaa matekani kwa siku 56. Operesheni hiyo ilipelekea watu wanane wanaoshukiwa kuhusika na utekaji huo kukamatwa, huku wengine wakiuawa wakati wa makabiliano.

==================
At least 20 people have been killed in northwest Nigeria after armed gang members attacked villages in Zamfara State, according to the AFP news agency.

“Today, between 3pm [14:00 GMT] and 4pm [15:00 GMT], a large number of bandits have invaded our communities, targeting all the people they meet,” Nasiru Lauwali, the representative of the Sauna district in the local government zone of Talata Mafara, told AFP on Wednesday.

he attacks come amid increasing violence in northwest and central Nigeria, where armed gangs or bandits have raided villages in recent weeks. They are accused of stealing livestock and kidnapping residents for ransom.

Late on Tuesday, at least three suspected bandits were killed by security forces in the country’s Kwara State, according to Nigeria’s The Punch news website. The news service said that security forces managed to rescue a businessman, Tuhkur Sanni.

Kidnappings have become common in Nigeria, as armed groups seek large ransoms from the government and citizens.

The situation has been worsened by a security crisis, partly fuelled by the Boko Haram rebellion in the country’s northeast. In 2024, attackers earned more than $1.6m in ransom payments, according to SBM Intelligence.

Dozens of students and teachers were Defence Minister Christopher Musa said the suspects planned to use the hostages as leverage to pressure the government to release some of their commanders from prison.56 days after they were kidnapped from three schools in the southwestern state of Oyo.

Eight of the suspected kidnappers were arrested and an unspecified number were killed, according to a statement issued by President Bola Tinubu.

Defence Minister Christopher Musa said the suspects planned to use the hostages as leverage to pressure the government to release some of their commanders from prison.

Source: Al-Jazeera
 
Nini kimeikumba Nigeria mpaka kugeuka failed state.

Mbona serikali za kiraia zimeonyesha udhaifu mkubwa sana kuongoza nchi na kukabiliana na ukosefu wa Usalama?.... T14 Armata
 
Dini ya kiislam inapaswa itizame upya mafundisho yake katika madrasa kwani ni kichocheo kikubwa cha kusababisha ugaidi kwenye nchi za kiislamu au maeneo yenye idadi kubwa ya jamii ya kiislam.

Haiwezekani maeneo yenye idadi kubwa ya jamii ya kiislam ndio yagubikwe na vitendo vya kigaidi.
 
Dini ya kiislam inapaswa itizame upya mafundisho yake katika madrasa kwani ni kichocheo kikubwa cha kusababisha ugaidi kwenye nchi za kiislamu au maeneo yenye idadi kubwa ya jamii ya kiislam.

Haiwezekani maeneo yenye idadi kubwa ya jamii ya kiislam ndio yagubikwe na vitendo vya kigaidi.
Nadhani tatizo sio Dini ila itikadi za Kisiasa zilizovalishwa koti la Dini.

Nchi kama Malaysia na nchi za Ghuba kuna waislamu wengi ila hamna vurugu kama za huko Nigeria.
 
Back
Top Bottom