Ahlan wa sahlan
Naiomba serikali ifunge hizi ofisi uchwara zilizopo hapa maeneo ya shekilango na Urafiki. Mabasi ya mikoani yamekuwa hayaendi tena kupaki stendi ya Magufuli pale Mbezi badala yake yamekuwa yakijazana maeneo ya Shekilango na Urafiki nyakati za Alfajiri na Mchana. Najiuliza ile stendi ya mabilioni pale Mbezi imejengwa kwa ajili ya kina nani?
Wahusika mpo na mnalifumbia mamcho jambo hili.Stendi imekuwa ikikosa mapato ya getini kwa abiria wanaoingia ndani ya stendi kutokana na watu sasa kumiminika kwenda maeneo ya Urafiki na Shekilango.
Wito wangu kwa serikali ni kuhakikisha mnazifunga mara moja ofisi hizi uchwara za haya mabasi hapa Shekilango na urafiki kwani hawa jamaa wameshageuza eneo hili kuwa Binafsi naishukuru serikali kwa kurusu kuwe na stand ndogo kama mabasi yanavyotoa huduma kutokea sehemu mbalimbali urafiki shekilango mbagala chanika kigamboni nk uku ni kukua kwa huduma na ni kuondoa usumbufu kwa wananchi pata picha nakaa mkuranga nasafiri na watoto nikifika mbagala napata huduma ya usafiri kwa uhakika kuliko niende mbezi kwanza mbali pili ni changamoto kwa iyo wewe kama mwananchi wa kawaida upaswi kulalamika hata kidogo kwa sababu huduma ya usafiri imekuwa ila kama unamaslahi binafsi na stand ya magufuli tafuta plan B siyo unataka kurudisha ugumu wa uduma ya usafiri bila sababu