Je, Shekilango na Urafiki ndio Stendi mpya za Mabasi yaendayo mikoani?

Ukweli ni kuwa mtoa mada hajui alisemalo.
Basi zote lazima ziingie stendi ya Magufuli. Haijalishi imetoka Shekilango, kariakoo au magomeni.

Mapato ya serikali yapo pale pale.
Hivi lengo la kusema mabasi yaende pale stendi ya Magufuli ni ili tu yakalipe ushuru? Mfano kama bus halina abiria yoyote anaepanda/shuka magufuli terminal, kwanini liende? Ushuru si wanaweza wakalipa hata kwa mpesa au wakaamua kulipia mabasi yao yote kwa mwezi shida iko wapi?
 
Haya gari linapaki Mbagala.

Abiria wengine wanakaaa Mbagala au Magomeni na maeneo ya Karibu.

Kwahiyo inatakiwa Bus litoke Mbagala likiwa TUPU mpaka Magufuli stand.

Na abiria apande daladala mpaka Magufuli stand kwenda kulipandq Hilo Bus.

Hii ni akili au mtindio wa ubongo????

Na Jioni ukifika Dar, Bus linatakiwa likushushe magufuli stand wakati unaenda Riverside na huko huko ndiko Bus linakoenda kulala??

Siyo???
 
Muwe mnasoma hoja vizuri, jamaa hazungumziii kukata tiketi, hoja ya msingi hapa na baadhi ya mabasi kutopitia kabisa Mbezi Bus Terminal, zinapandisha abiria hapo Urafiki na kupita juu kwa juu.
Habar za ticket nimequote jamaa aliyezungumza kuhusu ticket, ungeelewa kwanza yaye alisemaje ndo ukaniambia hivyo

Acheni papara nyie kujifanya kujua, hata hivyo suala la tiketi na usafiri ni nje ya mada?
 
Muwe mnasoma hoja vizuri, jamaa hazungumziii kukata tiketi, hoja ya msingi hapa na baadhi ya mabasi kutopitia kabisa Mbezi Bus Terminal, zinapandisha abiria hapo Urafiki na kupita juu kwa juu.
Yataje hayo mabasi
 
Shekilango International Airport
 
 
LATRA wamezidiwa nguvu na matajiri wa mabasi.

Kiongozi wa mbio za mwenge 2024 alitoa maagizo kuwa Mabasi yote yapakie Magufuli terminal lakini maagizo yamepuuzwa.
 
Sioni shida wao kupakia huko Shekilango Kisha waje Magufuli.Binafsi sipendi nikitaka kwenda Moshi au Arusha mabasi mazuri mengi hayaji kabisa Magufuli yanaondokea hukohuko Shekilango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…