Bado upo pale pale tu: Science vs Maagizo!
Kama nilivyosema, mafundisho yanasema “Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi na kama hamjauona, kamilisheni siku 30"!
Mafundisho hayajataja mambo ya Saudi Arabia, Mecca, Madinna wala suala la "masaa" kuwa sawa! Kwani Mtume hakufahamu role ya Saudi Arabia kwenye masuala ya imani?
Na hata wanaotumia mwandamo wa Saudi Arabia, sijawahi kusikia wakitoa argument ya kufanana masaa! Watu watafuata ama mwandamo wa Saudi Arabia au mwandamo wa maeneo yao/na majirani!
Halafu soma hii Tweet:-
View attachment 1782827
Kama hoja ni mwezi mmoja, kwanini Surpreme Court iwatake Waislamu wa Saudi Arabia peke yake na isiwatake Waislmu kote duniani?!
Ukiitafakari hiyo kauli kwa makini, utagundua hata Saudi Arabia na wenyewe "...wanafunga na kufungua kwa kuuona mwezi kwenye eneo lao, au maeneo ya jirani (gulf) na sio kwingine kokote kule"
And be informed kwamba, Saudi Arabia wanategemea sana astronomical calculations kuliko kuuona mwezi kwa macho, na hivyo tayari wanakuwa na kalenda yao inayoitwa The Umm al-Qura Calendar.
Angalia hii kalenda yao hapa chini:-
View attachment 1783004
Hapo juu nilipozungushia RED, ndo tarehe ya leo kwa kutumia astronomical calculation wanazofanya!!
Hapo chini nilipozungushia blue, ni siku ya Eid mwaka 2029... yaani miaka 9 ijayo, kwamba, kwa kutumia mahesabu yao, mwaka 2029 Eid itakuwa February 14, 2029, kwa maana nyingine mwezi utaonekana February 13.
Watachofanya ni kwamba, ikifika February 12, 2029, wataanza kuutafuta mwezi kwa macho na kwa darubini! Wakiuona, hiyo tarehe itabadilika; wasipouona kwa macho wala darubini, wataendelea kutumia hiyo tarehe waliyoandika hapo!
Msema Kweli ni mpenzi wa Mungu! Nilishawahi kufanya kazi eneo lenye Waislamu wengi na walikuwa wanatumia hiyo The Umm al-Qura Calendar. Kwa miaka 4 niliyokuwa pale, Siku za Eid na kuanza kufunga ziliendana na kalenda ya Saudi Arabia!
But that is another case kwa sababu suala la The Umm al-Qura Calendar au fixed calendar halijatajwa popote kwenye Quran wala Hadith. Na ingawaje mataifa kadhaa ya Ghuba hutumia hiyo kalenda, kuna wengine hawakubaliani na hizo calculations!
Isitoshe, hata hao Saudia walianza kutumia huo mfumo kutokana na maendeleo ya unajimu, na sio kwamba tangu enzi hizo walikuwa wanatumia huo mfumo!