Je sheria inaruhusu uwekezaji wa kujenga Mortuary binafsi

Je sheria inaruhusu uwekezaji wa kujenga Mortuary binafsi

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
6,289
Reaction score
10,998
Habari zenu wadau wa jukwaa hili.. Nichukue nafasi hii kuwataka radhi wale ambao watachukizwa na uzi huu lengo langu ni kupata ushauri juu ya wazo langu la biashara.

Nianze kama ifuatavyo:

Mimi ni mfanya biashara wa huduma ya majeneza na vifaa vingine vya mazishi kiukweli kuna kipindi niliyumba sana kibiashara kutokana na kujiingiza kwenye mikopo mkubwa bank na kuanzisha matawi baadhi ya mikoa ili kujipanua kibiashara ila badae nilijikuta baadhi ya sehemu kama Zanzibar hakuna kabisa biashara ilibidi nifunge kabisa!

Sasa kama ujuavyo biashara yoyote kibongo bongo lazima upambane sana hivyo mwaka jana nililazimika kutafuta wataalamu sehemu tofauti final nikapata mganga mmoja akaninyooshea mambo kiasi kwamba mpaka naanza huu mwaka biashara iko vizuri sana kiasi kwamba nimeweza kukuza mtaji na sasa nimefanikiwa kununua eneo la hekari nne hapa Dodoma eneo liko Nala nje kidogo ya mji

Sasa lengo la huu uzi ni kwamba nilipata wazo la kufanya uwekezaji kwenye hili eneo nililonunua yaani nijenge Mortuary binafsi pia nitengeneze eneo zuri la makaburi ya kulipia kwa wale watu ambao watakuwa na uhitaji

Yaani natengeneza makaburi kwa mpangilio mzuri na panakuwa na garden nzuri na mwonekano mzuri ili hata watu wakijiskia kutembelea kaburi la ndugu yao wanakuja wanakuta kaburi linatunzwa vizuri kama yale makaburi ya ulaya(sijawahi kwenda naonaga kwenye movies)

Sasa sijajua kwa sheria za nchi yetu naruhusiwa kuanzisha mortuary binafsi na kuajili wataalamu kama ilivyo dispensary?

Na pia naruhusiwa kumiliki eneo la makaburi ya kulipia?

Naomba pia kwa mwenye uelewa wa gharama za kuanzia ujenzi, vifaa na kila kitu mpaka kukamilisha kuwa na Mortuary binafsi.
Natanguliza shukrani.
 
Mortuary ni gharama..

Majokofu sana sana..

Baadhi ya hospital kubwa tu za Serikali hazina Mortuary.

Imagine watu wanahifadhi mwili wa mpendwa wao alafu hawaji kuuchukua on time, na wakija wanasema hawana hela.. utafanyaje?

Makaburi ya kulipia ni idea nzuri, je yatakuw na dini zote?

Pia nashaur ktk wazo lako uweke na ile sehem ya kuchomea kabisa (Crematorium).

Pia sehem ya kuosha kwa dini zote.. na sehem ya embalming iwe safi..
 
Boresha au anzisha huduma ya mazishi iliyo classic kama uchagani.
▪️Uwe na gari maalumu za kubeba majeneza, Mercedes benz na escort nzuri. Weka kwa mfumo wa package
▪️Uwe na mashine ya kushusha jeneza ndani ya kaburi..full automated
▪️Uwe na MC, vyombo vya music ikiwezekana na waimbaji.
▪️Huduma ya chakula msibani.. buffet.
Kwa kifupi ukipewa tukio la msiba unaweza toa huduma zote
 
Back
Top Bottom