Je, sheria ya makosa ya kimtandao hapa kwetu Tanzania ni sheria kandamizi?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Natoa angalizo mapema kabisa mimi sio mtaalamu wa masuala ya sheria. Ila nimeuliza hili swali nipate msaada. The Cyber crimes Act,2015 .Ni sheria kandamizi?

Kwa sababu ni wazi kabisa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni umewekwa wazi katika katiba ya JMT ibara ya 18 kujieleza huku katika katiba ya JMT ni pamoja na kutoa taarifa ambazo kwa namna moja au nyingine ni msaada kwa jamii.

Sasa ukija kwenye hii sheria ya makosa ya kimtandao kuna kuwa na ukakasi huko kujieleza kumebanwa na hii sheria au?

Au kuna tatizo watu hawakupewa elimu ya kutosha kwamba hii ni sheria na ni Act of parliament.Kwamba imetungwa na Bunge na ikianza kufanya kazi ina kuwa binding.

Sitaki kuongea mengi sana ila ukiangalia tu kifungu cha 22(1) utaona kwamba kuna shughuli pevu hapa kwa watumiaji wa mitandao.

Kifungu cha 23 kinacho husika na Cyber bullying ni hatari kabisa. Mtu ana tweet "Waziri Mijicho" alafu anaweka na picha yake.

Kwa hii sheria watu wengi wataumia sababu tu wengi hawana elimu juu yake. Nasisitiza elimu kubwa inahitajika watu wajue kwamba kuna sheria ambayo ilipitishwa na Bunge na ambayo inakupasa uwe makini sana unapotumia mitandao.

Sheria kama hizi zimepitiswa na nchi nyingi ili kuzuia uhalifu wa kimtandao. Na nina uhakika sio Tz tu hata Us na nchi za majuu wana sheria kama hii.
 
Pipa na funiko
Kama hujui ni sheria ipi itakulinda unapoandika kitu ambacho kitachafua watu au Serikali, basi busara pekee ya kuepuka kuvunja sheria ni kuwa msomaji tu.

In God we Trust
 
Sheria ya faragha ndiyo itaondoa huo mzozo
 
Hiyo sheria ilitungwa na wabunge vilaza wa ccm nasahivi ndo imekuwa mkuki wakuchoma watu ...kila mtu anayemkosoa Jambazi mkuu anakamatwa.
Ila mle mjengoni wabunge wa Chadema,Cuf na Act walikuwemo na ndio walioipitisha.
 
Yuko hospitali pale kijitonyama. Unaweza kwenda kumwona, ukifika getini waambie 'cactus', watakuelewa.
 
Natoa angalizo mapema kabisa mimi sio mtaalamu wa masuala ya sheria. Ila nimeuliza hili swali nipate msaada. The Cyber crimes Act,2015 .Ni sheria kandamizi?

Kwa sababu ni wazi kabisa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni umewekwa wazi katika katiba ya JMT ibara ya 18 kujieleza huku katika katiba ya JMT ni pamoja na kutoa taarifa ambazo kwa namna moja au nyingine ni msaada kwa jamii.

Sasa ukija kwenye hii sheria ya makosa ya kimtandao kuna kuwa na ukakasi huko kujieleza kumebanwa na hii sheria au?

Au kuna tatizo watu hawakupewa elimu ya kutosha kwamba hii ni sheria na ni Act of parliament.Kwamba imetungwa na Bunge na ikianza kufanya kazi ina kuwa binding.

Sitaki kuongea mengi sana ila ukiangalia tu kifungu cha 22(1) utaona kwamba kuna shughuli pevu hapa kwa watumiaji wa mitandao.

Kifungu cha 23 kinacho husika na Cyber bullying ni hatari kabisa. Mtu ana tweet "Waziri Mijicho" alafu anaweka na picha yake.

Kwa hii sheria watu wengi wataumia sababu tu wengi hawana elimu juu yake. Nasisitiza elimu kubwa inahitajika watu wajue kwamba kuna sheria ambayo ilipitishwa na Bunge na ambayo inakupasa uwe makini sana unapotumia mitandao.

Sheria kama hizi zimepitiswa na nchi nyingi ili kuzuia uhalifu wa kimtandao. Na nina uhakika sio Tz tu hata Us na nchi za majuu wana sheria kama hii.
Kwa Africa huwa ni maalumu zimewalenga wakosoaji watu waonyeshao udhaifu,wizi,upigaji wa watawala.Watawala upenda kuonekana wasafi mbele za watu madhaifu yao,kuboronga kwao kusiwekwe peupe.Nje ya Africa watawala uwategemea Sana wakosoaji kama kioo Chao kutojikwaa wasianguke kutaka kujua jamii yao inataka nn,inawaonaje,wapi waboreshe,uwatumia wakosoaji positively thus wanapata matokeo mazuri maana kioo cha mtu ni watu.
 
Kama hujui ni sheria ipi itakulinda unapoandika kitu ambacho kitachafua watu au Serikali, basi busara pekee ya kuepuka kuvunja sheria ni kuwa msomaji tu.
Au utumie codes zenye tafsiri tofauti iliyo ngumu kueleweka kisheria but ujumbe umefika.Sheria sio hesabu jibu liwe moja ni uwezo wako binafsi kucheza na tafsiri ya neno kwa neno
 
Kwa Africa huwa ni maalumu zimewalenga wakosoaji watu waonyeshao udhaifu,wizi,upigaji wa watawala.Watawala upenda kuonekana wasafi mbele za watu madhaifu yao,kuboronga kwao kusiwekwe peupe.Nje ya Africa watawala uwategemea Sana wakosoaji kama kioo Chao kutojikwaa wasianguke kutaka kujua jamii yao inataka nn,inawaonaje,wapi waboreshe,uwatumia wakosoaji positively thus wanapata matokeo mazuri maana kioo cha mtu ni watu.
Suala sio kukosoa ,kuonyesha madhaifu ya viongozi na kuibua madudu. Suala la msingi unakosoa vipi? Na unatumia lugha ya staha? Ndio nasisitiza watu waelewe hii sheria ipo. Na watu wawe makini sana.
 
Back
Top Bottom