SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wazee wa vichaka hauwasikii tena wakiongelea habari za kubeba mafyekeo. Kelele zilikuwa kwa ajili ya kujaza watu uwanjani, zoezi ninalosikia halikufanikiwa. Wamekwenda machakani, wamekuta vyura wenzao wamezaliana, zoezi likasitishwa.
Tuachane na hayo, turudi kwenye mada kuu.
Simba ina nafasi ya kubeba ndoo ya CAF Shirikisho msimu huu wa 2024-25. Ikifanikiwa hilo inaenda kuwa top 5 katika orodha ya ubora Afrika au kwa kimombo, "ranking".
Simba ikiwa bingwa inaweza kushika nafasi ya 3 iwapo mambo haya yatatokea -
Mamelodi isifike nusu fainali halafu TP Mazembe wala Zamalek wasifike fainali. Haya yote yanawezekana kutokana na ushindani katika mashindano yao na ubora wa wapinzani wao.
Esperance asipovuka kwenda robo fainali, Simba ina nafasi ya kuwa hata nafasi ya 2 iwapo itabeba ndoo. Hii ni ngumu kutokana na performance ya Esperance ya miaka ya karibuni lakini nataka sana Utopolo waendelee kutufanyia kazi hizi chafu kama walivyotufanyia msimu uliopita kwa CRB. Yanga wamekuwa kama watumwa wa Simba katika mashindano ya kimataifa, tunamtuma tu, embu kamuondoe yule ili tusogee juu kidogo na wenyewe kwa raha zao wanaifanya kazi kwa weledi.
Nipo hapa nampigia Motsepe awapange Yanga katika kundi moja na Esperance au Mamelodi, wampunguze mmoja halafu na yeye robo fainali atupiliwe mbali arudi kucheza na Dodoma Jiji.