Android ni
jina la aina ya
mfumo huria wa uendeshaji wa
simu za mikononi. Mfumo huo hutumiwa hasa katika
simujanja, kama vile
Google inavyomiliki
Google Nexus, vilevile
kampuni nyingine zinafanya vivyohivyo ikiwa ni pamoja na
HTC na
Samsung. Mfumo huo wa uendeshaji umepata kutumika pia katika
kompyuta bapa kama vile
Motorola,
Xoom na
Amazon Kindle Fire.
[1]

Android logo 2023
Google imetoa pia Android nyingine kama vile
Android TV ya
televisheni,
Android Auto ya
magari,
Android Things kwa ajili ya
vifaajanja na
Wear OS ya
saa ya mkononi. Aina nyingine za Android hutumiwa pia kwa
michezo ya kompyuta na
kamera za
kidijiti.
Android mwanzoni iliundwa na
Android Inc. kabla ya kununuliwa na Google mwaka
2005. Matumizi rasmi ya
kibiashara yalianza mnamo Septemba
2008. Toka mwaka huo Android imetoa matoleo mbalimbali. Toleo la sasa ni
9 "Pie" lililotolewa Agosti
2018. Android Q beta ilitolewa
Machi 13,
2019. Programu ya msingi ya Android inaitwa Android Open Source Project (AOSP) ambayo hutolewa kwa
Leseni ya Apache.
Google inasema zaidi ya
simujanja milioni 1.3 zenye mfumo wa Android zinauzwa kila
siku.
[2] Hii imeifanya Android kuwa miongoni mwa mifumo ya uendeshaji wa simu inayotumika sana duniani.
Copy&pest
Kuwakimbia wamarekani itakua kazi nzito sana...
View attachment 3392415