Je, Spika Ndugai asaidiwe kisaikolojia au aachwe?

Nimefanya magazijuto, wapi! Nikarudia hesabu za chekechea, wapi! Nikasema nijaribu primary, wapi! Kwa ufupi huo mnyumbulisho sijauelewa kabisa.

Anaposema jumla ya wajumbe ilikua 30 na alipata zote, inamaana TAL alipata zero. Unapomuwekea jamaa 24 na yeye akapata 30 ni kusema jumla ya wajumbe ilikua 54.

Lazima kuna mtu hasemi ukweli hapo.
Hakujiandaa
 
Wanasema tusihangaike naye kuna maono juu yake yatatimia baada ya muda mfupi
 
Kwani hao wabunge wasipokuwepo bungeni ww unapata faida gani?

Kitu gani kinaongezeka?

Au na ww ni kama wale viongozi wako ambao walishawaweka wake zao na wale wanawake ambao walishalipa milion kumi kumi?

Ww ni mmoja kati ya hao wabunge nini? Maana hii mada huwa inakukwaza sana. Kwani kuna ulazima gani wa ww kuwepo huko bungeni?
 
Ndugai tatizo lake jingine anajisahau.Yeye ni speaker wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.Siyo speaker wa ccm.Aache mambo ya kujibishana kichama chama,Chadema wakiamua kufanya naye bifu kibinafsi,itashusha heshima yake katika jamii.Ukibeep watu wanakupigia.Chadema inawafuasi wengi,kwenye kampeni za Lisu mwaka jana inazihirisha hilo.Wakiamua wafanye naye beef hatobaki salama.Kwanza hata Bungeni chadema hawapo,yeye angekomaa na kutoa umasikini kwa watanzania.Siyo mabeef.
Yeye kapewa zamana ya uongozi afanye kazi,hasa ya kuwatoa umasikini uliopitiliza kwa wananchi wa jimbo lake la Kongwa
tushaanza kampeni tayari - ya kumtangaza jamaa kama maajabu ya dunia !! watu waje wamshuhudie ni kivutio kingine kipya cha utalii wa ndani na nje ya nchi.
 
Ww ni mmoja kati ya hao wabunge nini? Maana hii mada huwa inakukwaza sana. Kwani kuna ulazima gani wa ww kuwepo huko bungeni?

Ulazima upo mkubwa tu
Kwani wasipokuwepo ww unadhirika na nn?
 
Dunia kuna vituko sana, Moja ya vituko vinapatikana Bungeni vikiongozwa na Job Ndugai. Huyu Ndugai anajulikana kama mheshimiwa Spika.

Leo Ndugai ametumia dakika nyingi Bungeni akitaka kutetea legacy yake na kujifananisha na Spika Marehamu Samwel Sitta, Ndugai anaumia na kukwazika sana kwanini watu walimuheshimu Samwel Sitta na kuheshimu Bunge la tisa la Samwel Sitta.

Ndugai amejitahidi kulia na kubembeleza kwa wabunge kuwa naye atajitahidi kuandika mambo aliyoyafanya ili watu wamuelewe, Je mbona Samwel Sitta hajaandika popote legacy yake lakini anakumbukwa.

Ndugai ni moja ya Spika atakaye Kumbukwa kwa maovu na ukatili wa hali ya juu kinyume na mwanadamu wa kawaida.

Ndugai asipojirekebisha ataunganishwa na mwendazake kama watu walioharibu Uchumi wa nchi mpaka kufika ukuaji wa asilimia 4% ambao watu wengi wamepoteza ajira.

Ndugai atakumbukwa kama mtu asiyekuwa na busara na Hekima kwa maamuzi yake yaliyoharibu Taifa.

Maamuzi ya kupitisha sheria uchwara kama za uhujumu Uchumi ili kumfurahisha mwendazake, Bila aibu Ndugai anashawishi sheria hizi sasa ziletwe Bungeni tena baada ya kuona upepo umekaa hovyo.

Ndugai ameshiriki kupitisha sheria za mifuko ya jamii kandamizi ili kuwaumiza wastaafu, Mifuko ya jamii iliunganishwa na pesa kufilisiwa kwa kisingizio zinajenga miradi, Leo Mama Samia anapata wakati mgumu sana.

Ndugai atakumbukwa kama mtu aliyegeuza Bunge genge la watu wasiojielewa ambao kazi yake imekuwa kuzurula na mwendazake kila kona wakati wa kuzindua miradi, Ndugai alipokea maagizo hata ya kuwanyima stahiki zake wabunge kama Tundu Lissu.

Ndugai Leo amepoteza muda kujibu hoja za Nape kwa aibu kubwa, Ndugai bado haamini kama Mwendazake hayupo alishatangulia, Nina uhakika kauli ya Nape kuwa wabunge wale 19 na chadema wapo pale sio kihalali angetamka wakati ule Ndugai angemfukuza Nape Bungeni ili kumfurahisha Mwendazake.

Hawa ni viongozi wa kitaifa lakini mwisho wa siku wataandikwa kwenye historia kama moja ya watu pekee kutokea Tanzania walioendesha nchi kama gari bovu isiyokuwa na sheria, kanuni na taratibu.

Hakika Ndugai atatumia muda mwingi kutetea legacy yake huku akisahau legacy inajitetea yenyewe.

Pole Sana Mheshimiwa Ndugai, Tafuta mwalimu wa Saikolojia aliyekufunza ukatili hayupo tena.
aachwe, ni pyschological healing.
 
Sijui kama mwana sheria mkuu wa serikali ana fanya kazi yake sahihi hapo bungeni
Angekuwa ana mshauri Ndugai kuhusu sheria za nchi na utii wa katiba, Ndugai hange fanya huu uharo anao fanya
Kwa kifupi huyu mwanasheria anaingia kwenye kundi la covid.
Nashauri kabla Mh Rais hajachukua hatua ya kuingilia kati huu mgogoro kati ya bunge na Chadema, aondoke kwanza na mwanasheria wa serikali.
 
Ndugai endelea kupiga spana hizi nyumbu hadi akili iingie vema.
Kwahiyo Mama Samia aliyesema kuwa mijadala ya wabunge haina afya kwa taifa naye ni nyumbu aliyepigwa spana na Ndugai?
 
Kwani hao wabunge wasipokuwepo bungeni ww unapata faida gani?

Kitu gani kinaongezeka?

Au na ww ni kama wale viongozi wako ambao walishawaweka wake zao na wale wanawake ambao walishalipa milion kumi kumi?
Hili ndilo tatizo la kuwazia kupitia mlango wa fahamu wa nyuma.
Yaan ww unaona kawaida tu watu 19 ambao hawana sifa ya ubunge kulipwa tsh 11 per month. Kwa nn hizo pesa zisisaidie wahitaji ? Bora zinunue madawa wagonjwa wapate kupona.
 
Hivi sasa Watanzania kuongozwa na viongozi wagonjwa si jambo la ajabu tena. Ingawa tumebahatika kuondokana na moja, wengi bado wametamalaki.

Ndugai ni mgonjwa na hilo kila mtu analifahamu. Ugonjwa wake si siri na hilo kila moja analifahamu. Cha kujiuliza ni watanzania tumefikaje hapa.

Kama tuliweza kuvumilia hali hiyo kwa miaka mitano, tusife moyo. Ipo siku tutaamka na kukuta maombi yetu yamejibiwa hivyo tusikate tamaa.

Katiba ya nchi ina uwezo wa kujilinda na inapochokozwa inajibu mapigo. Wote waliojaribu kuisigina Katiba kwa namna yoyote ile, walilipa kwa namna fulani.
 
Dunia kuna vituko sana, Moja ya vituko vinapatikana Bungeni vikiongozwa na Job Ndugai. Huyu Ndugai anajulikana kama mheshimiwa Spika.

Leo Ndugai ametumia dakika nyingi Bungeni akitaka kutetea legacy yake na kujifananisha na Spika Marehamu Samwel Sitta, Ndugai anaumia na kukwazika sana kwanini watu walimuheshimu Samwel Sitta na kuheshimu Bunge la tisa la Samwel Sitta.

Ndugai amejitahidi kulia na kubembeleza kwa wabunge kuwa naye atajitahidi kuandika mambo aliyoyafanya ili watu wamuelewe, Je mbona Samwel Sitta hajaandika popote legacy yake lakini anakumbukwa.

Ndugai ni moja ya Spika atakaye Kumbukwa kwa maovu na ukatili wa hali ya juu kinyume na mwanadamu wa kawaida.

Ndugai asipojirekebisha ataunganishwa na mwendazake kama watu walioharibu Uchumi wa nchi mpaka kufika ukuaji wa asilimia 4% ambao watu wengi wamepoteza ajira.

Ndugai atakumbukwa kama mtu asiyekuwa na busara na Hekima kwa maamuzi yake yaliyoharibu Taifa.

Maamuzi ya kupitisha sheria uchwara kama za uhujumu Uchumi ili kumfurahisha mwendazake, Bila aibu Ndugai anashawishi sheria hizi sasa ziletwe Bungeni tena baada ya kuona upepo umekaa hovyo.

Ndugai ameshiriki kupitisha sheria za mifuko ya jamii kandamizi ili kuwaumiza wastaafu, Mifuko ya jamii iliunganishwa na pesa kufilisiwa kwa kisingizio zinajenga miradi, Leo Mama Samia anapata wakati mgumu sana.

Ndugai atakumbukwa kama mtu aliyegeuza Bunge genge la watu wasiojielewa ambao kazi yake imekuwa kuzurula na mwendazake kila kona wakati wa kuzindua miradi, Ndugai alipokea maagizo hata ya kuwanyima stahiki zake wabunge kama Tundu Lissu.

Ndugai Leo amepoteza muda kujibu hoja za Nape kwa aibu kubwa, Ndugai bado haamini kama Mwendazake hayupo alishatangulia, Nina uhakika kauli ya Nape kuwa wabunge wale 19 na chadema wapo pale sio kihalali angetamka wakati ule Ndugai angemfukuza Nape Bungeni ili kumfurahisha Mwendazake.

Hawa ni viongozi wa kitaifa lakini mwisho wa siku wataandikwa kwenye historia kama moja ya watu pekee kutokea Tanzania walioendesha nchi kama gari bovu isiyokuwa na sheria, kanuni na taratibu.

Hakika Ndugai atatumia muda mwingi kutetea legacy yake huku akisahau legacy inajitetea yenyewe.

Pole Sana Mheshimiwa Ndugai, Tafuta mwalimu wa Saikolojia aliyekufunza ukatili hayupo tena.
****** is a lost cause. HAIWEZEKANI tena kumleta kwenye ubinadamu. Kwanza ni mtaalamu wa wanyama pori by profession hivyo amezoea kuona wanyama wakitafuna wanyama wenzao (cannibalism).

Pili VVU vimekamata ubongo, ni Mungu atende kama alivyotenda kwa Mwendazake
 
Back
Top Bottom