Je, taarifa binafsi (Mitihani na CV's) zinazotumiwa kama vifungashio na wafanyabiashara zinatoka wapi?

Je, taarifa binafsi (Mitihani na CV's) zinazotumiwa kama vifungashio na wafanyabiashara zinatoka wapi?

Kuna watu uwa wanatembelea maofisi mbalimbali wakiwa na pesa mfukoni wakitafuta nyaraka zisizotumika ili wakatengeneze hivyo vifungashio. Sasa hapo utegemea na sera za utunzaji wa nyaraka kwa kila taasisi na kukiwa na mianya basi watu wa masjala uwa ni fursa kwao kufanya biashara na hao watafuta nyaraka kwa bei chee.
 
Haya twende sawa.

Nafasi ya kazi inatangazwa moja, wanafanya maombi watu mia 5 kupitia posta...
Umemaliza kilakitu hapa...makampuni yote Tanzania huwa wanachukua maombi Kwa njia ya makaratasi.
Mtoa mada ameona mbali Sana
 
Taarifa Binafsi ni maelezo fulani ambayo yanamtambulisha mtu, au kueleza jambo fulani kuhusu maisha yake.
Taarifa Binafsi huweza kuwa majina ya mtu, namba ya simu, mwaka na tarehe ya kuzaliwa, dini, kabila, mahali anapoishi na mengineyo yanayombainisha mtu fulani.
Nimenunua vitafunwa Asbh nikapewa kwenye Bahasha hii;

1654671684193656064039912683575.jpg
 
Hiyo tu? Zipo mpaka salary slip zikionesha mpaka mikopo iliyokopwa benki na kiasi cha mshahara anayolipwa. Hizi nyaraka huwa zinatupwa kizembe kwenye madampo ya ofisi hizo baada ya kuonekana hazitumiki tena.
Hizo karatasi ni dili sana zinauzwa Kwa kilo Kwa watengenezaji vifungashio pale mbagala rangi 3 kuna maduka wanauza hizo karatasi Kwa kilogrammes....ni biashara kubwa Sana
 
Kuna tabia ile ya kutuma tuma application hovyo bila mpangilio kwa lengo la kubahatisha ajira matokeo yake ndio haya.

Mtu unafanya application 100 kwa mwaka unategemea nini kitokee. Unakuta mtu anawatumia kampuni bahasha hata kumi kwa mwaka akiomba kazi nafasi tofauti tofauti hadi kampuni wanamfahamu na kumzoea kwa barua hadi majina.

Masecretary huwa hizi bahasha wanatumbukiza tu kwenye trashcan au kuzigawa kwa watu wanaotafuta raw materials za kutengeza paper envelopes au vifungashio.

Ni vema tukajifunza kuwa academic documents zinatakiwa kuwa handled with maximum care sababu zinabeba taarifa zako nyeti za kitaaluma na kiweledi.

Usiwe mwepesi sana kuprint vyeti na CV documents zako kumpa mtu randomly kisa tu kaahidi kukusaidia ajira na mwisho wa siku usihoji documents zako zimehifadhiwa wapi.

Ngoja niwape siri leo.

Kuna dada nilipewa kisa chake kuwa alipata ajira mizani mwaka 2016. Alipoingia kulianza kampeni ya serikali kupekuwa vyeti feki. Yeye ni miongoni mwa watu walirudishwa nyumbani na kusimamishwa kazi sababu ya utata wa vyeti vyake kuonekana ni feki na forgery.

Ilibidi jitihada za ziada kufautilia. Ikaja kuonekana kuna mdada anatumia jina lake na amesomea vyeti vyake vya form four na six katika kusomea level ya masters degree na yupo kazini wizarani kitambo.

Sasa kwasababu issue ilikuwa ni ya moto yule dada wa wizarani ambaye inasemekana ni mchepuko wa kigogo wa serikalini alimtafuta bi dada kwa simu na kuomba waonane ili amtafutie mchongo kwenye kampuni binafsi aachane na habari ya kufatilia maswala ya vyeti na kuprove huko wizarani na maswala ya mahakamani kutoa viapo na kadhalika.

Bi dada walionana na alilipwa milioni 10+ kisha alitafutiwa ajira kampuni binafsi inayofanya kazi na TCRA hapo. Msala ukaishia hapo maisha yakaendelea.

Miongoni mwetu kuna watu vyeti vina ufaulu mzuri ila kwasababu ya kukosa access na support ya kupata ajira serikalini tumejikuta tunasusa kufuatilia ajira tunapambana na maisha kwa deals na codes za mtaani plus kufukuzia michongo na kampuni binafsi tu maana serikalini hakuingiliki. Ila kuna mamia ya bahasha zetu zikiwa na full package ya hizo documents zetu zimezagaa kusikojulikana huko kiasi kwamba zinakuwa rehani na accessible kwa watu ambao wanaweza kufanya lolote kutokana na uwezo walionao na watu wanaoweza washika mkono.

Vyeti siku hizi vinatengenezwa tu. Kwann ishindikane kutumia taarifa zako kutengeneza copy yako ambayo itaenda kusoma na kujiendeleza kielimu kutokana na vyeti vyako vya sekondari ambavyo umeshavitosa kabatini na huna kazi navyo tena miaka 10 ijayo utaajiriwa na nani una miaka 45+ [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Sasa its better kama unakabidhisha documents zako basi kuwa na uhakika zinakwenda wapi na ni nani anazipokea na kuzifanyia kazi. Nje ya hapo acheni kutuma tuma bahasha zenye nyaraka zako za kitaaluma kwenye maofisi na haujui zitakuwa handled na nani wala watazihandle vipi baada ya kuzisoma.

Asante
 
Njaa hii nifungiwe kitumbua nianze kusoma? Akitokea mwingine kuomba aah sina hiyo time, kwanza karatasi yenyewe inajaa mafuta tu wala hayasomeki
 
Kuna watu uwa wanatembelea maofisi mbalimbali wakiwa na pesa mfukoni wakitafuta nyaraka zisizotumika ili wakatengeneze hivyo vifungashio. Sasa hapo utegemea na sera za utunzaji wa nyaraka kwa kila taasisi na kukiwa na mianya basi watu wa masjala uwa ni fursa kwao kufanya biashara na hao watafuta nyaraka kwa bei chee.
Ni kweli kabisa nafikiri inahitajika elimu kwa watu hawa
 
Back
Top Bottom