Papy ndombe
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 3,761
- 4,535
Wameshauliwa Sana wawape polisi awataki kusikiaHuku mitaani mabaa kibao, wale wadada wanalipwa kati ya 80'000/- up to 180'000/- wawape neema hao jamani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wameshauliwa Sana wawape polisi awataki kusikiaHuku mitaani mabaa kibao, wale wadada wanalipwa kati ya 80'000/- up to 180'000/- wawape neema hao jamani.
Hana njaaYawezekana kabisa wameshindwa kuwanunua akina mbowe
CCM wanakutumia alafu wanakuacha unashangaa, ndivyo itakavyokuwa kwa hao akina Halima na wenzake
BrightgNakupa swali moja upime utajua ni ya kweli au ya uongo. Huyu dada aliyekuwepo magereza chadema ilijua ni lini atatoka ili wamuorodheshe kwenye viti maalum? je ni jitihada za chedema kuwa huyu dada atolewe usiku magereza ili aapishwe asubuhi? sasa waliandikaje jina la mtu ambaye hawajui lini atatoka magereza.
Hayo Nayo ni maajabu mengine ya duniaTume inaleta maajabu ya mtu kulala mfungwa kuamka mbunge.
Why wasiteue toka vyama vingine coz cdm awazitaki nafasi hizo
mkulima gwakikolo
Utashangaa kuona kuwa Spika Ndugai atavunja kanuni zilizotungwa na Bunge lake lenyewe, kuwa mbunge akishafukuzwa uanachama na chama kilichomdhamini kuingia Bungeni humo, automatically anakuwa amepoteza nafasi yake ya ubunge, lakini katika suala hili la wabunge wa viti maalum wa Chadema, atajifanya kaweka pamba masikioni na ataendelea kuwakumbatia!
Sasa tumuulize Spika Ndugai kama ataendelea kuwakumbatia wabunge hao, watakuwa ni kutoka chama gani?
Je atakuwa amevunja Katiba ya nchi hii ambayo INALAZIMISHA kuwa sharti mbunge yeyote ndani ya nchi atokane na chama cha siasa?
Kwa kuwa chama wanachotoka wabunge hao cha Chadema, kupitia kikao chao cha Kamati Kuu wameutangazia Umma kuwa wameshawafukuza uanachama wao katika chama hicho
Hivi hawa CCM katika watu wote makini walionao, ilikuwaje wakamuweka huyu Zinjathropus Ikulu? Jamaa anaishi zama za mawe katika zama za taarifa
Ya kipumbavu sana.Mambo yanayofanywa na tume ya uchaguzi ni ya kihuni Sana.
He will never answer. He is not credible any more.Nimesoma kitu kinachoitwa TAARIFA KWA UMMA iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi, iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Dkt Mahera, tarehe 27/11/2020, naomba maswali yafuatayo uyajibu Dkt Mahera:-
1. Katika taarifa yako kwa Umma umedai kuwa ulipokea majina hayo ya wabunge wa viti maalum, toka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, tarehe 19/11/2020, je taarifa hiyo ilikuwaje iwe na jina la Nasrat Hanje, ambaye alitolewa gerezani rumande, usiku wa tarehe 23/11/2020 kwa amri ya DPP, Biswalo Mganga, ambako Jeshi lenu la Polisi lilimbambikia kesi ya kukusanyika bila kibali na kutompa dhamana pasipo halali, ambapo alikaa rumande kwa siku 133?
2. Tunakuomba Mkurugenzi wa uchaguzi, Dkt Maheta uutangazie Ulimwengu kuwa kauli tuliyosikia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema aliyoitoa kwenye kikao na waandishi wa habari hapo tarehe 26/11/2020 kuwa form zenu za Tume ya uchaguzi, alikuwa nazo ofisini kwake zikiwa hazijajazwa hata kidogo na kuwa form hizo hazijatumwa kwenye Tume yenu ya uchaguzi, kuwa ilikuwa ni kauli ya uwongo?
3. Iweje Bunge la Jamhuri la Muungano, chini ya Spika wake Job Ndugai na Katibu wake, Kigaigai, wakiuke kanuni zake yenyewe na kuwaapisha "kisiri siri" tena kwenye eneo nje ya Bunge wabunge hao wa viti maalum, wakati kanuni zinawataka ni LAZIMA tendo hilo lifanyike rasmi ndani ya Jengo la Bunge, kwa kuwa tendo hilo siyo la unyago, ambalo lingehitaji usiri mkubwa?
4. Iweje Spika wa Bunge, Job Ndugai anukuliwe kwa kutoa taarifa kuwa Bunge lake litawalinda kwa gharama zozote wabunge hao wa viti maalum wa Chadema, kama ambaye anajua kuwa uapishwaji wao ulikuwa batili?
5. Iweje Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt Mahera usitoe taarifa hiyo nyeti mapema, hadi ungojee sakata hilo la wabunge wa viti maalum wa Chadema, li-trend sana kwenye social media na usubiri chama kikuu cha upiinzani nchini Chadema, kiitishe kikao chao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chama chao kuwajadili hao ambao mmewahalalisha kuwa wabunge wateule wa viti maalum!
Kama Dkt Mahera amethubutu kutupa taarifa za uwongo kuhusiana na suala la kuapishwa kwa wabunge wa viti maalum wa Chadema, tunawezaje kumuamini kwa taarifa aliyotupa ya matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambayo kwa mujibu wake kuwa Rais Magufuli alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura milioni 12 ambayo ni zaidi ya asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa nchini?
Naomba hayo maswali machache unijibie Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt Mahera ili kuondoa huu utata mkubwa uliogubika zoezi hili zima la kuwaapisha hao wabunge wa viti maalum wa Chadema.