Je, Taifa linahita toba kuwanusuru viongozi waandamizi kutwaliwa?

Je, Taifa linahita toba kuwanusuru viongozi waandamizi kutwaliwa?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Kiimani yapo mapigo umfanya mwanadamu kuhojiana na Muumba kuhusu tafsiri ya kile kinachotokea. Kwenye bibla tunasoma miaka Saba ya njaa na Saba ya shibe, tunasoma kuuwawa kwa watoto wote wa kiume kwa amri ya mfalme na tunasoma namna machukizo ya wanna wa Israeli yalivyo wapa mapigo safarini kutoka Misri. Haya tunayasoma yatusaidie kuzitambua nyakati na majira yakuogofya au kufurahisha.

Tukiri, tumepoteza viongozi wengi sana kwa kipindi kifupi. Kiimani tunasema ni mpango wa Mungu lakini pia kwa mapigo haya tunaweza kumuuliza Mungu Kama muda ulifika au aliwaondoa kwa lengo la Taifa kujifanyia toba? Tusipoangalia Jambo hili kiroho itakuwa ngumu kulifanyia toba endapo linahitaji toba.

Tunao umuhimu wakumuuliza Mungu Kama kweli viongozi tunaowapata wanatoka kwake kama imani yetu itutumavyo? Endapo hawatoki kwake ni kipi tufanye atupe wadumuo?

Naomba tutafakari sana Jambo hili maana linagusa viongozi na hivyo lina athari kubwa hasa kiuchumi. Akiondoka mbunge mtarejea uchaguzi, akiondoka Rais mtastructure serikali upya. Hizi gharama za kufanya haya zingeweza kuelekezwa kwingine , hivyo tunaweza tukaona kwamba suala hili lisipotafakariwa kiroho lina athari za kiuchumi,kisiasa na kijamii.

Tumwombe Mwenyenzi Mungu atufunulie tupaswayo kuyafanya, awalinde viongozi lakini pia atupe watu sahihi.

Sabato njema ndugu zangu
 
Enyi vizazi mlkokosa imani, mpaka lini mtaacha kujiangaisha na mambo yasiyowahusu.

Taifa hili mwaka juzi na jana tulifanya maombi ili Mungu atunusuru na ugonjwa wa Corona, pia mwaka jana Taifa liliomba Mungu asimamie uchaguzi mkuu.

Mungu alitusikia na kwa sasa anatenda, hivyo atuna sababu yeyote ya kujiangaisha tena na mambo ambayo tulikwisha mwachia Mungu.

Kazi tuliyonayo kwa sasa ni moja.
"KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO"
 
We unaamini wote wanatwaliwa kwa mpango wa Mungu? Killuminati wapo kazini endelea kujiongopea
 
Watu walishiriki katika uongozi ambao ulikuwa unabaka wananchi,unalawiti wananchi,kuteka watu,kutesa,kuua,ukabila,ukanda,udini,ubaguzi wa rangi,kuua demokrasia,kuua uhuru wa kujieleza,kuiba kura,kuua uchumi na kadhalika.Sasa unategemea kuwa watu kama hawa laana/karma isiwatafune?Are you serious?
 
Enyi vizazi mlkokosa imani, mpaka lini mtaacha kujiangaisha na mambo yasiyowahusu.

Taifa hili mwaka juzi na jana tulifanya maombi ili Mungu atunusuru na ugonjwa wa Corona, pia mwaka jana Taifa liliomba Mungu asimamie uchaguzi mkuu.

Mungu alitusikia na kwa sasa anatenda, hivyo atuna sababu yeyote ya kujiangaisha tena na mambo ambayo tulikwisha mwachia Mungu.

Kazi tuliyonayo kwa sasa ni moja.
"KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO"
😆😆😆
 
Back
Top Bottom