Je, Tanzania inahitaji BBI kama Kenya?

Je, Tanzania inahitaji BBI kama Kenya?

Je na Tanzania nasi tunahitaji BBI?
Kwanza kuwaza tu kuanzisha kitu kama hicho sijui utaanzia wapi wakati upande mmoja ukijiona una nguvu zote na mabunduki yote ya kuwanyamazisha wa upande wa pili.

Kumbuka chimbuko lake..., ni baada ya uchaguzi mkuu wenye utata sana ambao hadi mahakama kwa mara ya kwanza Afrika, wakafuta ushindi wa aliyetangazwa kuwa ameshinda.

Hata baada ya uchaguzi kurudiwa na wapinzani (Odinga) kuugomea uchaguzi wa marudio, hali haikuwanzuri.

Uhuru Kenyatta akaapishwa kuwa Rais; lakini Odinga naye kang'ang'ana na kuapishwa kama Rais wa wananchi (People's President).
Sasa jiulize mwenyewe, ingekuwa hapa kwetu, Odinga kweli asingekuwa mahali pasipofaa kwa sasa au futi sita chini? Jiulize hilo bila unafiki, hakuna atakayejua ulichojibu.
 
Kenya wanaishi watu, Tanzania wanakaa nyumbu, kila jambo wao ni kufuata na kusifia tu, bado tuna safari ndefu sana miaka zaidi ya 100,na bila kutoana ngeu huko hatufiki ng'o.hatuwe
Watawala wanaona kama wanaongoza mazombie hawana hofu yoyote.
Kama mazombi niliyoona juzi ufipa yakisifia na kuabudu dj, hatuwezi kufika.
 
Chadema kwa kuwa ndio chama kikuu cha upinzani, kinapaswa kuyachukua haya na kuyawekea kipaumbele kuelekea uchaguzi wa 2020. Hizi ndizo zilizokuwa Sera za Maalim seif, na ndizo zilizopelekea kushinda chaguzi nyingi za nyuma ingawa hakuthibitishwa.

CDM Mubadilike. Else wanajukwaa kwa Sera hizi naamini ni wakati muafaka wa wa kuanzishwa chama kipya cha siasa chenye muelekeo huu. Na pendekezo la jina LA chama hicho ni BBP - BUILDING BRIDGE PARTY; CHAMA JUMUISHI
 
Tanzania tunahitaji kuitoa CCM, hatuhitaji BBI
LAKINI CCM ikijisahihisha na kuitisha mkutano wa maridhiano na kuutekeleza ,na kubadilisha katiba na kuleta ile ya wananchi sina shina nayo.
Mbona watakuwa wamejiongeza vizuri tuu
 
Tanzania tunahitaji kuitoa CCM, hatuhitaji BBI

Lengo letu kama wananchi ni kuona maisha yanaboreka kuanzia Upatikanaji na Ubora wa huduma za Afya, Elimu, Maji na Miundombinu, Na pia uhuru na Umoja, Haki, usawa na Ustawi wa Jamii,
Mengine tutayafanya wenyewe.
Whoever comes into power akifanya hayo basi ni Sawa,
Hatuwezi kuwa na Lengo la kuitoa ccm Madarakani, that’s ridiculous.
 
Umesema kweli, ila nadhani hujanisoma vizuri. Chanzo cha BBI ni handshake ya watawala wawili tu Raila na Uhuru. Handshake, yaani kupeana mikono au kuungana haikushuka chini, yaani Wakenya wote waanze kuungana baina ya makabila huku wakipeana mikono ya heri, umoja na upendo miongoni mwao.

Kinachoshushwa chini sasa hivi, si handshakes wala mpango wa kuwaunganisha Wakenya kama inavyoitwa BBI. Ukiisoma BBI yote imejaa namna ya wanasiasa watawala watakavyogawana madaraka au vyeo. Soma vizuri hiyo BBI utashangaa! Kalamu1,
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Moja ya vijana hazina muhimu ni ndugu yangu G. Malisa. Asante kwa kuibua mjadala huu muhimu wakati muhimu. Kwenye hili la BBI binafsi limezidi kunipa mtazamo tofauti kwenye mambo tunayoona ni kipaumbele ili tufanikiwe. Wenzetu Kenya walipoanza mchakato wa Katiba mpya hadi kuipata tuliona kama wamepata mwarobaini halisi wa matatizo yao ikiwemo swala la tume huru ya uchaguzi.

Huu ujio wa BBI ambao nao wengine wanaushangilia ingawa hata mimi naona umejaa neema lakini utakuwa muarubaini wa matatizo halisi ya Wakenya? Sio matakwa ya wakati ya wanasiasa? Mara nyingi ajenda za wanasiasa zimegeuzwa kuwa agenda za wananchi ndio maana mara nyingi baada ya kupitishwa hamuoni mabadiliko ya msingi mliyoahidiwa.

Ushauri wangu kwetu Watanzania, Lazima tutambue kwa kinabaubanga nini Taifa linahitaji kwa miaka 50 ijayo kutokea uhalisia uliopo? Nini chanzo cha matatizo yetu toka uhuru hadi sasa na suluhisho lake. Kama tuna mifumo ya kifisadi, hata ikiundwa serikali ya mseto ufisadi utakuwa pale pale, Hata tukiwa na tume huru ya uchaguzi (tume huru inahitaji kutafsiriwa vyema) na kutoa nafasi kwa chama chenye uwezo kushinda bado si mwarobaini wa ufisadi au fimbo ya kuleta maendeleo.

Siamini kwenye hizi tume na madaraka yake, mabadiliko ya Katiba n.k sababu zinajaa influence za wenye nguvu wakati huo iwe ni CCM, Chadema, CUF n.k wengine wenye nguvu ni zao la vyama hivyo hivyo na wanahama na fikra zile zile. Kama Bunge na Rais wanaweza kuridhia mchakato wa kubadili katiba utakaojumuisha wananchi wote (inaweza kutafutwa mechanism huru kukusanya maoni) na pia mchakato wa unyambulifu kabla ya mapendekezo ya hiyo Katiba kuhusisha tume ya walimu wote wa vyuo vikuu wenye ngazi ya elimu kuanzia PHD pamoja na makundi maalum ambayo yatateuliwa kwa kupendekezwa na tume hiyo wa walimu wa vyuo vikuu. Kidogo hii italeta uhuru wa kile tutacholetewa kama mapendekezo.

Wanasiasa hawakwepeki lakini kwa nchi zetu hizi bado hatujakomaa kisiasa kiwango cha wanasiasa kuamua kuweka maslahi yao na vyama vyao pembeni na kusimamia Taifa iwe ni upinzani au chama tawala. Tutafikia ukomavu huo lakini kwasasa lazima wakae kando na kuzuiwa kujihusisha au ku influence zaidi ya kushiriki kama raia wengine.
 
...I think the problems in Tanzania are peculiar to Tz just the way Kenyan ones are to Kenya and so what may seem a solution to one may not necessarily be to the other
 
Kwetu itafikia siku maafa yakitokea vinginevyo tukubali kuwa watumwa milele
 
Building Bridges Initiative (BBI) yaani Mpango wa Kujenga Madaraja au kuwaunganisha Wakenya ni mpango mzuri ila umejaa namna ya kuwaunganisha wasaka madaraka au wanasiasa wa juu na kugawana vyeo - si kuwaunganisha wananchi wote wa Kenya ngazi ya chini!

Ulianzia juu na handshake ya Raila na Uhuru, natamani ungeshuka chini na kuhamasisha handshakes nyingi miongoni mwa wananchi wa makabila tofauti: handshake ya mkikuyu na mjaluo, mkamba na mkalenjin, mluhya na mpokot, mteso na mturkana, nk.
Mkuu, mgawanyo unaanzia kwa viongozi. Viongozi ndio wanaowagawa watu. Ngojs tuanze juu, then automatic hali hiyo itashuka hadi chini. Suala la kugawana madaraka, ni wananchi ndio wanawapa hao watu madaraka, so, sioni shida yoyote.
 
Safi sana MTAZAMO kwa uchambuzi makini na mzuri
Moja ya vijana hazina muhimu ni ndugu yangu G. Malisa. Asante kwa kuibua mjadala huu muhimu wakati muhimu. Kwenye hili la BBI binafsi limezidi kunipa mtazamo tofauti kwenye mambo tunayoona ni kipaumbele ili tufanikiwe. Wenzetu Kenya walipoanza mchakato wa Katiba mpya hadi kuipata tuliona kama wamepata mwarobaini halisi wa matatizo yao ikiwemo swala la tume huru ya uchaguzi.

Huu ujio wa BBI ambao nao wengine wanaushangilia ingawa hata mimi naona umejaa neema lakini utakuwa muarubaini wa matatizo halisi ya Wakenya? Sio matakwa ya wakati ya wanasiasa? Mara nyingi ajenda za wanasiasa zimegeuzwa kuwa agenda za wananchi ndio maana mara nyingi baada ya kupitishwa hamuoni mabadiliko ya msingi mliyoahidiwa.

Ushauri wangu kwetu Watanzania, Lazima tutambue kwa kinabaubanga nini Taifa linahitaji kwa miaka 50 ijayo kutokea uhalisia uliopo? Nini chanzo cha matatizo yetu toka uhuru hadi sasa na suluhisho lake. Kama tuna mifumo ya kifisadi, hata ikiundwa serikali ya mseto ufisadi utakuwa pale pale, Hata tukiwa na tume huru ya uchaguzi (tume huru inahitaji kutafsiriwa vyema) na kutoa nafasi kwa chama chenye uwezo kushinda bado si mwarobaini wa ufisadi au fimbo ya kuleta maendeleo.

Siamini kwenye hizi tume na madaraka yake, mabadiliko ya Katiba n.k sababu zinajaa influence za wenye nguvu wakati huo iwe ni CCM, Chadema, CUF n.k wengine wenye nguvu ni zao la vyama hivyo hivyo na wanahama na fikra zile zile. Kama Bunge na Rais wanaweza kuridhia mchakato wa kubadili katiba utakaojumuisha wananchi wote (inaweza kutafutwa mechanism huru kukusanya maoni) na pia mchakato wa unyambulifu kabla ya mapendekezo ya hiyo Katiba kuhusisha tume ya walimu wote wa vyuo vikuu wenye ngazi ya elimu kuanzia PHD pamoja na makundi maalum ambayo yatateuliwa kwa kupendekezwa na tume hiyo wa walimu wa vyuo vikuu. Kidogo hii italeta uhuru wa kile tutacholetewa kama mapendekezo.

Wanasiasa hawakwepeki lakini kwa nchi zetu hizi bado hatujakomaa kisiasa kiwango cha wanasiasa kuamua kuweka maslahi yao na vyama vyao pembeni na kusimamia Taifa iwe ni upinzani au chama tawala. Tutafikia ukomavu huo lakini kwasasa lazima wakae kando na kuzuiwa kujihusisha au ku influence zaidi ya kushiriki kama raia wengine.
 
Umesema kweli, ila nadhani hujanisoma vizuri. Chanzo cha BBI ni handshake ya watawala wawili tu Raila na Uhuru. Handshake, yaani kupeana mikono au kuungana haikushuka chini, yaani Wakenya wote waanze kuungana baina ya makabila huku wakipeana mikono ya heri, umoja na upendo miongoni mwao.

Kinachoshushwa chini sasa hivi, si handshakes wala mpango wa kuwaunganisha Wakenya kama inavyoitwa BBI. Ukiisoma BBI yote imejaa namna ya wanasiasa watawala watakavyogawana madaraka au vyeo. Soma vizuri hiyo BBI utashangaa! Kalamu1,
Lakini si hiyo 'handshake' sasa inawapa nafasi wananchi nao wapeane 'handshake' yao kama wanataka?

Ni fursa ambayo wananchi wameipata. Wakitaka kusema wao wanataka 'handshake' ya kwelikweli na sio mzaha walioufanya Uhuru Kenyatta na Oginga Odinga, si fursa ya kufanya hivyo sasa wanayo?

Ni lazima pawe na mahali pa kuanzia kuleta mabadiliko wanayoyataka. "Handshake" wakitaka kuitumia kufanya hivyo ni fursa nzuri kwao.

Mabadiliko hayawezi kuota tu kama uyoga bila ya kuwepo na maandalizi.
 
Asante mleta mada, japo sijakaa niisome vizuri BBI, lakini kwa jinsi ulivyoichambua, kama haya umeyatabainisha ni ya kweli, aisei nitaiunga BBI kwa mikono na miguu yangu yote, ama kwa kweli itakua nzuri sana na kuboresha katiba yetu zaidi ya hapo ilipo.
Lakin lazima nipitie neno kwa neno kuhakiki hawajachomekea humo mambo ya kuturudisha nyuma kama nchi.
 
Duh, sina cha kukuelezea zaidi ili uelewe. Sikujua kuwa kuna ugumu kiasi hicho katika kitofautisha BBI na handshake! Ila wakati wote naheshimu sana mitazamo tofauti ya watu hata kama natofautiana nao
Lakini si hiyo 'handshake' sasa inawapa nafasi wananchi nao wapeane 'handshake' yao kama wanataka?

Ni fursa ambayo wananchi wameipata. Wakitaka kusema wao wanataka 'handshake' ya kwelikweli na sio mzaha walioufanya Uhuru Kenyatta na Oginga Odinga, si fursa ya kufanya hivyo sasa wanayo?

Ni lazima pawe na mahali pa kuanzia kuleta mabadiliko wanayoyataka. "Handshake" wakitaka kuitumia kufanya hivyo ni fursa nzuri kwao.

Mabadiliko hayawezi kuota tu kama uyoga bila ya kuwepo na maandalizi.
 
Oginga Odinga alishafariki siku nyingi! Aliyepo anaitwa Raila Amolo Odinga
Duh, sina cha kukuelezea zaidi ili uelewe. Sikujua kuwa kuna ugumu kiasi hicho katika kitofautisha BBI na handshake! Ila wakati wote naheshimu sana mitazamo tofauti ya watu hata kama natofautiana nao
 
Duh, sina cha kukuelezea zaidi ili uelewe. Sikujua kuwa kuna ugumu kiasi hicho katika kitofautisha BBI na handshake! Ila wakati wote naheshimu sana mitazamo tofauti ya watu hata kama natofautiana nao
Sasa unazidi kuchanganya. Nini tofauti ya "Handshake na BBI".
BBI sio matokeo ya handshake?

Unapoona kwamba wewe unao uelewa zaidi ya wengine, na huelezi uelewa huo, hapo utakuwa unajidanganya mwenewe.

Eleza 'Handshake' ni nini, na BBI ni nini na tofauti zake ni nini.
Ukifanya hivyo nitaheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani nayo.

Nieleze kinagaubaga, ni nini nilichoeleza mimi unachodhani "sielewi" swala zima la "Handshake" na "BBI". Usitake tu kuninyamazisha kwa ulalamishi.
 
Nakuachia unachoelewa wewe na ni haki yako!

Back
Top Bottom