KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kwanza kuwaza tu kuanzisha kitu kama hicho sijui utaanzia wapi wakati upande mmoja ukijiona una nguvu zote na mabunduki yote ya kuwanyamazisha wa upande wa pili.Je na Tanzania nasi tunahitaji BBI?
Kumbuka chimbuko lake..., ni baada ya uchaguzi mkuu wenye utata sana ambao hadi mahakama kwa mara ya kwanza Afrika, wakafuta ushindi wa aliyetangazwa kuwa ameshinda.
Hata baada ya uchaguzi kurudiwa na wapinzani (Odinga) kuugomea uchaguzi wa marudio, hali haikuwanzuri.
Uhuru Kenyatta akaapishwa kuwa Rais; lakini Odinga naye kang'ang'ana na kuapishwa kama Rais wa wananchi (People's President).
Sasa jiulize mwenyewe, ingekuwa hapa kwetu, Odinga kweli asingekuwa mahali pasipofaa kwa sasa au futi sita chini? Jiulize hilo bila unafiki, hakuna atakayejua ulichojibu.