Gentleman,Habari za wakati huu;
Nachokoza mjadala kidogo ambao naamini kabisa ndio mjadala unaoendelea kwa sasa hapa nchini kwetu.
Mara nyingi nimekuwa nikisikia tuhuma kwamba Chama Tawala CCM kimeungana na serikali sana na hivyo kinaitwa chama dola.Katika siasa tunapozungumzia Chama Dola tunazungumzia chama cha siasa katika nchi ambacho ni Mamlaka ya Juu kabisa katika NCHI yaana-PARTY SUpremacy.Katika mfumo huu chama cha siasa kinakuwa ndicho chenye maamuzi ya mwisho kabisa katika mustakabali na uelekea owa nchi na kwamba maamuzi ya chama ndio maamuzi ya nchi na uongozi wa chama ndio uongozi wa nchi.
Katika mfumo ambapo DOLA ndio ina mamlaka ya mwisho yaani STATE Supremacy chama kinakuwa tu ni kama usafiri wa kumuingiza mtu kwenye DOLA akishaingia chama hakina uwezo wa kumfanya chochote kwa sabab sasa anakuwa ni sehemu ya DOLA na dola haiwezi kufanywa chochote kile na chama.
Kwa muktadha huu ina maana kwamba DOLA hata ikikosea Chama hakiwezi fanya jambo lolote lile.Ninapozungumzia DOLA ninazungumzia Mahakama,Bunge na Serikali.
Nimeona niliweke hili sawa ili tunapojadiliana basi tuelewe tunajadiliana nini.
Kwa upande wa TANZANIA tangu enzi za Nyerere kulikuwa na PARTY SUPREMACY kwamba chama ndio kilikuwa na mamlaka ya mwisho ila sasa ili kukwepa mivutano CCM ililiamua kwamba RAIS wa nchi ni lazima awe mwenyekiti wa Chama ili kuepuka MVURUGANO unaotokana na tofauti za kisiasa.Uamuzi huu ulifanyika kwa sababu hatukataka kukubali mfumo wa state supremacy kwa sababu ya uchanga wa demokrasia yetu na mifumo yetu.
Vilipokuja vyama vingi,Mfumo wa Party Supremacy uliendelea,Ndio maana kwa mujibu wa sheria,Mbunge lazima awe na chama na akiondolewa chamani basi na ubunge unakoma vivyo hivyo kwa RAIS n.k.
Sasa leo hii ningependa tujadiliana kwa utulivu na kwa HOJA Je sisi kama Tanzania Tunataka tuwe na mfumo ambao STATE Ndio Supreme Authority?Je kama tukifanya hivyo tutakuwa n hali njema?Au e tubaki na mfumo uliopo Je huu mfumo unatufaa?Je tuna mfumo mbadla ambao tunaweza utumia ambao unaweza kuwa na maslahi zaidi?
Tunaweza tafuta mifano kutoka nchi mbalimbali ili tuone uelekeo wa nchi yetu.
Labda nikupe mfano wa mfumo wa Marekani.Katika mfumo huu Serikali ni Supreme.Chama ni Ngazi tu kwa ajili ya kupata uongozi.Ukishapata uongozi kazi ya chama imeisha.Baada ya Hapo ni mambo ya kuendesha nchi ndio yanabaki.Ukienda China Chama ndio kinaamua kila kitu.Chama kina maamuzi ya mwisho kabisa katika uelekeo wa nchi.Gentleman,
kwenye mfumo wa vyama vingi unatenganishaje chama tawala na dola vitu ambavyo vyote ni mali ya umma?
kwasababu,
dhamira, malengo na misingi ya kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa ni kushindanisha agenda, mipango na hoja za kisiasa, kijamii na kiuchumi, ili hatimae atakae shinda uchaguzi kwa kura nyingi, apewe dhamana ya umma kwa mujibu wa sheria, ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi wote.
hii ikimaamisha,
chama chochote cha siasa kitakachoshinda uchaguzi kwa mujibu wa katiba, kitakabidhiwa dhamana ya umma ya kukamata dola, kuunda serikali na kuongoza nchi kwa niaba ya wananchi wote.
Na karibu vyama vyote vya siasa hulenga hayo ukiachilia mbali vyama vichache vya mchongo ambavyo ni vitega uchumi vya watu.
Ni muujiza upi utatumika kutenganisha upacha huo wa chama tawala na dola? Kwasababu dola ndio nyenzo kuu ya chama chochote kile tawala ya kuongoza nchi na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama husika inatekelezwa kadiri ya vipaumbele vya wananchi waliokipa dhamana ya uongozi ya chama hicho.
Dola ni mali ya umma, na vyama vyote vya siasa pia ni mali ya umma. Hakuna namna ya kutenganisha upacha huo wa kihistoria ulimwenguni kisiasa 🐒
Tunajadiliana.Nidhamu inaweza simamiwa kwa mifumo ya kisheria na kikatiba ya nchi bila vikao vya chama.Nchi yetu bado haina taasisi imara za kusimamia state supremacy. Tukisema chama kisiwe na kauli, tutatengeneza madikteta serikalini ambao hakuna wa kuwahoji.
Chama angalau kina vikao vya ndani vya nidhamu, lakini serikali ikiwa na absolute power, nani atamfunga paka kengele?
Nani anayesimamia hiyo mifumo ya kisheria? Si ni viongozi wale wale waliowekwa madarakani na chama?Tunajadiliana.Nidhamu inaweza simamiwa kwa mifumo ya kisheria na kikatiba ya nchi bila vikao vya chama.
nadhani uko sambamba kabisa na maana ya maelezo yangu.Labda nikupe mfano wa mfumo wa Marekani.Katika mfumo huu Serikali ni Supreme.Chama ni Ngazi tu kwa ajili ya kupata uongozi.Ukishapata uongozi kazi ya chama imeisha.Baada ya Hapo ni mambo ya kuendesha nchi ndio yanabaki.Ukienda China Chama ndio kinaamua kila kitu.Chama kina maamuzi ya mwisho kabisa katika uelekeo wa nchi.
Nchi Iwe na serikali 5, maraisi wa 5, itakayowakilishwa na Mfalme 1.Habari za wakati huu;
Nachokoza mjadala kidogo ambao naamini kabisa ndio mjadala unaoendelea kwa sasa hapa nchini kwetu.
Mara nyingi nimekuwa nikisikia tuhuma kwamba Chama Tawala CCM kimeungana na serikali sana na hivyo kinaitwa chama dola.Katika siasa tunapozungumzia Chama Dola tunazungumzia chama cha siasa katika nchi ambacho ni Mamlaka ya Juu kabisa katika NCHI yaana-PARTY SUpremacy.Katika mfumo huu chama cha siasa kinakuwa ndicho chenye maamuzi ya mwisho kabisa katika mustakabali na uelekea owa nchi na kwamba maamuzi ya chama ndio maamuzi ya nchi na uongozi wa chama ndio uongozi wa nchi.
Katika mfumo ambapo DOLA ndio ina mamlaka ya mwisho yaani STATE Supremacy chama kinakuwa tu ni kama usafiri wa kumuingiza mtu kwenye DOLA akishaingia chama hakina uwezo wa kumfanya chochote kwa sabab sasa anakuwa ni sehemu ya DOLA na dola haiwezi kufanywa chochote kile na chama.
Kwa muktadha huu ina maana kwamba DOLA hata ikikosea Chama hakiwezi fanya jambo lolote lile.Ninapozungumzia DOLA ninazungumzia Mahakama,Bunge na Serikali.
Nimeona niliweke hili sawa ili tunapojadiliana basi tuelewe tunajadiliana nini.
Kwa upande wa TANZANIA tangu enzi za Nyerere kulikuwa na PARTY SUPREMACY kwamba chama ndio kilikuwa na mamlaka ya mwisho ila sasa ili kukwepa mivutano CCM ililiamua kwamba RAIS wa nchi ni lazima awe mwenyekiti wa Chama ili kuepuka MVURUGANO unaotokana na tofauti za kisiasa.Uamuzi huu ulifanyika kwa sababu hatukataka kukubali mfumo wa state supremacy kwa sababu ya uchanga wa demokrasia yetu na mifumo yetu.
Vilipokuja vyama vingi,Mfumo wa Party Supremacy uliendelea,Ndio maana kwa mujibu wa sheria,Mbunge lazima awe na chama na akiondolewa chamani basi na ubunge unakoma vivyo hivyo kwa RAIS n.k.
Sasa leo hii ningependa tujadiliana kwa utulivu na kwa HOJA Je sisi kama Tanzania Tunataka tuwe na mfumo ambao STATE Ndio Supreme Authority?Je kama tukifanya hivyo tutakuwa n hali njema?Au e tubaki na mfumo uliopo Je huu mfumo unatufaa?Je tuna mfumo mbadla ambao tunaweza utumia ambao unaweza kuwa na maslahi zaidi?
Tunaweza tafuta mifano kutoka nchi mbalimbali ili tuone uelekeo wa nchi yetu.
Baada ya Kupata uongozi kati ya Party na State ni upande upi uwe Supreme?Maana wakati wa uchaguzi hakuna shida yoyote ila baada ya uchaguzi ndipo shida inaanzanadhani uko sambamba kabisa na maana ya maelezo yangu.
China ni kesi tofauti kabisa.
ndivyo demokrasia ya vyama vingi sehemu kubwa duniani huwa.
dola iko pale tayari na ni huru kusubiri chama cha siasa chochote kinachoshinda uchaguzi ili kitumie hiyo dola kuongoza nchi. Ukiondoka, unaondoka na chama chako, unaiacha dola na wengine waliopewa dhamana ya umma nao kuitumia kwasababu ni mali ya umma wa wote.
Na ndio maana kipindi cha kutafuta uongozi,
yaani kampeni, utakuta mngombea wa democratic anailaumu republican, na mngombea wa republican anailaumu democrats kwa matumizi holela ya dola. Vivyo hivyo Tanzania na maeneo mengine yenye mfumo wa kidemokrasia 🐒
Asante, lakini nakuomba usome post iliyojuu ya post yako hii kipo kitu ambacho tanzania inapaswa kukipata hili kutatua matatizo yake.Kwa mujibu wa katiba, Tanzania ni nchi inayofuata demokrasia ya vyama vingi.
Viongozi wa serikali huchaguliwa kupitia kwenye vyama vyao ili waongoze dola.
Watumishi wa Uma wakiwemo wale wa vyombo vya dola hawatakiwi kuonesha ushabiki au ufuasi wa vyama vya siasa.
Changamoto kubwa tuliyo nayo ni ujinga, fikra duni za kitumwa ambapo watumishi hao hujiingiza moja kwa moja kwenye siasa na hivyo kuingiza taifa kwenye misuguano isiyo ya lazima.
Ujinga huo huo hufanya viongozi wa kisiasa (rais na serikali yake) kupata misukosuko isiyokuwa ya lazima.
Bila watumishi wa Uma wenye akili huru, katiba na sheria hazina walinzi na hivyo kusababisha vurugu.
Kabla sijaenda kuisoma Katiba yako naomba tutafakari kwa pamoja;Kitu pekee tanzania inaitaji ni katiba yenye mamlaka ya usimamizi wa misingi ya kitaifa, na ndio maana pendekezo langu la katiba lililopo kwenye www.katibampya.com linatoa jibu la swali lako.
Kwanza kabisa rasimu hiyo ina muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania.
Muundo huu unahakikisha uwazi, uwajibikaji na kutoingiliwa kwa mamlaka fulan kinyume na katiba na sheria za nchi.
Kwenye orodha hiyo limeongezeka baraza ambalo kwenye rasimu limetamkwa kuanzia ibara ya 98 mbaka 116, unaweza kwenda kulisoma na kulielewa kiundani.
Pili, tunapaswa kuwa na mamlaka ya Uwajibikaji wa lazima. Katika rasimu hiyo hiyo yapo mamlaka ya mwisho kabisa ya ulinzi wa katiba ambayo hata baraza lenyewe likitekwa au kudhoofushwa katika kulinda katiba basi Mamlaka hiyo uingia kwa mwisho kabisa, nayo ni Mamlaka ya kimapinduzi yaliyotamkwa katika ibara ya 255 mbaka 260 ya tasimu hiyo ya katiba.
Tembele tovuti www.katibampya.com hili ukajisomee mwenyewe, kisha rudi hapa kwa kuiunga mkono, kuihoji au kuikosoa kwa hoja zillizo wazi kabisa bila matusi wala kejeri.
Ndio, Rasimu ya katiba kwenye Tovuti tajwa imejibu swali hili kwa kuweka muhimili wa nne wenye jukumu la kusimamia misingi yote ya kitaifa, yaani misingi kama bunge kutoingiliwa, misingi ya demokrasia ya kisiasa kutodhoofishwa, Tunu za taifa, Dira ya taifa ya maendeleo endelevu na ustawi wa jamii n.kKabla sijaenda kuisoma Katiba yako naomba tutafakari kwa pamoja;
Kwa swali lililoulizwa Je Tunataka Chama Dola au Tunataka Dola Huru? Katiba yako inajibu swali hilo?
Ndio, Katiba hiyo imetamka wazi kabisa mamlaka ya kila muhimili na mipaka yake, pia swali ulilosema People's power ndio Tena yametamkwa katika ibara ya 12 ya katiba na kuwekwa ngubu yake katika ibara 74 kwamba si tu yamewekwa kama kauli ya rohoni bali kama mamlaka inayoweza kutekelezeka, pia ibara ya 286(2) imeweka ufafanuzi wa jumla wa katiba yote ambapo mamlaka ya Wananvhi yamewekwa juu kabisa ya mamlaka zote, mihimili yote na yanatekelezwa kutia Haki ya sauti ya taifa ( ibara ya 74) naomba uisome kidogo hili uelewe hiyo haki ya sauti ya taifa ni nini..Pili Je Mihimili yako hiyo minne uliyopendekeza imezingatia Checks and Balance?Je katiba yako imezingatia Mamlaka ya Umma(People's Power) na namna hayo mamlaka yatakavyotumika?
Kwenye Rasimu ya katiba niliyoitoa au pendekezo lilounganishwa na uzi huu ni kwa sababu swali lako linajibiwa kwamba Chama dola uzalisha udiktekta dhidi ya demokrasia, na Dola huru bila mamlaka ya usimamizi wa misingi yake dola ugeuka kuwa shamba la bibi lililokosa usimamizi, hapa sasa ndipo pendekezo langu la katiba yenye mihimili minne linaingia.Ila tunapswa tukubaliane Jambo moja kwamba Hatuwezi kukwepa mjadala wa Party Supremacy vs State Supremacy kwa sababu tukiweza kuamua hapo basi tunaweza amua iwapo People's Power itumike wapi.Je itumike katika kuendesha Chama ama itumike katika kuendesha State?
Exactly, Naomba nikujibu kwa ujasiri wa kisomi na kitaaluma kwamba Baraza la usimamizi wa Taifa ndio mamlaka iliyopewa dhamana ya kusimamia misingi ya kitaifa ambapo maadili ya taifa ni sehemu ya usimamizi wake.Ni muhimu sana kwa sababu nionavyo mimi,hatuwezi kuwa taifa ambalo kila mtu anafanya anavyotaka lazima tuwe na utaratibu na utaratibu huo lazima uwe wazi na unaoeleweka kwa mfano kama tukizingatia Party Supremacy inamaana kwamba Mchakato wowote ule lazima uanzie katika Ngazi ya Chama kabla haujafika kwenye ngazi za maamuzi ya serikali.
Kwanza kabisa naomba nikulekebishe neno dogo, Pale uliposema vyombo vya kiserikali Umechanganya Mihimili mingine kwamba hipo chini ya serikali na ulichotakiwa ni kutumia neno Dola. Kwenye rasimu hiyo ya katiba Kuna kanuni iliyowekwa inayoitwa "Kanuni ya ulinganigu wa nguvu za kikatiba" itakayowekwa ndani ya sheria ya usimamizi wa taifa kazi ya kanuni hiyo ni kupima hali nguvu ya mamlaka A kuwa juu ya mamlaka B kwa wakati C kisha mamlaka B kuwa juu ya mamlaka A kwa wakati D.Na iwapo tukiamua kwamba State Supremacy Ndio muhimu basi michakato yote lazima ianzie na kumalizikia kwenye Vyomba vya kiserikali ambavyo ni Bunge,Mahakama na Serikali Kuu.Kama ikiwa Hivyo ni lazima tuwe na Mahakama yenye Nguvu Kubwa,Bunge lenye Nguvu Kubwa na Serikali kuu Yenye Nguvu Kubwa. Sasa ili tutengeneze Hivi Vyombo Vikiwa na Nguvu Kubwa lazima tujiulize Central Power Atakuwa nayo nani? Je ni hili Baraza la Usimamizi wa Nchi?Kama ni hilo Je Baraza hili liundweje?Je liundwe na viongozi wa vyama vyote vya siasa?Kama ni Ndio Je Vyama Visajiliweje?Je Visajiliwe na Kusimamiwa na Sekretariat ya Hilo Baraza?Je Uchaguzi uendeshwe na nani?Je uendeshwe na Hilo Baraza la Usimamizi?
Kwenye nyoongeza ya katiba, yaani mwisho kabisa wa katiba na njee ya katiba yenyewe nimeweka Taratibu mbali mbali na kueleza ukweli wa gharama za uendeahaji lakini kwa ufupi kabisa baraza litaitaji 0.3% ya bajeti kuendeshwa lakini litaokoa 0.8% ya bajeti au zaidi iliyokuwa inapotea kwenye ubadhirìu, ufisadi na Wizi wa viongozi wa umma. Hili nalisema kwa ujasiri mkubwa sana kwamba ndio Muundo wa baraza unaweza kudhibiti Ufisadi na wizi wa mali ya umma kwa kiwango kikubwa.Je Gharama za uendeshaji wa hilo Baraza zitoke wpi?
Exactly, Marcostilone nakumbuka kwenye uzi wangu mmoja tuliongea kuhusu muhimili wa nne wa kitaifa wenye jukumu la usimamizi wa misingi ya kitaifa na leo umeingia kwenye pendekezo langu la katiba moja kwa moja bila kujua kuwa unaingia humo, kwanza kabisa nikuombe usome ibara ya 98 mbaka 116 inayoeleza muundo, majukumu, mipaka na mengineyo kuhusu baraza la usimamizi wa taifa.Nchi yetu bado haina taasisi imara za kusimamia state supremacy. Tukisema chama kisiwe na kauli, tutatengeneza madikteta serikalini ambao hakuna wa kuwahoji.
Chama angalau kina vikao vya ndani vya nidhamu, lakini serikali ikiwa na absolute power, nani atamfunga paka kengele?
naomba nijibu Swali lako.Ni muujiza upi utatumika kutenganisha upacha huo wa chama tawala na dola? Kwasababu dola ndio nyenzo kuu ya chama chochote kile tawala ya kuongoza nchi na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama husika inatekelezwa kadiri ya vipaumbele vya wananchi waliokipa dhamana ya uongozi ya chama hicho.
Dola ni mali ya umma, na vyama vyote vya siasa pia ni mali ya umma. Hakuna namna ya kutenganisha upacha huo wa kihistoria ulimwenguni kisiasa 🐒
dhamira, malengo na misingi ya kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa ni kushindanisha agenda, mipango na hoja za kisiasa, kijamii na kiuchumi, ili hatimae atakae shinda uchaguzi kwa kura nyingi, apewe dhamana ya umma kwa mujibu wa sheria, ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi wote.
Baraza halina kiongozi wa kisiasa hata mmoja, wote wanatokana na sifa, weledi na masharti ya kikatiba.Nani anayesimamia hiyo mifumo ya kisheria? Si ni viongozi wale wale waliowekwa madarakani na chama?
Conflict of interest itaua hiyo nidhamu mapema mno.
Gharama za uendeshaji dola.....?Nchi Iwe na serikali 5, maraisi wa 5, itakayowakilishwa na Mfalme 1.