PUTIN: AFRIKA HAITOKAA IWE HURU
Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.
Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."
Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?
Quote