Uchaguzi 2020 Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...

Uchaguzi 2020 Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kipenga cha kuanza kwa kampeni za Uchanguzi Mkuu ujao kimepulizwa leo na fungua dimba amekuwa Chadema.
Nimeangalia kidogo kupitia live ya TBC, kiukweli nilichoshuhudia, ndicho kimenipelekea mimi kuanzisha huu uzi ambao ni swali.

Je, Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini, wenye the ability, the capacity and the capabilities za kuleta upinzani wa kweli wenye uwezo wa kuing'oa CCM madarakani?, au upinzani wetu hapa Tanzania ni bado sana?.

Nimeuliza hivi kufuatia nilichokishuhudia leo, kwenye uzinduzi kampeni za Chadema, pale uwanja wa Mbagala Zakhem, kiukweli ...
kwa vile na mimi siku hizi ni kada, kuna vitu naomba nisiviseme nikaonekana ni kupiga siasa!.

Kwanza natoa hongera kwa Television ya Taifa, TBC kutangaza live uzinduzi huo wa kampeni za Chadema!. Japo matangazo yenyewe ni kwa kukata kata, lakini something is better than nothing!.

Je, kitendo alichofanya M/Kiti Mbowe, kuwafukuza live TBC, huku wakiwa live ni sawa?!.

Nimetoa pongezi na hongera kwa TBC kutangaza live matangazo ya uzinduzi kampeni za Chadema!, ile tuu TBC kukubali kutangaza live uzinduzi wa Chadema huku unajua kabisa watu wa type yao ni wasemji wa namna gani!, huku Mbowe, huku Lissu, huku Lema, na bado TBC ikakubali kuwapa live, hatua hii pekee, inastahili pongezi.

Lakini Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Mbowe aliposimama kuzungumza, aliwafukuza live TBC huku wakiwa live hewani!. Kitendo alichofanya Mwenyekiti Mbowe, cha kuwafukuza TBC, sio sawa, it is not right, hajaitendea haki TBC, hajaitendea haki media, hajaitendea haki Chadema, hajawatendea haki Watanzania kukosa kusikia sera za Chadema.

Hasira za Mkizi kwenye siasa, kiukweli kabisa hazisaidii kitu!.

Wakati Mhe Mbowe anasema TBC wamekata matangazo, TBC ilikuwa iko live wakati Mhe. Mbowe akitangaza kuwafukuza na kuwasingizia kuwa TBC wamekata matangazo, ilikuwa sii kweli kwasababu TBC walikuwa live kabisa na hawajakata matangazo!, kitendo cha Mwenyekiti Mbowe kuwafukuza TBC na kuwaambia TBC waondoke, sio kitendo cha kistaarabu, hakikubaliki, vyama vya habari tusilinyamazie hili, na mkinyamaza nitawashangaa!, maana kwa wafuasi wa Chadema ninaowafahamu mimi, kitendo cha TBC kutoka salama mahali pale baada ya amri batili ya Mhe. Mbowe ni cha kushukuru Mungu, maana wangeweza kufanya chochote. Media ni kama Red Cross vitani, hawapasi kufukuzwa kivile!. Mhe. Mbowe akemewe, aombe radhi, Chadema ikemewe, ifunzwe kauli za kutoa kwenye live Broadcasting, na TBC ipongezwe kwa kujaribu, ila pia TBC ifunzwe political tolerance, na managing political diversity na kuepuka double standards kwa kuipendelea CCM!, kesho shuhudieni ufunguzi wa kampeni za CCM, muone kama matangazo ya CCM yatakatwa katwa kama ya Chadema, wakati kiukweli kuna wakati hata viongozi wa CCM wanasema vitu ambayo sio!.

Hili la viongozi kusema sema, niliwahi kushauri
Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.

Kitu ambacho ni kweli nilikiona ni TBC kuwa na kibarua kigumu cha kufanya censorship matamshi yoyote hatarishi na ya kichochezi. Sii wengi wanajua kuwa kwenye matangazo ya live, mtu ambaye yuko responsible na kinachorushwa hewani, sio yule msemaji, bali ni mrusha matangazo, yaani TBC, hivyo mwanasiasa anapoibuka na kutoa kauli za kiajabu ajabu, ambazo ni za uchochezi au kuhatarisha amani, utulivu na mshikamano wetu, then TBC wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kufanya censorship, ndio maana matangazo yalikuwa yanakatwa katwa na kurudishwa studio.

NB. Ikitokea Chadema ikashindwa kwenye uchaguzi, isilalamike kuwa CCM imebebwa na TBC ndio maana ikashinda, Chadema wamepewa fursa ya kuitumia TBC, Chadema wenyewe ndio wamekataa na kuwafukuza TBC, hivyo sasa wanategemea nini?.

Hizi ni Hasira za Mkizi!

Hata hivyo, TBC tunapoelekea kwenye uchaguzi wa vyama vingi, TBC inatakiwa iji redifine its role kwenye uchaguzi, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo inagharimiwa na serikali sio kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, TBC na RTD ni Public Broadcasting Stations, ambayo ni TV ya umma na Redio ya umma ambayo is paid by taxpayers money kutoka serikalini lakini inatakiwa kuwatumikia Watanzania wote , wa vyama vyote kwa haki sawa na kwa usawa bila upendeleo unaoonekana kwa CCM kupendelewa zaidi!.

TBC inabidi iwatumikie watu wote ikiwemo serikali na sio kuitumikia serikali as if kwasababu ni malí yake, TBC sio mali ya serikali ni mali ya umma kwa udhamini wa serikali kama ilivyo BBC!. Vyombo vya habari vya serikali ni gazeti la Daily News, Habari Leo, Idara ya Habari Maelezo, na The Government Gazzette.

Kwa hali ya siasa ilivyo sasa, TBC is as if inaipendelea sana serikali na CCM kwa kurusha matukio ya serikali au ya CCM bila any censorship lakini kwenye mikutano ya upinzani kwa kufanya censorship ya kiana kwa kurejea studio.

Viongozi wa TBC na viongozi serikali wanapaswa kuiwezesha TBC kwa rasilimali watu na rasilimali fedha kuweza kuwatumikia wananchi wote Watanzania kikamilifu na hata kuisaidia serikali kwa kuweka vipindi critical kwa serikali ambavyo vitafanya a constructive criticism kwa lengo la kujenga na sio kubomoa na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi CCM na waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu tuu au ni mali yenu. TBC ni TV yetu sisi sote Watanzania, tuna wajibu wa kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manufaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania TBC ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli!. TBC ifungue zaidi milango yake ya vipindi kwa kuruhusu vipindi kutoka outside kwa independent producers na production houses ili kupata diversity na good mix from the society.

Wito kwa wapinzani, mnapapata fursa za kuwa coved live, mna wajibu wa kuwa wastaarabu kwa kutangaza sera, na kutumia lugha za staha na sio lugha za kuudhi.

Ndio maana nimeuliza, kama upinzani wenyewe ndio huu tuliouona kwa Chadema, halafu hawa ndio watu wanaotaka Watanzania tuwape Ikulu yetu watutawale, kama hata kujitawala wenyewe tuu ni issue, hili la kuwapa nchi, itakuwaje?

Namalizia kwa lile swali la msingi la bandiko hili, jee Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini, wenye the ability, the capacity and the capabilities za kuleta upinzani wa kweli wenye uwezo wa kuing'oa CCM madarakani na wenyewe kutawala nchi yetu?, au upinzani wetu hapa Tanzania kiukweli kabisa ni bado sana?

Paskali
 
Amefafanua kwamba hatazindua sera kwanza ilihali wagombea 53 na 47 kwa upande wa Zanzibar wameenguliwa
Kwa aliyochofanya ni kutoa mwelekeo wa chama

Kuhusu TBC ni kwamba aliposimama Mbowe wakadivert akawa hasikiki bali watangazaji wanaongea sasa kulikuwa na haja gani ya kurusha live kama ninyi watangazaji mnaongea badala ya watu kumsikiliza Mbowe tbc inataka watu kusikiliza watangazaji

Kama TBC wanaona ni maneno ya kichochezi wasingeenda je kuna haja gani ya kwenda? ndio maana akawatimua

Je anayeona ni maneno ya uchochezi ni nani?

Pascal Mayalla endelea kufukuzia uteuzi upinzani imara unauhitaji wa nini wakati wewe ni ccm?
 
Wakwende huko. Wanatoa matangazo na kukatakata ndio wamesaidia Chadema? Chadema ina nguvu ya umma. Sisi wananchi ndio tunamuweka Tundu Lissu madarakani -kwenye kiti cha Urais.

Hao CCM pamoja na wewe mbaki na TBC yenu. Tumechoka manyanyaso, hatuvumilii tena ujinga ujinga.

#TunduLissu2020 #NiYeye #SasaBasi
 
Hivi paskali hii censorship huwa haimuhusu rais anapokuwa anaongea enh!

Tbc kwanza engo ya camera ilikuwa ni moja tuu picha haziluchanganywa. Pia walikuwa wanakatisha matangazo na kuongea udaku. Tufike mahali tukubali mazingira ya kisiasa sio rafiki kwa vyama upinzani.

Pia muda wote chadema tulitegemea SMN. Leo tbc ni ama waliambiwa warushe live ili watu / mtu fulani ayapate matangazo bila kutumia bando. Ama tbc walitaka kumake hela kwa kupata viewers wengi
 
Vipi kwa ile hotuba ya Lissu leo hamjaandaa RB mpaka muda huu kweli? Maana nadhani mpaka leo iishe kutakuwa kumetolewa matamko kila idara yenye mamlaka leo. Ila nikuulize kitu, Hivi Walichofanya TBC ulikiafiki na wewe?
 
Kwa mara ya kwa Pasco nakuita wewe ni mpumbavu na hii njaa itakuvunjia sana heshima mjini.

Hata mjinga akinyamaza uhesabiwa hekima.
TBC walikuwa kimkakati. Na sijui kwann ccm wamahofia upinzani kiais hiki ilihali wao wana jeshi na kila kitu.

Kitendo.cha kuengua wabunge zaid ya 100 wa upinzani ninishara tosha kuwa wanataka wawe na uhakika wa quarom wakati wa kupitisha hoja zao za kionezi
 
Bandiko refu sana, umekomaa na Mbowe kuwafukuza TBC.

Lkn kwann TBC na sio wengineo?

TBC hiii hi?? Huu sio wakati wa kubembelezana na wanafiki , Wanafiki Tupa kule.

Kwamba kila spana zikipigwa ndo matangazo yanakata?

Waende huko, nahata ningekua mimi kwanza Toka awali WASINGEKUWEPO.

TBC kitu gani? Mbona watanzania wote nchi hii wamejua Lissu karudi, Kachukua Fomu, sasa ni mgombea na wamejua pasipo hata tangazo moja toka kwa TBC.. Nini sasa?
 
Umeanzisha uzi wako huu kwa kukurupuka,ungeuleta kesho baada ya chama cha wapiga spana(CCM)kuzindua kampeni zake kesho kwa kulinganisha jinsi TBCccm walivokuwa wanatangaza ufunguzi wa kampeni ya CHADEMa na hiyo yenu ya kesho.
 
Nyoki la chadema mbagala leo...
Hata wananchi wamekisusa hiki chama na msipobadilika chadema mtabakia viongozi pekee wa chadema....
B10085EF-BA7E-4CC6-8B17-6BBDF1F2163E.jpeg
 
CHADEMA wajipange vizuri zaidi maana bado muda wa kampeni upo,ila nadhani kuenguliwa kwa idadi kubwa ya wagombea wao wa ubunge na udiwani kwa sababu za kutiliwa shaka zimewavuruga na kuwapa wakati mgumu.
 
Jibu ni hapana. Upinzani wa sasa ni kama mtoto wa kambo. Kutwa kulalamika na kutegemea huduma kama vile mtoto halisi wa mama. Wapinzani acha waendelee kuokota wabunge wawili watatu wa kuwapa ruzuku. Very soft. Too soft.

Pia inaonesha wanaamini sana katika harakati kuliko mipango madhubuti ya kitaasisi. I think the ruling party just won on the very beginning.
 
Back
Top Bottom