Je, Tanzania tunahitaji Gen Z?

Mmekuwa kama wajinga jana mlisema jeshi lipo barabarani hawataonekana leo mnasema ukabila 🤣🤣.
Mkuu sio lazima kila wanachofanya muige kama wao wanataka raisi atoke madarakani nyie mumshinikize huyu wenu watendaji wawajibishwe lakini pia akomeshe utekaji nyara ma mauwaji ya raiya mkaishia hapo...sio lazima kila kitu mfanye kama wao
 
Sawa
 
We sijui kama ni mtanzania kweli hata mababu zetu waliuwawa ili sisi tuwe huru kwa hyo gharama haziepukiki waambie watawala wako waendelee kutumia mabavu na kuwadharau wananchi ipo siku yao inakuja.
 
Kwani mkuu nimekosea kuelezea?
Hii dhana ya kugawa vizazi kwenye generations, ilianzia marekani, waligawanya vizazi vyao kulingana na mabadiliko ya kijamii ,kiuchumi na kisiasa kwa vipindi maalumu vya nyakati , kulingana na muonekano wa mabadiliko kwenye vizazi vyao .

Kwa dhana hii , kulinganisha na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa na kijamii kwa Tanzania bado haijakidhi vigezo vya kuwa na kizazi z generations kwa mujibu wa waasisi wa hizi generations.
 
Ok nimekuelewa
Kwa US wanasema ni late 1990's hadi 2010's lakini kwa Africa sidhani...

Tukiachana na waasisi, naona kwetu hio ndio Gen Z yetu.

we si unaelewa huku January Makamba anaitwa kijana😀, na Mo Dewji anaitwa tajiri kijana.
 
Kizazi hiki hapa Tanzania kipo, yaani "Zoomers", kwani hawa ni vijana wazaliwa wa kati ya mwaka 1995 hadi 2009.

"Generation Z (often shortened to Gen Z), colloquially known as Zoomers, is the demographic cohort succeeding Millennials and preceding Generation Alpha. Researchers and popular media use the mid-to-late 1990s as starting birth years and the early 2010s as ending birth years. Most members of Generation Z are the children of Generation X or older Millennials" - Source Wikipedia.
 

Attachments

  • IMG_20240627_165719.jpg
    48.8 KB · Views: 5
Wewe ni ignorant ila unataka kujifanya mjuaji.


1. Kwanza, Napinga suala la ukabila. Maandamano ya Kenya yamefanyika nchi nzima. Kuanzia Nairobi, Isiolo, Nyeri , Eldoret kwa Ruto, Mombasa etc. kule Eldoret kwa Ruto watu waliishusha alama ya mkokoteni wa UDA katikati ya mji, Nyeri kwa Gachagua Wakikuyu walishambulia Supermarket ya mbunge wa UDA na kufanyaaandano makubwa. Giturai 45 kwa Wakikuyu maandamano makubwa yalifanyika Hadi vijana kulimwa risasi na kufariki.

Swali linakuja Kama kwenye ngome ya Ruto na Gachagua maandamano yamefanyika sambamba na Kisumu, Mombasa na Kakamega je ukabila upo wapi hapo?.


2. Pili, Hakuna mkono wa mtu kwenye maandamano haya. Makamu wa Rais Gachagua amekiri Gen Z Wakenya hawakuwa na kiongozi ndio maana walifanikiwa azma yao ya kuingia bungeni na kuliharibu ili akili irudi Kwa wabunge wasiojitambua.

3. Tatu, naomba nikushauri, usipende kuangalia matokeo angalia chanzo Cha matokeo. Shida yako unaangalia matokeo ya maandamano ya Gen Z bila kuangalia chanzo Cha maandamano ya Gen Z. Chanzo ni wabunge kutoheshimu maoni ya wananchi na baadala yake kutaka kumfurahisha Ruto.

Siku nyingine tumia nguvu kubwa kujadili bajeti ya Tanzania.
 
Kinazungumziwa 'kizazi' mithili ya Kapelo au Kobazi za Kimasai.
Hizi shule zetu sijui huwa zinafundisha nini?
 
Jifunze hapa kaka. Haiepukiki
 
Umesema tutumie nguvu ya ballot box!? How?!... ballot box ina nguvu gani Tanzania?
Sisi watanzania wabinafsi sana.

Dawa ni kuliwasha tu kwa kina Mwigulu ndio tutaheshimiana.
 
Mtoa mada anamaanisha vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 27 wote nchini Tz haiwahitaji wauliwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…