Je, Tanzania tunahitaji Gen Z?


Anafikiri Gen Z ni kama Machawa, Machinga au yale magroup ya Vijana yaliyokuwa yana terrorize watu mitaani .... sijui wanaitwa nini vile .... Nimesahau....!! Yah Right PANYA ROAD!!
 
Ndiyo,,kwani kuna tatizo
Tatizo liko moja tu kwako, hujui kuwa hujui. Sina hakika kama utaelewa hata ninachosema hapa. Asiyejua kwamba hajui ni hasara kubwa katika dunia hii ya leo.

Gen Z utake usitake wapo Tanzania na ni wengi sana. Wapo kwa sababu tu walifyatuliwa lakini uwepo wao hauna faida kwa taifa. Hawajui wanakotoka wala wanakoelekea.

Tatizo la Gen Z wa Tanzania ni kwamba wako kama wewe, wenyewe wanamini wanajua kumbe hawajui kitu. Sasa jaribu kuwakumbusha hilo, majibu ndio hayo unayoyatoa wewe.

Kama kungekuwa na uwezekana, hawa Gen Z wa Tanzania wangefutiliwa mbali kabisa katika ramani ya Tanzania kwani wanachojua kwa hakika ni kuvuta hewa, kula, kunywa na kulala.

Hongereni sana Gen Z wa Kenya na Gen Z popote pale mlipo ulimwenguni. Nyie ndio wajenzi na walinzi wa dunia ya kesho!
 
Sawa
 
Kenyans should remind themselves what happened in Libya
 
Bandiko refu hamna content ya maana
Ccm mna laana nyie

Uwaite gen z au vinginevyo utaona inafa, ukweli ni kwambac tunahitaji vijana wazalendo, waandamanaji watakao wafurusha watawala mafisadi
 
Sabato ya Leo ni kuliombea taifa letu tusifike huko walikofika Wenzetu

Watoto wanawaongoza Wakubwa, hatari sana 🐼

Nawatakia Sabato Njema 😄
 
Wanaopeleka watu huko ni watawala kwa ajili ya faida ya matumbo yao na watoto wao. Ukiwashauri au kuwakosoa utasikia wewe ni Chadema au wewe ni CUF au utapewa chama chochote Cha upinzani. Wanaamini wasiojitambua wako CCM. Kwa mfano Mpina wameshamuweka kwenye kundi hilo kisa anahoji mambo magumu mpaka wanaongeza vipengere visivyokuwapo vya kanuni ili ahukumiwe vikao 15 angalau kelele zake zitapungua wanataka wabunge kama Abood na wengine. Wanaochangia mwaka mzima mara 2 au 3 tuwakatae! Ndiyo maana Morogoro ya mwaka 2000 mpaka leo Chanzo ni kile kile Cha maji Bwawa la Mindu bila kujali ongezeko la watu. Area six maji mara moja kwa wiki tena wakati mwingine usiku wa manane ukipishana nayo utakutana nayo wiki ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…