Je, Taoism ni uchawi? Je, unaweza kutumia Taoism kutabiri mambo ya mbeleni? Nitajaribu kukuelewesha

Je, Taoism ni uchawi? Je, unaweza kutumia Taoism kutabiri mambo ya mbeleni? Nitajaribu kukuelewesha

Hello bosses and roses.

Nimekua napokea maswali mengi kiasi kutokana na maandiko yangu kadhaa nioandika hapa siku za nyuma. Lakini maswali mengi yanajikita kwenye haya mawili, Je Taoism ni uchawi? Na je unaweza kutumia Taoism kutabiri yatakayotokea mbeleni?

Kabla ya kujibu hayo maswali labda nielezee Taoism ni nini kwa maneno ya kawaida kabisa.

Taoism ni Namna ya kuishi kwa kuendana na lengo la Nguvu kuu inayoendesha au iliotengeneza ulimwengu. Hivi ulishajiuliza kwamba force of gravity ingekua kubwa zaidi ya ilivyo basi nini kingetokea? kila kitu kwenye ulimwengu huu kingevutwa sehemu moja kama sumaku vile, na pia ushajiuliza kama gravity ingekua ndogo zaidi ya ilivyo kila kitu kingepepea infinitely?

Na ushawahi kusikia kuwa kiasi cha nishati (energy) hapa ulimwenguni kiko fixed? Ila tu nishati ile ile inajibadili badili? Sasa hizo facts nlizosema hapo na nyingine zote zinamaanisha kwamba duniani kuna NGUVU moja kuu ambayo ndio ilioweka na inayomaintain hio BALANCE.

Hio Nguvu kuu inajionesha kwa mambo mengi, na ndio maana ina majina mengi kutokana na watu tofauti. Wengine wataita Mungu, Wengine Allah, na kadhalika.

Kazi kuu ya Taoism ni kuhakikisha binadamu anaishi kutokana na matakwa ya hio Nguvu Kuu. Kwenye Taoism hio nguvu tunaiita "Tao" au "The Way" kwa kiingereza. Na hio Nguvu, haielezeki, wala haina jina. Ndo maana kwenye kitabu kikuu cha Taoism kinachoitwa Tao Te Ching,kuna aya inaaema ".....The Tao that can be named is not an eternal Tao....."

Sasa Taoism imekuwepo toka zamani saaaaana, na Taoism sio dini. Ni njia ya moja kwa moja ya kufikia hio Nguvu kuu, lakini dini ni kama Agent anaekupromise atakukutanisha na hio Nguvu kuu. Kwa sababu Taoism imekuwepo toka zamani basi imekutana na maboresho mengi ambapo watu baadhi hutumia mafundisho yake kufanyia mambo mbalimbali. Mfano, ulishasikia Tai Chi? Hio ni style ya kupigana kwa kutumia body balance na softness ili kumshinda adui yako, lakini imezaliwa na Taoism.

Kwa maana hio kuna watu walitumia mafundisho ya taoism kutengeneza factions za kichawi, hapa ninajibu swali la kwanza, je Taoism ni uchawi? Kiufupi taoism sio uchawi, ila mafundisho ya Taoism yanabeba mambo mengi sana ambapo ukiweza kutumia ukaapply kokote kule iwe kwenye Siasa, Biashara, Vita, Uchawi, nk nk... utapata matokeo unayotaka sababu Taoism inakuonesha Nguvu kuu inataka nini, na ukiweza kuji-align na hio Nguvu basi utapata chochote unachokitaka. Kuhusu swala la uchawi kwenye taoism, haina tofauti na mtaalam wa physics akatumia ujuzi wake kutengeneza Nuclear bomb.

Swali la pili kuhusu kutumia Taoism kutabiri mambo ya mbeleni. Hili mitalijibu kiufupi sana ili nisikuchanganye ndugu msomaji.

Hivi mfano wewe si unajua kwamba ukivuta mlango kwa nguvu na mlango ukiwa hujawa locked basi mlango utafunguka?

Sasa kwa mfano huo hapo juu, chukulia una manuals (mafundisho) yanayoelezea kila kitu au kila tendo na outcome yake. Sasa utashindwa nini kutabiri kitu gani kitatokea baada ya kitu fln kufanyika? Kama nilivyosema awali kwenye Taoism kuna mafundisho meengj sana, mengine hadi ukitumia unaweza tabiri kabisa moves za adui yako, hili linatumika hata kwenye Tai Chi, kwa masters wa Tai Chi, wao ukipigana nao anakua anajua next move yako ww ni ipi. Sasa jiulize kama Taoism imezaa Taaluma kama hio, kwa nn mafundisho yake yashindwe kukufanya ww kutabiri mambo yatakayotokea? Kuna mafundisho mengi sana kwenye Taoism, na kuna Sages wengi sana wameandika. Na nisikudanganye, sio kila mtu anaweza kufikia hio level ila nakwambia hapa uhusiano wa Taoism na utabiri wa mambo ya mbeleni

Mwisho kama unataka kuona nilichoandika hapa ni porojo au sio porojo, chukua muda, soma kitabu kinaitwa TAO TE CHING. Ni kitabu ambacho kiukweli kimebadili maisha yangu na namna ninavyoona vitu au situations mbalimbali. Ni ktabu ambacho nikiwa naona nimefail au nimekwama kabisa basi nakisoma na napata jibu nifanye nini. Ni kitabu kifupi sana, kiliandikwa kwa kichina miaka ya zamani lkn kuna tafsiri nyingi sana zipo mtandaoni.

Remember, the goal is to be a decent human being. Until next time, stay safe!

~ kali linux
666
 
Utapoteza muelekeo sababu vyote vimewekwa kwenye mfumo maalumu ili vitende kazi
Kama binadamu tumeweza ku overcome Nature kwa baadhi ya mambo mfano kurusha ndege 🛫, kurusha satellites, kupeleka vyombo mwezini na anga za juu zaidi kwa kuweza ku overcome force of gravity, Je huoni kwamba siku za mbeleni tutaweza mambo mengi zaidi?
 
Umefanya nini kwenye world of science
Kwa sababu unatumia nguvu ya kubisha ili ushinde na sio hoja
Sijafanya kitu.

Na hoji hiyo science inaweza kusolve vitu kwa kiwango kipi?

Maana kuna vitu vingi sana havina majibu licha ya sayansi kujaribu kutoa majibu ya muda tu.

Bado kuna maswali mengi kuliko majibu kwenye sayansi.
 
Tanzania vipimo vya akili ni vidogo
Hizo statement anazo-copy wikipedia ndo unamuona ana akili

Wewe mbona huleti sources zako za information?

Huelezi umefanya nini kwenye world of science?

Weka hapa researchs zako na tafiti zako za kisayansi tofauti na hizo za Wikipedia..
 
Habari Kiranga
Mimi sio mtalaam sana wa Quantum Physics au Quantum Mechanics ila huwa kila siku najitahidi kujifunza kwa sababu nahisi ndo kuna majibu mengi yamejificha huko kwanini wanaofanya vitu wanafanya wanayoamua kufanya!..

Kuna kitu kimoja umezungumzia kime-trigger ..
My DLPFC (Dorsolateral prefrontal cortex) brain Part na nimeona nikushurikishe kama utanipa maelezo zaidi..
Umezungumzia Swala la Photons na image preview au production..

(Nita paraphrasing ulichosema na utanirekebisha kama nitakosea kuna some information nimeziongeza kutokana na uelewa kidogo)

"Kwamba ili image iweze Kuonekana,Lazima Photons from the objects,leaves the objects na inaingia kwenye camera through lens na lens inaifocus Hiyo "Photons" through the image sensor ("Pixels"),Na ikikutana na Hizo pixels ndo hutengeneza Electrical Signal na the camera Inaprocess hiyo signal kuwa digital Image...."

Sasa nina maswali kadhaa..
  • Photons ni particles smallest kuliko hata Atom nafikiri Na hucarry Energy (Japo inategemea na wingi wake) and if so hiyo haimaanishi kwamba tunaweza kupoteza Energy kadhaa kwa kupiga Picha (Japo inaweza isiwe kwa kiwango kikubwa?
  • Kama wingi wa Photons unaweza kuwa determined na lens...So lens zenye ukubwa huweza kuchukua energy kubwa kuliko zingine?
  • And if so Nini kifanyika (Hata kama energy ni ndogo) maana kidogo kidogo hukamilisha kibaba..?

Nategemea majiby yako mkuu!
CC: Kiranga
Daah ngoja nifatilie habari za chama na mondi 🤣🤣🤣
 
Wewe mbona huleti sources zako za information?

Huelezi umefanya nini kwenye world of science?

Weka hapa researchs zako na tafiti zako za kisayansi tofauti na hizo za Wikipedia..
Mimi sina ujuaji
Mimi taosim siijui ndo naisikia yaani kitu ambacho sikijui nianze kukipinga

Mimi sio wewe unapinga pinga tu hata mambo huyajui
 
Kama binadamu tumeweza ku overcome Nature kwa baadhi ya mambo mfano kurusha ndege 🛫, kurusha satellites, kupeleka vyombo mwezini na anga za juu zaidi kwa kuweza ku overcome force of gravity, Je huoni kwamba siku za mbeleni tutaweza mambo mengi zaidi?
Hakuna mapya yajayo yatakayoenda against nature
 
Wewe unataka kupewa majibu kulingana na kile unachofahamu tu na kutaka kila swali lifuate mrengo wa jibu unalotaka kusikia kama vile unavyo fahamu tu.

Ukisikia jibu tofauti na unalotaka kusikia unasema ni ubishi.
Nasaidia kumjibia uliyemuuliza.

Mimi nipo kujifunza hapa,

Sina nalofahamu kuhusu haya nayoyasoma hapa, sijatia neno lolote nipo natafakari ili badae katika tafakuri zangu nione kama ntapata maswali ya kumuuliza mtoa mada ili nielewe zaidi.


Hii ni tofauti na wewe, huwa unakuja juu na maswali ya kuonyesha wazi kuwa unapinga kwenye mada ambayo unaona hauielewi...

Ndio maana unaitwa kwa majina tofauti hapo, Mara kilaza and etc

Na kingine punguza pupa, Una pupa ya kujibu kila kitu ambacho hakitoshi kwenye uelewa wako ndio maana unaitwa mjuaji.

Wewe husomi ili uelewe unachokisoma, Unasoma haraka haraka ili uje kupinga unachokisoma.

Badilika.
 
"In Taoism, nature is viewed as an integral part of the Tao, which is the fundamental force that flows through all things"

Hii sehemu yenyewe tu imekaa ambiguous.

Kwanza, inaanza kwa kutoeleza nature ni nini, inaanza kwa kueleza how nature is viewed in Taoism.

Hatuambiwi the essence of nature, tunaambiwa a Taoist interpretation of nature.

Halafu, tunaambiwa nature ni an integral part of the Tao. Which still does not tell us anything about the essence of nature. We are merely told of nature as a characteristic of the Tao.

Yani ni kama uambiwe kuwa "the atom is an integral part of matter". Hatujui characteristic za atom, hatujaambiwa ina spin, angular momentum, subatomic particles, how does it get to be an atom and not a molecule, tunajua characteristic za matter, you are telling us more about matter than the atom. Na hatujui kuwa kuna ma element na ma molecule nayo ni ma integral parts of matter.

You are telling us more about the Tao than about nature.

Halafu tunapata confusion zaidi tunapoambiwa "which is the fundamental force that flows through all things".

Which which is which?

Is the Tao the fundamental force that flows through all things? Or was this fundamental force which flows though all things part referring to nature?
What really is your point chief. Kama kuna maswal unaona hawajib sawa bas fanya wewe kuweka sawa na maelezo ya kutosha sote tujifunze. Ujue ukiuliza swal mara ya kwanza ukaluliza tena kwa njia nyine na tena na tena but hupat majibu, kwann usitoe wewe hiyo elimu ili kuwasaidoa unaowauliza maswali na hawakujibu?
 
Umefanya nini kwenye world of science
Kwa sababu unatumia nguvu ya kubisha ili ushinde na sio hoja
Yan mtu mbishi mbish huwa anakera sana.. kama unaona wewe una ufaham mpana huendan na watu but toa elimu au lah kaa kimya acha watu wajifunze..unapoona hapaend sawa badala ya kukosoa, elekeza!.
 
Okay.. vizuri. Lakini ngoja nikueleweshe.

Kwanza mfano wa Draft ni irrelevant hapa coz ina finite moves, lkn universe haina finite moves. Labda ungesema chess au go, na zote zisingelezea ninachomaanisha

Tai Chi inaunganisha Biomechanics, breathing, human physiology, etc... kujua mtu akijikunja vp basi ana uwezekano wa kufanya nn.

Sasa Taoism imekusanya kila kitu kwenye huu ulimwengu na kukupa Guiding principles, kumbuka Tai Chi ni part tu ya Taoism.

Ninachoona wewe umefocus zaidi na mifano niliotoa badala ya elimu ninayotoa. Focus kwenye elimu ninayotoa.
Mwamba unajua sana👍
 
Huyo alibahatika kutabiri na sio uchawi.
Sayansi ya uchawi ufanya KAZI kama ilivyo mfumo wa umeme lazima pawe na chanzo kupitia mawimbi nguvu ya uchawi inasafiri thus unaweza mloga mtu aliye marekani na akadhurika kupitia manuizi.
Naomba mniroge nipo Mwanza...mnitumie hayo manuizi yenu...
 
Back
Top Bottom