Hii nakupa kutokana na uzoefu mkuu
Mwaka 2019 nilimuuguza mama akiwa na umri karibu na mzee wako ye alikuwa 65 kwa ugonjwa huo huo na Sasa amepona yuko sawa akiwa na 70 yake
Nilimpeleka regency wakampa dawa ya dharula Kisha Dr kisanga anakanipa number ya Dr Njenje yuko hapo muhimbili
Jamaa Wana hospital Yao pale nje ya muhimbili kama unaenda mbele kidogo ratiba zao huwa ni asubuhi na mapema sana
Jamaa akanishauri nikaenda kule kinondoni kwa wachina kufanya scan ikaonesha athari
Nikarejea akaniandika dawa mbili ambazo gharama ilifikia kama 2000000
Nikaenda pale Robby one kariakoo nikawa nazinunua kwa mafungu anameza hadi akawa sawa
Angalizo dogo
Jitahidi utumie private hospital kama hao na wale wachina wa kinondoni ili usikawie sana na mgonjwa asichoke na abadani usitumie mitishamba au dawa za asili zinaweza kufanya tatizo liwe kubwa zaidi
Mwisho naamini mzee atakuwa sawa sana
Awe anapata mda wa kupumzika na sio Kila saa kumuuliza unajisikiaje