Je, tausi anaweza kuishi mwenyewe porini?

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Au wameshakuwa kama kuku kwamba bila kufugwa na watu hawawezi kustawi? Karibuni kwa taarifa wajuzi!
 
Yule ndege haitwi tausi. Lakini watu wengi hawajui hilo. Yule anaitwa ndege mnana. Au ndege mwanana. Tausi ni jina la mkia wake na haswa pale anapouchanua na kutengeneza ua. Lile ua ndilo tausi.
Sawa mkuu turudi sasa kwenye swali
 
au wameshakuwa kama kuku kwamba bila kufugwa na watu hawawezi kustawi? karibuni kwa taarifa wajuzi!
Wanaishi porini. Kuna tausi wa aina tatu. Aina mbili zinapatikana Asia na nyingine Afrika, Congo. Ukienda maeneo ya bonde la Congo utakuta hao wa aina ya Afrika. Tembelea mbuga inaitwa Salonga National Park, utawaona.
 
Kama ni jamii ya wanaofugwa inakuwa ngumu ukimuweka porini ila kama ni wa porini anajiadapt kuishi porini hii ni kwenye jamii kubwa ya wanyama hata paka mfano kuna wa nje na wa ndani sasa yule wa nje ndo anakimbiza panya na kuwaua n.k lakini paka wa ndani ndo kwanza atacheza nae 😅😅 au atamuangalia akimbie yeye 🤣🤣🤣 kwasababu anakuwa hana survival skills kama za paka wa nje!
 
Yule ndege haitwi tausi. Lakini watu wengi hawajui hilo. Yule anaitwa ndege mnana. Au ndege mwanana. Tausi ni jina la mkia wake na haswa pale anapouchanua na kutengeneza ua. Lile ua ndilo tausi.
oh, kumbe!!!!
ahsante kwa elimu hii
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
paka wa ndani wanazingua sana......halafu wanajenga tabia ya kudeka kadiri wanavyokuzoea. niliachana kabisa na suala la kufuga paka
 
Hakuna mnyama wa nyumbani anapenda starehe kama paka. Yaani yeye muda wote anadeka tu, mara ajisogeze kwenye miguu yako..kupumzika hapumziki kwenye sakafu kama wenzake, yeye ni juu ya sofa.
 
Wanaishi porini. Kuna tausi wa aina tatu. Aina mbili zinapatikana Asia na nyingine Afrika, Congo. Ukienda maeneo ya bonde la Congo utakuta hao wa aina ya Afrika. Tembelea mbuga inaitwa Salonga National Park, utawaona.
anhaa, ahsante sana kiongozi!!
 
Hakuna mnyama wa nyumbani anapenda starehe kama paka. Yaani yeye muda wote anadeka tu, mara ajisogeze kwenye miguu yako..kupumzika hapumziki kwenye sakafu kama wenzake, yeye ni juu ya sofa.
hahahahaaaa, ni kweli kabisa!
 
Yule ndege haitwi tausi. Lakini watu wengi hawajui hilo. Yule anaitwa ndege mnana. Au ndege mwanana. Tausi ni jina la mkia wake na haswa pale anapouchanua na kutengeneza ua. Lile ua ndilo tausi.
Rudi kwenye mada...acha ujuaji
 
Hakuna mnyama wa nyumbani anapenda starehe kama paka. Yaani yeye muda wote anadeka tu, mara ajisogeze kwenye miguu yako..kupumzika hapumziki kwenye sakafu kama wenzake, yeye ni juu ya sofa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanazingua
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
paka wa ndani wanazingua sana......halafu wanajenga tabia ya kudeka kadiri wanavyokuzoea. niliachana kabisa na suala la kufuga paka
Acha kudeka, mpuuzi sana paka anaweza akakulia pose mjengoni kama mlipa kodi wanalinga sana.
 
Paka mi hua ananifurahisha tu alivyo hana shobo na anavyowadharau wanyama wengine hasa mbwa. Yani paka hua anajiona yeye ndio mwenye haki humo ndani na hana mda wa kuhangaika kujipendekeza kwa mwanadamu. Ukiwa unafuga paka na mbwa, ukirudi nyumbani ni kama paka hua anamuambia mbwa "oya.. we mbwa.. hebu kimbia kampokee bosi wako.." yeye ndio kwaanza anageukia upande wa pili anaendelea kuchapa usingizi 😂😂😂
 
Back
Top Bottom