Je, Time Travel Inawezekana? Einstein Alitupa Jibu Miaka Kadhaa Iliyopita

Je, Time Travel Inawezekana? Einstein Alitupa Jibu Miaka Kadhaa Iliyopita

Jamaa upo humble sana..
Daah aiseee hongera sana mkuu 🙏🙏🙏🙏🙏🙏 unajua nini mkuu haya maisha haya acha tuu
I feel you bro unajua kua upside-down ni lazma ziwepo tu kwa kila aliepo hai japokuwa zinatofautiana.
Waambie bana haya maphysics na chemistry tunayajua sana ila tulishindwa kuyageuza hela tukayaweka kando na kuanza kuzisaka
Ni kweli kabsa bro makebo hujakosea unayoyasema 😂😂
 
Waambie bana haya maphysics na chemistry tunayajua sana ila tulishindwa kuyageuza hela tukayaweka kando na kuanza kuzisaka
Kweli kabisa mkuuu..
Yaani mpaka sasa naangaliaga show wanazofanya wale madogo kule insta naina kabisa ni mambo yangu.

Miaka imepita ila kichwa kimejaa madini kama library ila nikiwaza mambo ya pesa tuu nachoka
 
Kwa hiyo tukisafiri kwenda past, present yetu inakuwa future, na tukienda future present yetu inakuwa past. Si ndio!?
Tukisafiri kwenda future ni sahihi present itakuwa past, lakini tukienda past present yetu haiwezi kuwa future.

kwasabubu future ina-time line ambayo hatujawahi iishi, lakini tukisema past maana yake tayari tunakuwa tumewai ishi kwenye hiyo timeline.
 
Umeeleza relativity vizuri, na Uislamu haupingani na ukweli wa kisayansi kwamba muda unaweza kuhusiana na mwendo na mazingira ya gravitational field. Lakini kuna jambo muhimu: relativity si ushahidi kwamba Einstein aligundua asili kamili ya muda.

Qur’an yenyewe inaonyesha kwamba kipimo cha muda kwa viumbe si lazima kiwe sawa na kipimo chetu. Allah anasema:

“Na hakika siku moja kwa Mola wako ni kama miaka elfu katika mnayoyahesabu.”
(Qur’an 22:47)

Na pia:

“Malaika na Roho hupanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu hamsini.”
(Qur’an 70:4)

Hivyo, kwa mtazamo wa Kiislamu, muda ni kiumbe cha Allah, na Allah ndiye aliyeumba space, time na ulimwengu. Qur’an haisemi kwamba binadamu anaweza kurudi nyuma katika historia kwa kutumia time machine.

Kwa hiyo relativity inaweza kutuonyesha kwamba muda haupimwi kwa namna moja kwa kila mwangalizi, lakini haiwezi kuthibitisha kwamba mwanadamu anaweza kubadilisha yaliyopita.

Na hapa ndipo tofauti muhimu ipo: sayansi inaeleza jinsi ulimwengu unavyofanya kazi; Qur’an inatueleza nani aliyeuumba ulimwengu huo na kwamba uwezo wa Allah hauwekewi mipaka na vipimo vya viumbe.

Kwa hiyo usichanganye “time dilation” ya Einstein na madai kwamba mwanadamu amegundua siri yote ya muda. Bado kuna mengi ambayo sayansi yenyewe haijayajua.
Mzee wa Kuruani na Allah...😂

kwenye kila jambo unaweka Quran.

Sema nyie waislamu huwa mnashangaza sana.😂
 
Nataka kurudi nyuma time travel mnisaidie nifanyeje nione maisha ya huko nyuma Tena naseti nitokee 1960
 
Kidogo nimepata idea ya movie baada ya kusoma andiko lako😅


Movie ya Interstellar unaifahamu lakin?
20260823_201259.jpg

Kama ya Cooper ambayo wanaenda sayari nyingine kutafta sehemu binadamu wanayo weza kuishi.

nisawa naifahamu japo kulikua na confusion sikuielewa vizuri.
 
Hapana mkuu ni genre gani ?
Ni Sci-Fi, Kwenye hii filamu, muda hauendi sawa kwa kila mtu kama ulivyotanabaisha kwenye uzi sema kwenye movie inatokana na nguvu ya uvutano (gravity) ya shimo jeusi (Gargantua) saa moja kwenye sayari ya Miller ni sawa na miaka 7 ya duniani. Hii inasababisha main Character Cooper kubaki kijana wakati binti yake duniani anazeeka na kuwa mzee kuliko baba yake. Uhusiano huu wa muda unachanganya akili za wengi ikiwamo mimi, Pia kuna mahala Cooper anaongea na binti yake wakati huo huo Cooper yupo sayari nyingine 5D sijui anyways sielewi kifupi
 

Attachments

  • p10543523_p_v8_as.jpg
    p10543523_p_v8_as.jpg
    288.9 KB · Views: 7
Kuna kitu cha kushangaza kuhusu universe ambacho wengi tunakiona kila siku bila kufikiria sana muda hauendi kwa speed moja kwa kila mtu.

Einstein alionyesha kupitia Special Relativity kwamba kadri kitu kinavyosafiri kwa speed kubwa sana, karibu na speed ya mwanga, muda wake unaweza kupita polepole ukilinganisha na mtu anayebaki katika hali tofauti ya mwendo.

Kwanza tuweke fact sawa speed ya mwanga kwenye vacuum ni takribani c = 3 × 10⁸ m/s, yaani karibu kilomita 300,000 kwa sekunde.

Kwa speed hiyo, mwanga unaweza kuzunguka Dunia takribani mara 7.5 ndani ya sekunde moja. Hii ndiyo “speed limit” ya universe kwa taarifa na vitu vyenye mass, kulingana na relativity.

Sasa tuingie kwenye calculation. Kuna formula maarufu inayotumika kuelezea time dilation γ = 1/√(1 − v²/c²).

Usiiogope formula hii, tunaweza kuifanya simple. Tuchukulie spaceship yetu inasafiri kwa 90% ya speed ya mwanga, hivyo v = 0.9c.

Tunaweka kwenye formula:

γ = 1/√(1 − 0.9²) = 1/√0.19 ≈ 2.29.

Hii ina maana kwamba kwa kila saa 1 inayopita kwenye spaceship, takribani saa 2.29 zinaweza kupita katika reference frame ya Earth.

Ukiwa unasafiri kwa masaa 10 kulingana na clock yako, Earth inaweza kuwa imepita takribani masaa 22.9.

Hapo tayari unaona kitu cha ajabu wewe na mtu wa Earth mnaweza kuondoka pamoja, lakini mkakutana tena mkiwa na muda tofauti kwenye clocks zenu.

Sasa twende mbali zaidi. Fikiria spaceship inaweza kufika 99% ya speed ya mwanga. Hapo v = 0.99c, na calculation inakuwa:

γ = 1/√(1 − 0.99²) = 1/√0.0199 ≈ 7.09.

Kwa hiyo ukiwa kwenye spaceship kwa mwaka 1 kulingana na saa yako, katika reference frame ya Earth inaweza kuwa imepita takribani miaka 7.1.

Ukiweza kusafiri kwa 99.9% ya speed ya mwanga, γ inakuwa takribani 22.4.

Hivyo mwaka mmoja kwako unaweza kuhusishwa na zaidi ya miaka 22 kwenye Earth.

Hii ndiyo sababu wanasayansi husema relativity inaweza kuruhusu aina ya one way time travel kwenda future.

Si kwamba umefungua portal; wewe umefanya muda wako upite kwa kiwango tofauti na cha watu wengine.

Lakini kuna detail moja muhimu sana: hii haimaanishi binadamu anaweza sasa hivi kutengeneza spaceship inayokwenda 99.9% ya speed ya mwanga.

Kadri kitu chenye mass kinavyokaribia speed ya mwanga, ndivyo energy inayohitajika inavyoongezeka sana.

Kwa mfano, kufikia exactly c = 3 × 10⁸ m/s kwa object yenye mass si jambo tunaloweza kufanya kwa physics yetu ya sasa.

Equation yenyewe inaonyesha Lorentz factor ikiendelea kupanda bila kikomo kadri v → c.

Kwa hiyo kusema “tusafiri tu kwa speed ya mwanga halafu turudi past” si sahihi.

Speed ya mwanga inaweza kutusaidia kuelewa time dilation na kusafiri kuelekea future kwa maana ya relativity, lakini haitoi proof kwamba tunaweza kurudi nyuma kwenye past.

Na hapa ndipo mystery yenyewe inaanza.

Kama siku moja technology ingeturuhusu kusafiri karibu sana na speed ya mwanga, ungeweza kuondoka Earth, kusafiri kwa miaka michache kulingana na wewe, halafu urudi na kukuta Earth imezeeka kwa miongo au hata zaidi kutegemea speed na journey.

Hiyo ni aina ya real, physics based time travel kwenda future.

Lakini kuhusu kurudi kwenye past, kuna theoretical ideas kama wormholes na baadhi ya spacetime solutions, lakini bado hakuna ushahidi wa experimental unaoonyesha kwamba binadamu anaweza kuzitumia kama time machine.

Kwa hiyo swali kubwa si tu “Can humans travel through time?”

Bali ni kama universe tayari inaruhusu muda kupita tofauti kulingana na speed na gravity, je, kuna kiwango cha juu zaidi cha physics ambacho bado hatujakigundua?

Labda future ya time travel haiko kwenye machine pekee. Labda iko kwenye jinsi tunavyoelewa space, time, speed na spacetime yenyewe.

dosho12 and Poker
Sponsored by chat GTO
 
Kwenda mbele (future) inawezekana kabisa bila Shaka, lakini kurudi nyuma (past) itakuwa ni ndoto itakayolaza watu na viatu lakini labda inawezekana huko mbeleni.

Mimi Naamini wenzetu washafikia teknolojia ya kusafiri zaidi ya spidi ya mwanga lakini hawataki tu kutuonesha Kwa sababu wanazojua wao hasa US na Urusi au na China...

Kuhusu kurudi nyuma hapo unazungumzia kubadilisha hatima za watu, sio kubadilisha toka ulivyozaliwa, Bali kubadilisha pale ulipofikia kuanzia sasa hivi na kwenda mbele....Hii ishu ya kurudi nyuma lazima watu wachanganyikiwe maana it doesn't make sense.
 
Nilichogundua unaweza na Ufahamu mkubwa sana kuhusua haya mambo lakini je ni vipi yanaweza kusaidia mtu kupata ugali wa kila siku ...

Hapo ndo likaja wazo kumbe haya mambo ni story kama story zingine

Vijana tufanye kazi kwa bidii. Vijana tutafute pesa aiseee
Sio story, hayo mambo ndio yamewezesha kupata technology kama internet, rockets,GPS etc na hizo technology ukiwa mbunifu utapiga pesa, mfano uber ametumia internet na GPS technology kutengeneza multibillion business, facebook ukiangalia ni internet na GPS pia,hata Boeing, auto industry, weapons systems etc zote ni kutokana research na theory kama hizi, mambo yanaanzia kwenye theory discovery,academic research, halafu technology then watu wenye akili wanatafuta applications business zinazaliwa watu wanapiga pesa, dunia ya leo bila algorithm and matrix tusingekuwa na hii modern digital life kama cellphone na computer, na ziko research nyingi sana bado hazijapata applications zimekaa tuu kwenye lab na universities libraries
 
Nilichogundua unaweza na Ufahamu mkubwa sana kuhusua haya mambo lakini je ni vipi yanaweza kusaidia mtu kupata ugali wa kila siku ...

Hapo ndo likaja wazo kumbe haya mambo ni story kama story zingine

Vijana tufanye kazi kwa bidii. Vijana tutafute pesa aiseee
Mkuu,

Kuna watu wanaliga hela ndefu jwa kutengeneza videos za kuelezea haya mambo Youtube.

Zamani nilikuwa nayasoma sana kwenye vutabu, hususan pale United States Infirmation Service Centter Peugeot House miaka hiyo ya 1990s.

Siku hizi yanaelezewa kirahisi sana Youtube.

Watu wanatengeneza pesa kwa views za Youtube.
 
Kuna kitu cha kushangaza kuhusu universe ambacho wengi tunakiona kila siku bila kufikiria sana muda hauendi kwa speed moja kwa kila mtu.

Einstein alionyesha kupitia Special Relativity kwamba kadri kitu kinavyosafiri kwa speed kubwa sana, karibu na speed ya mwanga, muda wake unaweza kupita polepole ukilinganisha na mtu anayebaki katika hali tofauti ya mwendo.

Kwanza tuweke fact sawa speed ya mwanga kwenye vacuum ni takribani c = 3 × 10⁸ m/s, yaani karibu kilomita 300,000 kwa sekunde.

Kwa speed hiyo, mwanga unaweza kuzunguka Dunia takribani mara 7.5 ndani ya sekunde moja. Hii ndiyo “speed limit” ya universe kwa taarifa na vitu vyenye mass, kulingana na relativity.

Sasa tuingie kwenye calculation. Kuna formula maarufu inayotumika kuelezea time dilation γ = 1/√(1 − v²/c²).

Usiiogope formula hii, tunaweza kuifanya simple. Tuchukulie spaceship yetu inasafiri kwa 90% ya speed ya mwanga, hivyo v = 0.9c.

Tunaweka kwenye formula:

γ = 1/√(1 − 0.9²) = 1/√0.19 ≈ 2.29.

Hii ina maana kwamba kwa kila saa 1 inayopita kwenye spaceship, takribani saa 2.29 zinaweza kupita katika reference frame ya Earth.

Ukiwa unasafiri kwa masaa 10 kulingana na clock yako, Earth inaweza kuwa imepita takribani masaa 22.9.

Hapo tayari unaona kitu cha ajabu wewe na mtu wa Earth mnaweza kuondoka pamoja, lakini mkakutana tena mkiwa na muda tofauti kwenye clocks zenu.

Sasa twende mbali zaidi. Fikiria spaceship inaweza kufika 99% ya speed ya mwanga. Hapo v = 0.99c, na calculation inakuwa:

γ = 1/√(1 − 0.99²) = 1/√0.0199 ≈ 7.09.

Kwa hiyo ukiwa kwenye spaceship kwa mwaka 1 kulingana na saa yako, katika reference frame ya Earth inaweza kuwa imepita takribani miaka 7.1.

Ukiweza kusafiri kwa 99.9% ya speed ya mwanga, γ inakuwa takribani 22.4.

Hivyo mwaka mmoja kwako unaweza kuhusishwa na zaidi ya miaka 22 kwenye Earth.

Hii ndiyo sababu wanasayansi husema relativity inaweza kuruhusu aina ya one way time travel kwenda future.

Si kwamba umefungua portal; wewe umefanya muda wako upite kwa kiwango tofauti na cha watu wengine.

Lakini kuna detail moja muhimu sana: hii haimaanishi binadamu anaweza sasa hivi kutengeneza spaceship inayokwenda 99.9% ya speed ya mwanga.

Kadri kitu chenye mass kinavyokaribia speed ya mwanga, ndivyo energy inayohitajika inavyoongezeka sana.

Kwa mfano, kufikia exactly c = 3 × 10⁸ m/s kwa object yenye mass si jambo tunaloweza kufanya kwa physics yetu ya sasa.

Equation yenyewe inaonyesha Lorentz factor ikiendelea kupanda bila kikomo kadri v → c.

Kwa hiyo kusema “tusafiri tu kwa speed ya mwanga halafu turudi past” si sahihi.

Speed ya mwanga inaweza kutusaidia kuelewa time dilation na kusafiri kuelekea future kwa maana ya relativity, lakini haitoi proof kwamba tunaweza kurudi nyuma kwenye past.

Na hapa ndipo mystery yenyewe inaanza.

Kama siku moja technology ingeturuhusu kusafiri karibu sana na speed ya mwanga, ungeweza kuondoka Earth, kusafiri kwa miaka michache kulingana na wewe, halafu urudi na kukuta Earth imezeeka kwa miongo au hata zaidi kutegemea speed na journey.

Hiyo ni aina ya real, physics based time travel kwenda future.

Lakini kuhusu kurudi kwenye past, kuna theoretical ideas kama wormholes na baadhi ya spacetime solutions, lakini bado hakuna ushahidi wa experimental unaoonyesha kwamba binadamu anaweza kuzitumia kama time machine.

Kwa hiyo swali kubwa si tu “Can humans travel through time?”

Bali ni kama universe tayari inaruhusu muda kupita tofauti kulingana na speed na gravity, je, kuna kiwango cha juu zaidi cha physics ambacho bado hatujakigundua?

Labda future ya time travel haiko kwenye machine pekee. Labda iko kwenye jinsi tunavyoelewa space, time, speed na spacetime yenyewe.

dosho12 and Poker
Umeelezea vizuri.

Ingekuwa vizuri zaidi ungeelezea speed ya juu kabisa inayowezekana sasa na relativistic effects zake.

Na pengine energy inayotakiwa kusafirisha uzito wa mtu average na spaceship inakuwaje.

Na pengine namna tofauti za kuipata energy hiyo na changamoto zake kubeba energy ambayo inaongeza uzito na hivyo kuhitaji energy zaidi kusafirisha energy.

Na suluhisho la energy isiyo na uzito sana kama nuclear.

Kuna mengi sana ya kuzungumzia hapa, nineona mengi yameelezeea kwa Kiingwrwza lakini ninefurahia umejaribu kuelezea kwa Kiswahili.
 
Back
Top Bottom