Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Naitaji ramani pia
Kwa nyumba ya kawaida ya vyumba vitatu vya 3.5m*3.5m yanatosha ila inategemea na ukubwa wa msingi wa hiyo nyumba kutokana na mazingira ya eneo husika, maana matofali ya msingi yanalazwa (kama msingi mrefu yatatumika mengi) wakati matofali ya juu ya msingi ni ya kusimamisha tu (kuna baadhi ya vibopa na nyumba za serikali wanalaza pia).
 
Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Naitaji ramani pia
3D image ndio hio..

Screenshot_20210306-082838~2.jpg
 
Ramani ninayo, kama utahitaji ni Tshs 150,000/=

Unaenda mbali sana, ramani siku hizi tunapata kwa 10K.
Kadri siku zinavyoenda ndio umuhimu wa ramani zenu unapungua, watu waliosoma Civil Eng nao wanachora ramani siku hizi, architects nao wanachora unakuta mpaka masela wangu wa electrical nao wamo. Yaani ilimradi vurugu tu.

Auto CAD na zinginezo zimekuwa kimeo, kuna jamaa yangu kasoma account naye saiv anachora ramani tena za hali ya juu.

Sikukatishi tamaa ila hiyo bei umeweka kwa matarajio makubwa sana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ramani ni muhimu sana katika ujenzi na gharama zake kwa mtaalamu anayejielewa haipungui 500k...

Nafahamu lakin saivi hali ilivyo unaweza kuwa unajielewa na hizo ramani zako za 500K alaf kuna wajuba wanauza 10K tena ramani safi kuliko zako za 500K.

JPM sio mtu wa mchezo mchezo, zamani architects wanalinga, Civil wanalinga saiv hata ukimpa Civil 10K anashukuru anakuchorea ramani matata sana[emoji23][emoji23]
 
Kabla ya kujua kuwa zinatosha au la, ulitakiwa utupe maelezo ya eneo unalotarajia kuanza ujenzi na mkoa.

Mfano Dar hakuna mawe mengi na ukifanikiwa kuyapata ni gharama kubwa, lakini mikoa mingi wanajengea msingi mawe.

Kingine unajenga nyumba ya muundo gani, mfano master bedroom ngapi nk.
 
Kabla ya kujua kuwa zinatosha au la,ulitakiwa utupe maelezo ya eneo unalotarajia kuanza ujenzi,na mkoa...
Eneo ni Dar, chanika lengo nahitaji nyumba yenye vyumba 3, vyumba 2 vya kawaida na master 1, jiko, dining, choo
 
Back
Top Bottom