Ni sawa mkuu, lakini swala la wewe kudownload movie au nyimbo ni kweli na ukidownload kisha usiipende haitokigharimu chochote kuifuta na kujaribu kudownload nyingine, lakini ukijenga nyumba kwa ramani isiyokidhi ubora au mahitaji ya site yako jiulize ni gharama kiasi gani utahitaji kutatua tatizo, ni kama mtu anaelima kwa mara ya kwanza anawekeza 2M+ kisha anaona tabu kutoa pesa kidogo kwaajili ya consultation kwa mkulima mzoefu, au mtu anaeingia mkataba wa mamilion kisha anaona tabu kutoa pesa kwa mwanasheria kumsaidia na kumshauri, kuna watu wengi wanatapeliwa viwanja kisa tu aliona tabu kuiweka hiyo kisheria au hata kuwalipa kidogo serikali ya mtaa kwenye mauziano, matokeo yake unapoteza million 5+ kisa eti uliona gharama kutoa laki moja. Haya mambo yapo na watu wataendelea kuumia na wabongo wepesi wa kusahau na tunapenda sana shortcut.
Unajenga nyumba ya 30+ unaona tabu kulipia ramani Tsh laki tatu, ufanye kitu cha uhakika zaidi na ushauri wa mambo ya msingi ya kuzingatia ikiwemo na namna ya kupunguza gharama za ujenzi wako