Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Mi nauliza, Hivi ukianza msingi kwa mawe hauwezi kujenga kwa block za simenti??
Unaweza. Na msingi wa mawe ndio imara zaidi kwenye maeneo yenye high capillarity kwani mawe yafyonzi maji.
 
Eneo ni Dar , chanika lengo naitaji nyumba yenye vyumba 3,,,, vyumba 2 vya kawaida na master 1 ,,jiko , dining, choo ,
Kwa ushauri wangu, nadhani tufanye tofali 3500, kwasababu utaanza na msingi, ukienda tofali chache ni buku hadi buku jero.

Na tofali za msingi hulazwa kwahiyo zinaenda za kutosha kidogo.

Kanuni ya ujenzi, unaambiwa ni bora material yaongezeke kuliko kupungua.

Ongeza hizo 700 chief alafu muite fundi ili hata zikibaki zikusaidie baada ya kupiga bati kukazia.

A
 
Nafahamu lakin saivi hali ilivyo unaweza kuwa unajielewa na hizo ramani zako za 500K alaf kuna wajuba wanauza 10K tena ramani safi kuliko zako za 500K.

JPM sio mtu wa mchezo mchezo, zamani architects wanalinga, Civil wanalinga saiv hata ukimpa Civil 10K anashukuru anakuchorea ramani matata sana[emoji23][emoji23]
Hiyo 10K unamaanisha 10,000 au 100,000? Kama ni ten basi huo ni uongo ulikithiri labda kwa wanafunzi wa chuo

Pia unless ni ramani za kujenza kwenye slums ila kama ni ya kujenga kwenye plots zilizopangwa hakuna kitu kama hicho
 
Hapa ndipo tunapofeli wabongo. Kupenda sana shortcut. Hakuna mtu atakaa chini aanze kukuchorea ramani kwa 10k, sanasana ni utapewa tu michoro iliyotumika kwenye kiwanja cha mtu mwingine utumie kwenye kiwanja chako na baadae ukishajenga ndio utakugundua kuna vitu vingi havikuzingatiwa maana ili ramani iwe fit ni lazima kufanyike site analysis kwa mchoraji kuja kuona eneo lako na kuzingatia baadhi ya vitu kama north direction, access road, type of soil, water table na dampness ya eneo husika n.k.

Hivyo vyote vitasaidia kwa mchoraji kujua ni namna gani afanye proper zoning kwenye design yako na vitu gani apendekeze ili kupata nyumba yenye ubora kulingana na jiografia ya eneo husika. Kupenda sana shortcut ndio maana watu wengi wanalalamika nyumba zao zina cracks, nyumba zinasumbuliwa na fangasi na naamini kuna watu wengi wanajenga nyumba huku sebule, master bedroom na vyumba vingine muhimu vikiwekwa upande wenye jua kali huku vyoo, jiko au store vikiwa upande wenye kiupepo na hakuna jua kali, yote ni matokeo ya kupenda sana slope. Ukienda kwenye kurasa za ujenzi kwenye mtandao ya kijamii utakuta watu wengi wanaomba ushauri kwa mambo ambayo walitakiwa kuyachukulia tahadhari kwenye hatua za mwanzo za ujenzi.

Unajikuta unaanza kutoa pesa nyingi kuzuia cracks au fangasi kwenye nyumba. Sio mbaya kupenda vitu vya gharama nafuu lakini tuwe tunajaribu kutafuta hata ushauri kidogo na ku reason kidogo pia.
 
Hiyo 10K unamaanisha 10,000 au 100,000? Kama ni ten basi huo ni uongo ulikithiri labda kwa wanafunzi wa chuo

Pia unless ni ramani za kujenza kwenye slums ila kama ni ya kujenga kwenye plots zilizopangwa hakuna kitu kama hicho
Hadi za bure zipo, ramani siku hizi sio ishu labda usiwe mjanja au labda Kama unataka kujenga ghorofa! Ila kikawaida tu ramani sio ishu, nazungumza hivyo cause hata Mimi ramani sikununua...
 
Hiyo 10K unamaanisha 10,000 au 100,000? Kama ni ten basi huo ni uongo ulikithiri labda kwa wanafunzi wa chuo

Pia unless ni ramani za kujenza kwenye slums ila kama ni ya kujenga kwenye plots zilizopangwa hakuna kitu kama hicho

10k hata kuprint tu ramani haitoshi, afu mtu akae kwenye autocad week nzima umpe 10k labda kama ramani kadownload pintirest
 
Hapa ndipo tunapofeli wabongo. Kupenda sana shortcut. Hakuna mtu atakaa chini aanze kukuchorea ramani kwa 10k, sanasana ni utapewa tu michoro iliyotumika kwenye kiwanja cha mtu mwingine utumie kwenye kiwanja chako, na baadae ukishajenga ndio utakugundua kuna vitu vingi havikuzingatiwa maana ili ramani iwe fit ni lazima kufanyike site analysis kwa mchoraji kuja kuona eneo lako na kuzingatia baadhi ya vitu kama north direction, access road, type of soil, water table na dampness ya eneo husika n.k. Hivyo vyote vitasaidia kwa mchoraji kujua ni namna gani afanye proper zoning kwenye design yako na vitu gani apendekeze ili kupata nyumba yenye ubora kulingana na jiografia ya eneo husika. Kupenda sana shortcut Ndio maana watu wengi wanalalamika nyumba zao zina cracks, nyumba zinasumbuliwa na fangasi na naamini kuna watu wengi wanajenga nyumba huku sebule, master bedroom na vyumba vingine muhimu vikiwekwa upande wenye jua kali huku vyoo,jiko au store vikiwa upande wenye kiupepo na hakuna jua kali, yote ni matokeo ya kupenda sana slope. Ukienda kwenye kurasa za ujenzi kwenye mtandao ya kijamii utakuta watu wengi wanaomba ushauri kwa mambo ambayo walitakiwa kuyachukulia tahadhari kwenye hatua za mwanzo za ujenzi.
Unajikuta unaanza kutoa pesa nyingi kuzuia cracks au fangasi kwenye nyumba.
Sio mbaya kupenda vitu vya gharama nafuu lakini tuwe tunajaribu kutafuta hata ushauri kidogo na ku reason kidogo pia
Nitazingatia ushauri wako
 
Unaenda mbali sana, ramani siku hizi tunapata kwa 10K.
Kadri siku zinavyoenda ndio umuhimu wa ramani zenu unapungua, watu waliosoma Civil Eng nao wanachora ramani siku hizi, architects nao wanachora unakuta mpaka masela wangu wa electrical nao wamo. Yaani ilimradi vurugu tu.

Auto CAD na zinginezo zimekuwa kimeo, kuna jamaa yangu kasoma account naye saiv anachora ramani tena za hali ya juu.

Sikukatishi tamaa ila hiyo bei umeweka kwa matarajio makubwa sana
emoji23.png
emoji23.png
[emoji
10k ata kuprint tu ramani haitosh, afu mtu akae kwenye autocad week nzima umpe 10k labda kama raman kadownload pintirest
Si ndio hapo, watu wanafikiri ramani ni ule muonekano wa 3D na floor plan basi, ramani kamili inakua na michoro isiyopungua saba au zaidi kulingana na details gani muhimu zinahitajika kwenye design
 
[emoji1787][emoji1787] Huyu ni graduate archtecture sasa lecturer wake usikute kamwambia uki graduate unaweza kujiajiri chorea watu floor map @150k
Mkuu umenikumbusha juzi kuna dogo kaja kwenye duka langu la dawa akaniambia yeye ni famasisti anatafuta kazi ila mshahara lazima uwe 1m na atakuwa anakaaa mara mbili tu kwa wiki. Nikamuuliza mbona gharama iko juu akasema ndio walivyokubaliana chuoni kwamba mtu asikubali chini ya hapo. Nikambia sawa na kwa kuwa sijakutafuta basi sikuhitaji wewe endelea kupokea mshahara huo huo wa 1m mliokubaliana huko chuoni. Baadae akaniomba maji ya kunywa nikamwmbia yanauzwa 500 akasema hana hiyo hela. Nikaendelea kimsisitiza atumie sehemu ya huo mshahara waliokubaliana huko chuoni kwao. Naona hakunielewa vijana siku hizi hawaelewi kabisa dunia inapokwenda
 
😂😂😂Ana leta nadharia za shule
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Si ndio hapo, watu wanafikili ramani ni ulemuonekano wa 3D na floor plan basi, ramani kamili inakua na michoro isiyopungua saba au zaidi kulingana na details gani muhimu zinahitajika kwenye design
Inakuja gharama ndogo kwa sababu sheria za hatimiliki hazifuatwi. Ni sawa na kudownload movies 50 mpaka 100 kwa 10,000/- huku uswazi ni jambo la kawaida.

Au uniambie nidownload nyimbo ya diamond Moja kwa sh. 5000/- hiyo sitofanya hata uniambie quality ipo bora.
Kea sababu kuna piracy.

Ramani zipo tena wilayani surveyor ukimpeleka site anakupitishia mpaka michoro na kibali kwa 50,000/- na zinaendana na mazingira na sheria. nyumba zinasimama poa kabisa.

Tatizo kubwa ni kuwa kAzi za vipaji na ubunifu nchi hii hazisimamiwi na matokeo yake, watu wanakuwa siyo wabunifu.
 
Unaenda mbali sana, ramani siku hizi tunapata kwa 10K.
Kadri siku zinavyoenda ndio umuhimu wa ramani zenu unapungua, watu waliosoma Civil Eng nao wanachora ramani siku hizi, architects nao wanachora unakuta mpaka masela wangu wa electrical nao wamo. Yaani ilimradi vurugu tu.

Auto CAD na zinginezo zimekuwa kimeo, kuna jamaa yangu kasoma account naye saiv anachora ramani tena za hali ya juu.

Sikukatishi tamaa ila hiyo bei umeweka kwa matarajio makubwa sana[emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu nahitaji ramani ya nyumba
Nionganishe na mtu wa kunipatia ramani ya uhakika yet very cheaply.

Nicheck inbox
 
Inakuja gharama ndogo kwa sababu sheria za hatimiliki hazifuatwi. Ni sawa na kudownload movies 50 mpaka 100 kwa 10,000/- huku uswazi ni jambo la kawaida.

Au uniambie nidownload nyimbo ya diamond Moja kwa sh. 5000/- hiyo sitofanya hata uniambie quality ipo bora.
Kea sababu kuna piracy.

Ramani zipo tena wilayani surveyor ukimpeleka site anakupitishia mpaka michoro na kibali kwa 50,000/- na zinaendana na mazingira na sheria. nyumba zinasimama poa kabisa.

Tatizo kubwa ni kuwa kAzi za vipaji na ubunifu nchi hii hazisimamiwi na matokeo yake, watu wanakuwa siyo wabunifu.
Ni sawa mkuu, lakini swala la wewe kudownload movie au nyimbo ni kweli na ukidownload kisha usiipende haitokigharimu chochote kuifuta na kujaribu kudownload nyingine, lakini ukijenga nyumba kwa ramani isiyokidhi ubora au mahitaji ya site yako jiulize ni gharama kiasi gani utahitaji kutatua tatizo, ni kama mtu anaelima kwa mara ya kwanza anawekeza 2M+ kisha anaona tabu kutoa pesa kidogo kwaajili ya consultation kwa mkulima mzoefu, au mtu anaeingia mkataba wa mamilion kisha anaona tabu kutoa pesa kwa mwanasheria kumsaidia na kumshauri, kuna watu wengi wanatapeliwa viwanja kisa tu aliona tabu kuiweka hiyo kisheria au hata kuwalipa kidogo serikali ya mtaa kwenye mauziano, matokeo yake unapoteza million 5+ kisa eti uliona gharama kutoa laki moja. Haya mambo yapo na watu wataendelea kuumia na wabongo wepesi wa kusahau na tunapenda sana shortcut.
Unajenga nyumba ya 30+ unaona tabu kulipia ramani Tsh laki tatu, ufanye kitu cha uhakika zaidi na ushauri wa mambo ya msingi ya kuzingatia ikiwemo na namna ya kupunguza gharama za ujenzi wako
 
Ni sawa mkuu, lakini swala la wewe kudownload movie au nyimbo ni kweli na ukidownload kisha usiipende haitokigharimu chochote kuifuta na kijaribu kudownload nyingine, lakini ukijenga nyumba kwa ramani isiyokizi ubora au mahitaji ya site yako jiulize ni gharama kiasi gani utahitaji kutatua tatizo, nikama mtu anaelima kwa mara ya kwanza anawekeza 2M+ kisha anaona tabu kutoa pesa kidogo kwaajili ya consultation kwa mkulima mzoefu, au mtu anaeingia mkataba wa mamilion kisha anaona tabu kutoa pesa kwa mwanasheria kumsaidia na kumshauri, kuna watu wengi wanatapeliwa viwanja kisa tu aliona tabu kuiweka hiyo kisheria au hata kuwalipa kidogo serikali ya mtaa kwenye mauziano, matokeo yake unapoteza million 5+ kisa et uliona gharama kutoa laki moja. Haya mambo yapo na watu wataendelea kuumia na wabongo wepesi wa kusahau na tunapenda sana shortcut.
Unajenga nyumba ya 30+ unaona tabu kulipia ramani Tsh laki tatu, ufanye kitu cha uhakika zaidi na ushauri wa mambo ya msingi ya kuzingatia ikiwemo na namna ya kupunguza gharama za ujenzi wako
Uzuri wake ni kwamba hizi ramani za 10,000/- na ramani za 500,000/- zote ni sawa.
Kuna mwanajamii hapa alikua anaulizia gharama za ujenzi wa msingi. Ramani aliyoionyesha, Mimi nimeshawahi kuiona mtandaoni kwa $3.00 na ni ramani iliyochorwa kwa ajili ya nyumba itakayojengwa Ghana. Inamilikiwa na Mghana.
Na si kazi yeye kalipa zaidi ya 100,000/- wakati mtu kakopy.
Yaani hata hao wataalam wetu ni copy and paste. Ndiyo maana watu wanaona isiwe tabu. Na nyumba zinasimama poa tu.
 
Duuh noma sanaa [emoji38]
 
Back
Top Bottom