Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Asante mkuu nimejifunza kitu kikubwa sana kwako,, nilishaua injini ya gx100 kwa safari ndefu mwendo mkali na kuizima ghafla pindi ninaposimama, japo haikufa siku hizo ila baadae ilopoteza ubora wake, kurudia tena safari ndefu ikanilaza njiani
 
sasa ipsum unalinganisha na ist, ipsum ina injini kubwa kabisa ya cc2000. ist nafikiri ina 1300cc au 1500cc.
Ila hata IST inatoboa hadi mwanza bila kulala. sema tu mwendo wake utakuwa wa kawaida usishindane na mabasi au ma VX.
 
Kutoka maelezo ya handsome84, uchakavu wa gari huwezi ona papo kwa hapo ila kudumu kwa gari kutakuwa kwa mda mfupi, ni vizuri kuzingatia uwezo wa gari na uzito wa kazi, kwa uelewa wangu gari ndogo kama ist na passo sio za kuzipigisha safari ndefu mfululizo bila kuzipumzisha
 
What if ukazima baada ya kufika bila kuiacha ingurume kwa nusu saa ..itatikea tatizo gani
Endapo utafika na kuzima gari hapo hapo ambayo imetoka safari ya mbali hali hiyo inaweza kisababisha piston kung'ang'ania kwenye block kumbuka piston zinakuwa zinapishana nyingine zinapanda juu na nyingine zinashuka chini gari iapokuwa inatembea au kupinda cylinder head kumbuka chuma aina ya cast ambacho ndhicho hutengenezea vitu hivi nilivyovitaja vinataboa ya kutanuka vinapopata joto sana na vinatabia kusinyaa kwa ghafla vinapopata baridi hivyo huweza kubana piston vinaposinyaa kwa ghafla au sleav kupinda au hata camshaft kupinda au main na con kulika kwa urahisi ambazo ndizo zinashikilia cam shaft kwa kuwa vyuma vyote vinakuwa na moto sana na unapozima gari kwa ghafla unasababisha oil kushuka kwa kasi kwenye sample kwani inakuwa imeyeyuka sana na ni ya moto hivyo inauwezo wa kupita kwa kasi kwenye matundu yake na kushuka chini na kumbuka wakati huo ukizima gari oil pump ambayo kazi yake ni kupandisha oil juu hadi kwenye cylinder head ili vyuma vyote nilivyovutaja vipate oil ili vilainike vitakosa oil kwani nayo oil pump itazima kwa ghafla na hata kama feni ilikuwa inapuliza nayo itazima kwa gahfla na ndio maana huweza kuleta madhara makubwa kwenye injini. Na sio tu unapofika mwisho wa safari unashauriwa kuzima gari bali hata unapotaka kusafiri safari ya mbali unashauriwa uwashe gari yako kwa dakika 15 kwanza uiache ingurume ili kuweka uwiano sawa wa joto kwenye injini yako ili iweze kukabili safari unayotaka kwenda sio vyema unapotaka kusafiri safari ya mbali hapo hapo unawasha gari na kianza safari yako. Kama una swali zaidi karibu mkuu
 
Asante mkuu nimejifunza kitu kikubwa sana kwako,, nilishaua injini ya gx100 kwa safari ndefu mwendo mkali na kuizima ghafla pindi ninaposimama, japo haikufa siku hizo ila baadae ilopoteza ubora wake, kurudia tena safari ndefu ikanilaza njiani
Napingana nawewe kwenye swala LA 70kph kwann kwanza kabisa hizo gari wasingetoa na speed limit ya 160.wangetoa speed 90 kama ilivyokuwa kwa Volkswagen na Peugeot za zaman.2.barabara Japan na nchi za wenzetu zilizoendelea hatuwezi jifanananisha hata kidogo.cc tunatembea30. 50. Ukibonyeza kidogo 50 hiyo.wenzetu kunamahali huruhusiwi kuendesha chini ya 120kph.

Hili LA kuzima gari baada ya kutoka safari ndefu nakubaliana na wewe.ila nakuuliza MFANO nimetoka mbeya nakuja dar nimefika chalinze gari haItembei tena ule mwendo niliokuwa nao kutoka mbeya -chalinze, sasa natembea 70, 60,20 nafika kimara sasa ndio kusimama na kusogea he nikifika sinza kuna haja ya kuacha gari silence?
 
Nimekuja DM hujanijibu. Kwahyo unataka kunambia ukichukua gari yoyote yenye cc zaidi ya 1500 nikitaka kwenda hata kigoma nitaenda kwa siku moja ????
Ndio unaweza kwenda popote kwa kuwa gari hizo huwa na mfumo mzuri wa upoozwaji wa injini zake na pia ukubwa wa piston zake husaidia kuwa na mapigo machache na gari kuchanganya kwa urahisi bila kusababisha combastion kubwa kwenye injini.kumbuka kuanzia ukubwa wa cc inamaana ndio ukubwa wa rejeta,ndio ukibwa wa feni,ndio ukubwa wa piston nk. Hivyo huwa na mapigo machache na yanayosaidiana kwa uwiano sawa. Mfano piston mbili zikiwa chini mbili zinakuwa juu na hivyo kutoa gap kubwa kwa block kupoozwa vyema na maji yanayopita kwenye injini na kusaidia ufanisi mzuri wa injini yako.
 
Intercooler ni nn?
Naomba nikujibu intercooler ni mfumo wa injini kupoozwa kwa mifumo miwili kwa wakati mmoja mfumo mmoja ni wa kawaida ambao ni wa maji kutoka kwenye rejeta baada ya kupoozwa na feni na mfumo mwingine ndio huu wa intercooler ambao ni wa hewa inayoruhusiwa kupita pia kwenye injini kupitia rejeta ya hewa tu inayoitwa condensor inayokuwa kwenye uwazi unaopatikana kwenye bonet ya gari na kusaidia kupooza zaidi injini kumbuka mfumo huu wa intercooler huwa mara nyingi kwenye bonet ya gari inakuwa na kipande cha nafasi kinachoruhu hewa kupita na kuingia moja kwa moja kwenye injini kipitia condensor hivyo kadiri ya unavyo kimbiza gari yako ndivyo na kiwango cha hewa kinavyoingia kwa wingi zaidi na kuleta ufanisi zaidi wa kupoozwa injini yako kupitoa mfumo huu wa inyercooler ni magari machache sana yenye mfumo huu wa intercooler.
 
Asante mkuu kwa kunielewa vizuri sana. Zingatia watu wenye uwezo huzitumia gari hizi za cc ndogo kwa trip town tu ila siku akiwa na safari ndefu ndipo huamsha gari yenye uwezo mkubwa na kuitumia. Mfano mzuri angalia wachaga kipindi cha december wakienda moshi utaona magari mengi kwenye safari hizo ni yenye uwezo mkubwa hata kama ni gari namba A ila barabarani utashangaa uwezo wake na yanaweza kuhimili kwenda umbali na kwa kasi yoyote wanaohitaji kwenda wamiliki wa magari hayo.au utakuta mtu ana magari matatu moja ni gari kubwa la safari ndefu linatoka tu inapopatikana safari ndefu na trip town zinatumika hizi gari zenye cc ndogo.
 
Mimi nilisafiri na Passo Piston3 kutoka Dar mpaka Mwanza nilitoka Dar saa 9 kama na nusu nikaingia Mwanza saa 2 usiku wala sikupata tatizo lolote njiani wala sikupigwa Tochi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10 na niliendesha mwenyewe muda wote wa safari.
Roughly hapo ni kama 5hours ivi kwa dar-mwanza...kwa passo? Ok sawa
 
Kama unaipa service inavyopasa, IST inafika Mwanza bila shida kabisa.
 
Nakutumia msg PM haujibu mkuu, je MARK II GRAND kwa safari za mikoani vp ???
 
Roughly hapo ni kama 5hours ivi kwa dar-mwanza...kwa passo? Ok sawa
Matano madogo sana mkuu hata dodoma hufiki! Approximately nilitumia kama masaa 16 hivii mpaka kufika Mwanza.
 
Matano madogo sana mkuu hata dodoma hufiki! Approximately nilitumia kama masaa 16 hivii mpaka kufika Mwanza.
Rudi kwenye comment yako ya mwanzo uone ulichoandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…