Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Tumia huu ushauri mkuu
Inatoboa ila sina hakika kama ni moja kwa moja
Huu pia unafaaa mkuu
Inatoboa mwanza mapema sana mkuu hata usiwaze kabisa mwanza mapema sana bila touch mwanza masaa 9
Huu pia mkuu
 
Mimi nilisafiri na Passo Piston3 kutoka Dar mpaka Mwanza nilitoka Dar saa 9 kama na nusu nikaingia Mwanza saa 2 usiku wala sikupata tatizo lolote njiani wala sikupigwa Tochi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10 na niliendesha mwenyewe muda wote wa safari.
Saa 9 ulikuwa unamaanisha saa tatu asubuhi au saa tisa alasiri?
 
From saa tisa alasiri mpaka saa 2 usiku kutokea dar ukawa ushafika pande za nyegezi,uko vizuri mkuu
Sorry mkuu nimerekebisha reply yangu nilikuwa namaanisha saa 9 ya alfajiri samahani sana.
 
Nikueleweshe zaidi mkuu wangu suala la speed kuwekwa 160 au 180 haimaanishi ndio uendeshe kwa mwendo huo pili kwa nchi za wenzetu high way kuendesha ni speed 100 kuendelea au kama huendeshi mwendo huo unatakiwa kuendeshea service road na pia ni mara chache kukuta unaweza kundesha speed 100 au zaidi kwa km 50 au zaidi katika nchi za wenzetu. Lazima utakuta kuna taa,vizuizi nk ila nchini kwetu unaweza kuendesha speed 150 hata km 100 na bila kukuta hizo sheria na vizuizi. Hivyo wenzetu wakiendesha speed 100 akiona gari yake imezidiwa anasogea service road anaendesha mwendo anaotaka kuipimzisha gari yake. Huwa Ninakwenda mara nyingi kununua magari ya wateja wangu wanaponiagiza au magari ya kuweka yard kwangu kuyauza na ninapokuwa nayatest mfano yokohama au tokyo ndipo ninapokutana na hizo sheria za uendeshaji nilizokuambia hapo juu.pia speed ya gari toyota landcruiser mkonga iliyotengenezwa japan original ukiendesha ukiwa speed 100 na gari aina hiyo hiyo toyota landcruiser mkonga iliyotengenezwa afrika kusini ukiendesha speed 100 unaweza ukashangaa toyota original na hii toyota under licence utakuta zinapishana haziendi speed sawa moja itakuwa mbele zaidi ya nyingine Kwa mfano huu naimani utakuwa umenielewa au basi la abiria utakuta lina dashboard ina speed 100 tu ila basi hilo likiwa speed 80 unatashaangaa wewe unaendesha raum uko speed 120 lakini basi linakupita Hivyo dasboad speed sio kipimo tosha cha kujua mwendo unaoendesha ni ule uliooneshwe kwenye spedometer ya gari yako. Au utakuta unaendesha sehemu kuna kibao cha 50 kmph na dashboad yako inasoma 50 kmph ila utapigwa tochi na ukipewa picha ya gari yako utaona inasoma 65 kmph au 70kmph unapigwa fine.hivyo volkswagen akiwa speed 70 utashangaa wewe toyota uko speed 100 na bado mnaenda sawa. Kuna mambo mengi ya kujifunza bado kuhusu gari mkuu

. Nikujibu swali la pili kulingana na foleni haswa unapokuwa unaingia dar kuanzia mlandizi hadi kufika ubungo ni sawa na kuipooza gari yako kama nilivyotoa maekekezo hapo juu kwani foleni na gari iko silence injini inapoozwa vyema unaweza ukafika na kuizima gari yako mkuu.
 
Kuna moja nilisafiri nayo aisee me sio mpenzi wa toyota ila kapo vzuri bana ndani kapo very smart..kanatoboa ukikalazimisha ila uckaoverload. Ila kapo fresh sana yan maana ckutegemea kama kangekua vile..
 
Unaenda tena vzr tu, Mim ninayo hua natoka Mwanza saa mbili asubh naenda Dom saa kumi Au kumi na moja Nipo dom vzr kabsa. Cha msing Fanya service ya oil vzr, hakikisha coolant iko vzr na break. Njian Utakua unapita Kama risasi tu
 
Kuna watu huwa nahisi wanaota humu jf. Ikitoboa service yake atajuta
 
Toka Dar to mwanza ni km 120?????

Dunia imezungukaje hivyo????
 
Hiyo gari ni nzuri sana ,wewe ndo utachoka siyo gari.

Unajua kwa sisi tuliozoea safari Mwanza napaona karibu yaani ni kama vile kutoka home kwangu kwenda sokoni tu.
 
hpo unatoboa mzee vizur kabsa,lkn mi kwa safar za mkoan gar nzur zile zilizojuu,gar zilizochin sana bn huwa zinachosha sana hasa miguu na kiuno,
 
Unaenda hadi mwanza bila kupumzika njiani ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…