Je, tozo za miamala ya simu ni matokeo ya wabunge wa CCM waliopelekwa Bungeni kinguvu?

seedfarm

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
260
Reaction score
2,655
Tuna wabunge dhaifu na wengi wasiojielewa hawa wa CCM waliopita bila kupingwa na kulindwa na Mamlaka. Bungeni hawana uwezo wa kujenga hoja na wala hawana uelewa wa mambo ya Uchumi na Maendeleo.

Tuna wabunge wapiga meza na makofi Bungeni, Hawaelewi ipi ni "a" ndogo na ipi ni "A" kubwa. Wabunge waliopitishwa kinguvu hawajui maana ya kuwa Bungeni wala kwanini wapo Bungeni.

Aina za wabunge kama Gwajima, Bashiru na Humprey wanaelewa nini kuhusu Uchumi na Biashara, Wao kazi yao ni kupiga kelele na vigelegele ndio kazi waliyozoea, Hawana uwezo wa kuelezea mambo ya sheria hata kodi.

Hakuna mbunge wa ccm mwenye uwezo wa kujua Madhara ya maamuzi Katika kukandamiza wananchi, Walipora pesa zote kuwa nunua wafuasi wa chadema kupitia Humprey na Bashiru, Leo nchi ipo taabani haina pesa kabisa.

Leo wapo wana CCM wenyewe Bungeni bila mtu wa kuwakosoa, Hawasomi chochote wanacholetewa na Serikali Bungeni, Hata wakisoma Hawaelewi kitu hivyo ni kazi bure.

Mbunge kama Tale tale na Kibajaji wanaelewa kitu gani kuhusu Uchumi wa dunia na mambo ya diplomasia duniani, Wabunge wengi ni washamba sana sana, Wapo Bungeni kujadili watu.

Bunge la bajeti la kujadili tozo za miamala ya simu lilitumia asilimia 90% ya muda kujadili habari za Magufuli na Mbowe

Sheria ya tozo imepita nao wa nashangaa, Wabunge wa ccm Bungeni walikuwa wanapata u maarufu kwa kudakia hoja zinazoanzishwa na wabunge wa upinzani kama Peter Msigwa na Zito Kabwe.

Leo hii hakuna mbunge mwenye uwezo hata mmoja wa ccm wa kuelezea mambo kama Zitto Kabwe.

Bunge lote la ccm Bungeni ukiwa jumlisha na Dada zao wa viti maalum hawaufikii uwezo wa Zito Kabwe au Peter Msigwa hata kwa asilimia 1%.
 
Lile bunge la wachumia tumbo halina jipya, ni rubber stamp ya serikali, kuna wakati kina Nape walipiga kelele siku hizi naona nao kimya, sijui ndio wameshafungwa mdomo na chama chao.
 
Hivi unategemea kilaza kama babu Tale kutoa hoja ya kutetea wapiga kura wakati hakupigiwa kura? 80% ya Wabunge waliopo mjengoni wameingia kwa mabavu na wizi wa kura ulioratibiwa na vyombo vya dola ili kwenda kumuandalia mwendazake utawala wa kifalme.
 
Nikiwafikiria wabunge wote na mawaziri ninaowafahamu, hakuna hata mmoja ninayeona naweza kuwa ni high IQ. Wengi ni low minds, watu ambao wanaweza kuongeaongea lakini hawawezi kupanga na kutetea chochote kilicho muhimu kwa Taifa kutokana na uwezo wao wa akili kuwa mdogo.

Tunafahamu kuwa ndani ya CCM, wengi ni wajinga na wenye akili ndogo (utafiti wa TWAWEZA), lakini hulka ya marehemu kupendelea kufanya kazi na watu wenye uwezo mdogo wa akili, watu wanafiki, waongo, na wenye uwezo mkubwa wa kushangilia na kusifu, imechangia sana bungeni kuwa na watu wasiotambua chochote kilicho muhimu kwa Taifa.

Kwa ujumla, wala tusitegemee nchi yetu kwenda popote kwa kuwategemea wabunge na hata hawa mawaziri wa sasa. Hapa ni kila mmoja kuhangaika ili maisha yaende lakini kwamba eti nchi itanyanyuka kimaendeleo, kwa kuwategemea hawa wabunge aliowateua marehemu, na baadhi ndiyo mawaziri, tusahau. Kipofu hawezi kumsaidia anayeona kuvuka mto.
 
Unataka kuniambia kuwa Heche ni bora kuliko Bashiru?

Unataka kuniambia kuwa Msigwa ana mantiki kichwani kumzidi Jerry Slaa!! Mkuu tupa Shuka pembeni kumeshakucha tayari.
 
Laana yoye hii impate dikteta magufuli uko jehanam akiunguzwa na moto wa milele.
 
Unataka kuniambia kuwa Heche ni bora kuliko Bashiru?

Unataka kuniambia kuwa Msigwa ana mantiki kichwani kumzidi Jerry Slaa!! Mkuu tupa Shuka pembeni kumeshakucha tayari.

Mkuu na ww umeanza kuwa mchekeshaji lini? Msikilize Bashiru alichokuwa anaaongea wakati wa JK, na alivyokabidhi ubongo wake kwa Magufuli, na kwa sasa yuko kimya maana hajui aseme nini tena. Wakati Bashiru kapewa ukatibu mkuu wa ccm alisema amepata cheo kikubwa sana kiasi kwamba hatakuwa tayari kukubali cheo kingine tena. Mungu si Athumani, akachaguliwa kuwa katibu Mkuu Kiongozi, ulisikia alipoulizwa kuhusu hiki cheo kingine alisemaje? Huyo ndio kiongozi bora?
 
Wachekeshaji ni wale wanaoamini katika substance nyepesi ya wabunge wengi wa upinzani. Huwezi kumlinganisha Bashiru na mbunge yoyote wa upinzani, hicho ndicho kichekesho. Maisha ni fumbo hakuna aijuaye kesho inafanana vipi lakini sio kigezo cha kumlinganisha Bashiru na yoyote wa upinzani kielimu na hata kwenye masuala ya ujenzi wa hoja za aina mbalimbali.
 

Ana elimu lakini nje ya ajira hana uwezo wa kuendesha maisha. Vichekesho vingine bwana. Elimu ya Bashiru ni ya darasani, lakini imedhihirika hapa Tanzania, mwenye Elimu hana tofauti sana na asiye na elimu, na mifano halisi ipo.
 
Ana elimu lakini nje ya ajira hana uwezo wa kuendesha maisha. Vichekesho vingine bwana. Elimu ya Bashiru ni ya darasani, lakini imedhihirika hapa Tanzania, mwenye Elimu hana tofauti sana na asiye na elimu, na mifano halisi ipo.
Ni kweli kabisa,Bashiru anazidiwa mara elfu na kibajaji.
 
Walivyo wajinga, badala ya kuishauri serikali namna bora ya kuelekeza uchumi kipindi hiki kigumu, kama mataifa yanayojielewa yanavyofanya.
Wenyewe, kabla hata ya kura, wakawa wanafifia-sifia tu.
Kisha wakaipigia kura 100%.
Ama kweli, bora ukose mali ila upate akili.
 
Unataka kuniambia kuwa Heche ni bora kuliko Bashiru?

Unataka kuniambia kuwa Msigwa ana mantiki kichwani kumzidi Jerry Slaa!! Mkuu tupa Shuka pembeni kumeshakucha tayari.
Usimfananishe Heche na vitu vya ajabu ajabu. Kwa Basiru bora Prof Majimarefu.
 
Mkuu Mimi ni mwana ccm, Huyo Bashiru Ally wa udsm zamani hamna kitu huyo, Alikuwa anapiga kelele tu pale udsm na Kitila Mkumbo

Angalia utendaji wake kama Katibu Mkuu wa ccm, Hakuna katibu Mkuu wa ccm aliyefanya utoto na siasa za kijinga kama Bashiru wa udsm

1.Alitumia pesa za chama kununua upinzani akisahau upinzani ni itikadi na falsafa hata Nyumbani watoto wako hawawezi kukubaliana na wewe kwa kila kitu hivyo upinzani haufi kwa kuwanunua watu bali hufa kwa kutekeleza mapungufu yanayoongelewa

2.Ni mtu asiyejua anasimamia kitu gani? Ukatili au Haki. Alipofariki Magufuli aliyekuwa anampa kiburi cha Kutishia wana ccm ameufyata kimya kama kobe, Han chembe yeyote ya uongozi bali alibebwa kwa mbeleko na kuwa katibu mkuu kiongozi kwa wiki tatu tu

3.Hao ndio walioharibu hii nchi na kufanya kuwa maskini zaidi mpaka serikali ya Mama wanatafuta pesa kwa nguvu na kuamua kuweka kodi kwenye miamala ya simu bila kichwa wala miguu

Huyo alilazimisha vyombo vya habari kwa vitisho vimsifie Magufuli tu kila kona ya nchi

Huyo alishusha thamani ya magazeti ya nchi na taarifa za habari, Kila siku alilazimisha ziandikwe habari za Madaraja na Reli hata Madaraja yale ya mkoloni walizindua upya
 
Pigia mstari. Hakuna Mhunge hata mmoja kashinda kwa kura za kupigiwa na wananchi. Ndio maana hawaoni hata umuhimu wa kuwatetea. Mamlaka zilizowaweka ndio zenya nguvu juu yao.
 
Wakishapata vyeo zile akili za zamani sijui huwa zinaenda wapi. Njaa mbaya sana
 
Unataka kuniambia kuwa Heche ni bora kuliko Bashiru?

Unataka kuniambia kuwa Msigwa ana mantiki kichwani kumzidi Jerry Slaa!! Mkuu tupa Shuka pembeni kumeshakucha tayari.
Mkuu hatujaona makeke yao mjengoni wametulia tu kuvuna mmishahara na posho.
 
Bashiru is one the very hopeless PhD alchaic. Mchumia tumbo hata ungekuwa na degree saba huwezi kusimamia lolote.

Kuna anayeweza akaniambia kwa uwazi na kwa uhakika, Bashiru wa wakati wa Kikwete, Bashiru katibu mkuu wa CCM na Katibu Mkuu Kiongozi wa wakati wa Magufuli, na Bashiru mbunge wa viti maalum wa wakati wa Samia, kwa wakati wote amesimamia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…