Je, TRA wameruhusiwa kuajiri wenyewe? Tunaenda mbele hatua 2 tunarudi nyuma hatua 10

Mbona halmashauri zina ajiri watendaji, madereva n.k hata kama wako under supervision ya utumishi through kutuma afisa mmoja kama ni mianya ya corruption na nepotism ipo haiwezi kuzibwa.

Pia tamisemi wana ajiri watumishi wa afya, walimu, ma afisa ustawi, wizara ya afya ina ajiri watumishi yenyewe kwa nyakati tofauti mbona sio issue sana why TRA iwe nongwa!?

PSRS imeshindwa kutimiza majukumu yake kwa wakati, wacha taasisi zinazo hitaji watumishi kwa haraka ziajiri zenyewe huku wao wakiendelea na michakato ya miezi nenda rudi kama walivyo zoea.
 
PSRS ni 🚮🚮 kabisa
 
Nimeona tangazo la kazi za TRA. Kwa Sasa inaonekana wataajiri wenyewe bila kupita Utumishi.

Je, watoto wa Mamantilie watapita? Nakumbuka enzi za Dkt. Slaa na majina ya watoto wa vigogo BOT.

Yajayo yanafurahisha.
Ulitaka nani awaajiri.
Ndumbaro alikuwa anaweka ndugu na watoto wa viongozi tu akiwa utumishi.
Tangu 1995 utaratibu wa ajira ni taasisi husika zilikua zinaajiri, alipoingia chizi madarakani akabadilisha utaratibu.
Taasisi zilikua zinaomb vibali vya kuajiri inachukua hata mwaka bila kuvipata kisa tu ndumbaro
 
Tupambanie serikali ifungue fursa zingine. Serikali inaajiri kama watu 600,000 tu kati ya Watz zaidi ya 30m wenye uwezo wa kufanya kazi.
 
Tatizo hii nchi sasa hivi ni kama vile Rushwa imekuja kwa kasi ya Kimbunga. Nlishangaa sana ajira za nafasi ya Polisi zilipotangazwa kuna mdau alitakiwa kutoa milioni moja ili mwanae apate nafasi ya kujiunga. Sasa kama nafasi za Polisi rushwa inatembea sijui kwa TRA na taasisi nyingine itakuwaje.

Kadhalika hizi connection wanazofanyiwa watoto wa viongozi waliopo kwenye mamlaka kupata kazi bila ku-struggle kwenye interview ndio kunasababisha hata kusiwe na mikakati ya ziada kutengeneza ajira kwa vijana nchini. Laiti kama viongozi wangeruhusu fare competition katika ajira basi wangeona ni kwa namna gani vijana wanateseka kutafuta ajira. Watoto wengi wa viongozi hupata kazi tu pale wanapohitimu masomo yao ya chuo ndio maana issue ya high level of unemployment nchini kwao wanaona kawaida tu. Au kiongozi anaongea simple simple tu kuwa vijana wajiajiri. Ila Mwanae unakuta kamtaftia chaka la kazi sehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…